Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Viroba viko kundi gani?

Viroba nadhani ni kati kwa kati, maana kuna vingine havina standard kabisa, mara leo kinalewesha na kesho hakileweshi. Halafu vya magumashi ni vingi sana hapa town, unakumbuka kuna jamaa alikamatwa na mtambo wa kutengeza valuer na konyagi Kimara?

Unaweza kunywa gongo ukidhani ni konyagi.
 
Maziwa ya Kitimoto(nguruwe) upate mtu akukamile kwa usafi.
Unayachemsha vizuri yakipoa anayanywa haichukui mda anaacha kilevi.
 
ni kweli ndugu yangu, baba yangu aliteswa na pombe sana , tulihusunika sana bila kujua la kufanya maana hata harudi nyumbani bila kunywa kwanza, anaamkia bar bila kujali atafukuzwa kazi ambayo wanawe tulikuwa tunaitegemea, LAKINI KISUKari na BLOOD pressure ni kiboko hataki hata kusikia harufu ya pombe achilia mbali kuona chupa tu anahisi pressure na sukari vinapanda sasa kwa kweli hadhi yake katika jamii imeanza kupanda tena ! poleni sana mnaosumbuliwa na walevi!
Nikweli kabisa mi hapa niipo nisipokunywa hata 1 usingizi kupata ni tab sana mara unaota ndoto za ajabu ajabu jamani msaada nami niweze kuacha mtungi.
 
mie na ndugu yangu aliacha baada ya kuliwa boga na mmasai mlinzi...mbaya zaidi yule mmasai aliathirika..

daah..yan he was a very stressful guy..ila ndo maisha ase..kaacha kabiisa ila kisura ukimwangalia kama kalewa bado..due to msongo wa mawazo kila kukicha
 
Jamii forum dr kuna ndugu yangu anasumbuliwa na tatizo la ulevi wa pombe je ni kitu gani afanye kuacha hiyo kitu?

I have a son, he is growing up.... I dont ever want him to see me this way.

I will work on it.

Help me God.

Niliandika haya kwa Mfarisayomtata aliyeomba ushauri mwaka 2012. Ingekuwa vizuri kama angetupa feeback kama alifanikiwa kuacha pombe, alifanyaje mpaka akaacha na whole experience ya kuacha.

Mkuu kabla ya kuamua kuacha kunywa pombe kuna maswali ya awali ya kujiuliza.
1. Kwa nini unataka kuacha kunywa pombe? Watu wanaacha kwa sababu mbalimbali kama ukata etc.
2. Mambo gani mazuri yanatokana na wewe kunywa pombe? Muhimu kujua ili kutafuta njia mbadala baada ya kuacha.
3. Mambo gani mabaya yanayotokana na wewe kunywa pombe?
4. Mambo gani mazuri unayategemea baada ya kuacha kunywa pombe?
5. Mambo gani mabaya yanayoweza kutokana na wewe kuacha kunywa pombe?

Kutokana na majibu ya maswali hapo juu, hizi ni baadhi ya hatua unazoweza kuchukua. Zipo nyingi. Hizi ni baadhi tuu.

1. Kama ni mnywaji sana ongea kwanza na daktari wako. Kuacha pombe ghafla kunaweza kukuletea madhara hasa kama ni mnywaji sana. Kuacha ghafla unaweza kusumbuliwa na panic attacks, anxiety, kutetemeka, mapigo ya moyo kwenda mbio, au hata mwili kupungua mwili/uzito. Kwa hiyo, kunaweza kuwa na umuhimu wa kupata ushauri wa kitaalamu kwanza jinsi ya kuacha.

2. Badilisha attitude yako juu ya pombe. Kumbuka hakuna anayekulazimisha kuacha pombe. Pombe ni rafiki yako mkubwa ambaye amekuwa na wewe kwa muda mrefu. Kwa kumwacha siyo rahisi. Ni sawana kutaka kuachana na mpenzi wako unayempenda sana. Panga tarehe za kuacha. Be ambitious but reasonable. Kama ni mnywaji sana punguza kidogo kidogo. Ukiacha gafla unaweza kuugua ghafla. Ndiyo maana wanasizitiza kupata ushauri wa daktari ili aweze kukupangia kitaalamu jinsi ya kuacha pombe. Wanaotaka kuacha kuvuta sigara wanafanya hivyo hivyo, though mzazi wangu aliamka leo na kusema kuanzia kesho sivuti tena sigara na hajavuta tena mpaka leo.

3. Kama una mazoea ya kuhifadhi pombe nyumbani, get rid all of them. Unaweza kusema itabidi uache pombe kidogo kwa ajili ya wageni. Lakini it is perfectly fine kumpa mgeni chai, soda au hata maji. Kama ni mgeni aliyezoea kuja kwako na kunywa pombe ukimwambia kuwa huna pombe ndani kwa sababu una mkakati wa kuacha kunywa, nadhani atakuelewa vyema. Jenga mazingira ya kutohifadhi pombe nyumbani kwa ajili ya wageni. Wanunulie pombe tuu pale ambapo unajua wanakuja kukutembea, but wazoeshe kunywa soft drinks badala ya pombe. Kwa sie wapenda soka tuna kamtindo ka kununua bia za kunywa na kuweka home, halafu unashushia taratibu na washkaji huku tukiangalia mechi. Kama nawe ni mmoja wao, jaribu kuachana na hiyo tabia.

4. Go back to your feelings. Ukijiskia unataka kulia, then lia (specifically kwa @Karucee). Have a laugh, when you want to. Kula ukiwa na njaa. Kunywa maji mara kwa mara ili usikikie kiu. In fact, kunywa maji mengi yanasaidia ngozi yako kuwa laini. Lala ukiwa umechoka. Usitumie ule muda uliokuwa unautumia kunywa pombe kwa kwenda kulala. Haitasaidia. Mwanzoni itaonekana very weird but embrace it. Kuna uwezekano kwa sababu ya pombe hujawahi kujua hisia zako kwa muda mrefu mno. So, you will have to learn to curve.

5. Usifanye kitu ambacho hauko tayari kukifanya. Kama unaenda kwenye sherehe na kuna pombe usinywe pombe kwa sababu wengine wanakunywa. Mwanzoni inaweza kuwa ngumu lakini you will need to rain check. Protecting your sobriety should be your first priority.

6. Note kuna uwezekano mkubwa wa kuachana kwa muda na baadhi ya marafiki zako ambao ulikuwa unakunywa nao. Baadae utakuja kushangaa kuwa in fact marafiki ambao ulikuwa unakunywa nao walikuwa wanakunywa only occasionally, tena bia mbili tuu wakati wewe ulikuwa unakata bia tano mpaka kumi bila kujua.

7. Kama nyumbani unatumia viungo vya kupikia ambavyo vinalazimisha kuwepo kwa bia au wine, then achana navyo. Pia kuna wale wanaosema kuwa nyama choma haipandi bila bia. Itakubidi ukae mbali na nyama choma kwa muda. Wapo ambao wanachoma nyama na kuichanganya na bia wakati inachomwa. Itabidi uache kama unafanya hivyo.

8. Tafuta kibox kidogo cha mbao cha kuhifadhia fedha. Kila unapofikiria kununua pombe, chukua hizo pesa na tumbukiza humo. Baadae utakujashangaa kiasi cha fedha ambazo ulikuwa unapotezea kwenye pombe. Ikishindikana basi tumia hizo fedha kupunguza stress kama kupata massage au jiunge na gym.

9. Nununua ring ya bei rahisi na ivae kila wakati kama kielelezo kuwa haugusi tena pombe. Kama wewe ni Mkatoliki unaweza kuvaa Rozari kama kielelezo kuwa hutakunywa pombe wakati ukiwa umeivaa. Ukisikia hamu ya pombe tuu look at the ring au hiyo Rozari.

10. Kunywa maji kwa wingi. Hata kama ni kutembea na chupa za maji barabarani usiogope.

11. Omba msaada kutoka kwa ndugu zako, mme/mke, na marafiki wa karibu wasiokunywa kuhusu what you are going through and nini unachotaka ku-achieve.

12. Kama kuna chama chochote cha watu wanaotaka kuacha pombe, jiunge nacho. Kama ukikuta chama chenyewe hakina mshiko, don't feel guilty. Its not your fault. Nakukumbuka hapo nyuma kulikuwa na chama cha kimataifa cha watu wasiokunywa pombe, makao yake makuu yalikuwa Sweden. Kama bado kipo, au kuna chama kininge cha aina hiyo unaweza kuwasiliana nao kwa nia ya kuanzisha tawi hapa Tanzania.

13. Baada ya siku 90 ya kuwa sober, mwonekano wako utabadilika sana na mwili wako utakuwa in full recovery mode. Utakuwa mtu tofauti na ulivyokuwa na kuna uwezekano ukapungua pia. Don't worry.

14. Tengeneza list ya vitu ambavyo umefanya bila kutumia pombe then celebrate maana list itakuwa ndefu sana

15. Furahia how it feel unapokwenda kulala jioni bila kupoteza network.

16. Usijaribu kuwaelezea watu kuhusu kuacha kwako pombe. Watu wengi hawanywi pombe kama walivyokuwa wakinywa zamani. Hawapo kama wewe na hawataweza kukuelewa kuwa una tatizo la kunywa pombe. Of course, wako ambao wana hilo tatizo. Either way kuna uwezekano wakakuambia huna tatizo. Mtu akitaka kukukaribisha pombe mwambie asante lakini nitakunywa soda; najaribu kupunguza weight. Kama ni watu wa karibu ipo siku wataujua ukweli wataku-appreciate kwa kuamua kuachana na pombe.

17. Kubali na kumbuka kuwa pombe sio kitu muhimu maishani mwako kupita vyote.

18. Kuwa na sababu nzuri ya kuacha pombe. Ni muhimu sana kuwa na sababu tena iwe ya msingi. Kama sababu ni pesa imepungua, kuna uwezakano ukarudia tena pombe kama pesa ikiongezeka. So ni bora kuwa na strong and valid reason.

18. Usikwepe kwenda sehemu ambazo utakunywa pombe, kama kwenye sherehe, bar, club, n.k. Badala yake nenda kwenye hizo sehemu ukiwa na attitude nzuri na kumbuka kuwa na good time bila hata kunywa pombe. You can have a good time bila kunywa pombe. Yes, you can from my personal experience. Tena utashangaa jinsi watu na heshima zao wanavyo-behave baada ya kulewa. Kwangu hii ndio sababu pekee iliyonifanya nisinywe pombe until recently baada ya kujihakikishia kuwa I can control when and how much I should drink.

19. Memorize a prayer, shairi, nk then rudia kulisema pale unapokuwa katika hatihati za ku-loose your control. It will keep your heard together. Kwa mfano mtu ambaye anataka kuacha kuchukua rushwa anaweza ku-memorise baadhi ya sentensi kwenye speeches za Mwalimu Nyerere kama "Rushwa ni adui wa haki". Tafuta misemo ambayo inahusina na ulevi.

20. Jipe mwenyewe zawadi kila siku au kila saa kwa kutokunywa. Sio lazima iwe zawadi kubwa. Just a simple treat kujipongeza.

21. Nasistiza tena. Ongea na daktari wako. Kuacha pombe gafla kunaweza kukuletea madhara makubwa hasa kama ni mnywaji wa kupindukia.

22. Fanya mazoezi. Mazoezi yatakufanya u-deal the stress na pia yatasaidia kutuliza ubongo wako na kuboresha afya yako kwa ujumla.

23. Kulingana na ushauri wa daktari, meza vitamin B supplements kila siku kwa wiki ya kwanza ya kuacha pombe. Pombe inaadhiri uwezo wa mwili wako kupokea hivi. Upungufu wa Vitamin B unaweza kusababisha cognitive impairment. So, ongea na daktari wako juu ya hili na hasa kama unatumia medication nyingine.

24. Kama ni mlevi sana jaribu ku-visualize jinsi unatakavyokuwa wakati ukiwa umelewa na jiulize kama unataka kuendelea kuwa vile.

25. Kama unatoka kazini na kwenda moja kwa moja bar kunywa, jaribu kubadilisha routine kwa kufanya shughuli nyingine kama kutembelea ndugu na jamaa, kwenda gym au kanisani/msikitini. Ikishindikana kabisa then, jikite JF. JF is never boring na utafaidika zaidi ya kunywa pombe. Ni heri uwe mlevi ya JF kuliko mlevi wa pombe.

26. Kula kwanza kabla ya kunywa. Hii itapunguza interest ya kutaka kunywa.

27. Siku za mwanzoni punguza kiasi cha pombe unayokunywa. Halafu jaribu ku-imagine kutokana na kunywa mno jinsi unvyopoteza network, unavyojitapikia, kichwa kinauma asubuhi, nyumba inanuka harubu ya pombe uliyokunywa jana yake, unachelewa kazini, nk.

28. Don't give up. Wapo wanaosema wamekuwa wakinywa kwa muda mrefu sana kwa hiyo hawawezi kuacha, sijui wamejaribu kuacha mara nyingi lakini wakashindwa, n.k. Hakuna age limit ya kuacha kunywa pombe. Unaweza kuacha katika umri wowote. bado hujachelewa kuacha pombe.

29. Kama wewe ni mtu wa club sana, kuna strategy alikuwa anatumia rafiki yangu na ilimsadia sana. Kwamba yeye atakuwa dereva kila tukienda out. Kwa hiyo, hatagusa pombe kabisa ili aturudishe nyumani salama salimini. Ilimsaidia sana kutokunywa pombe. Kama una-drive try your best kuto-drive wakati umelewa.

29. Kumbuka kuacha kunywa pombe kutakuongezea urefu wa maisha yako hapa duniani. Pamoja na magojwa yanayosababishwa directly na unywaji wa pombe kupita kiasi, ukiwa mlevi kupindukia unaweza kufanya mambo ya ajabu na kusabisha sio kifo chako tuu bali vifo kwa watu wengine pia kama ku-drive wakati umelewa.

30. Don't let guilty affect you. Unaweza kuji-feel mshamba au guilty kwa kutokunywa pombe lakini usijilaumu mwenyewe au mtu mwingine. Hakuna kitu muhimu kama wewe. You are of no use to anyone kama ukifa na magonjwa yanayosabishwa na ulevi. Lazima ukubali kupambana ili kuipindua the oppressive rule of alcohol na kuanza maisha upya, just as any country in revolution. Jiulize Libya waliweza kuachana na Gadaffi wewe kweli utashindwa kuachana na pombe? It will be hard and you must learn from the past, lakini kumbuka kuwa umedanganywa na pombe kwa muda mrefu. Sasa ni muda wa kuanza kuyaishi maisha yako. Those around you will appreciate it too.

Pombe siyo mbaya kama ukiweza kui-control nadala ya pombe kuku-control. Lakini note kuna hasara za kuacha pombe pia. Kwanza, utaipunguzia serikali mapato ikizingatiwa kuwa mlipaji mkuu wa kodi ni TBL. Pili, @Asprin anaweza akaleta shida.

Goodluck.
 
EMT, you are such an inspiration. I will fight to divorce my 'Forever Fathful'

I believe am a strong woman na sijafika point of no return.

Thank you for your time and effort.

God willing nitakupa feedback.


Good Day.
 
Last edited by a moderator:
EMT, you are such an inspiration. I will fight to divorce my 'Forever Fathful'

I believe am a strong woman na sijafika point of no return.

Thank you for your time and effort.

God willing nitakupa feedback.


Good Day.
pole sana Karucee watu mnataka kuacha wakati wengine ndo tunapanda vyeo!. nimeandika kitabu kinaitwa ifahamu pombe kina sura zifuatazo
Aina za pombe.
Jinsi pombe inavyo fanya kazi.
Hangover na matibabu yake.
Faida na hasara za Unywaji wa pombe.
Unywaji wa pombe wa kupindukia
Jinsi na dawa za kusaidia kuacha pombe
Muingiliano wa pombe na dawa
nimechapisha nakala miatano na pia kwa ajili ya bajeti ndogo kina makosa ya hapa na pale mfano hakina profile ya mwandishi na vitu kama hivyo ambavyo nategemea kurekebisha nikitoa second edition. ila kwa contents waliokisoma wanakikubali sana. nilikuwa mgeni kwenye business nikaja gundua wasambazaji ni walanguzi. mi sasa niko mbeya ila vitabu viko dar .kwa watakaohitaji waseme hapa niwaconnect na msambazaji yuko dar.
 
Mimi nilikuwa mlevi mbwa kwa zaidi ya miaka 10,haiwezi kupita siku 1 bila kunywa tena ile bwii.lakini sasa naweza pita miezi 6,3,4,7 yaani kunywa naamua mm nikanywe cio pombe inaniamuru nanikitaka kuacha naacha ila sitaki kuna kitu nakipenda kwenye pombe sitaacha pombe ila siiruhusu inikontroo yenyewe.
 
Mimi nilikuwa mlevi mbwa kwa zaidi ya miaka 10,haiwezi kupita siku 1 bila kunywa tena ile bwii.lakini sasa naweza pita miezi 6,3,4,7 yaani kunywa naamua mm nikanywe cio pombe inaniamuru nanikitaka kuacha naacha ila sitaki kuna kitu nakipenda kwenye pombe sitaacha pombe ila siiruhusu inikontroo yenyewe.
tulivyo umbwa sio wote tunaaweza kutawaliwa na pombe. pia ipo tofauti ya kunywa kupindukia na kutawaliwa na pombe.
 
UNYWAJI WA POMBE KUPITA KIASI NA KUTAWALIWA NA POMBE
Kawaida watu huanza kunywa pombe kwa kiasi kidogo tu. Baada ya muda hujikuta wanaanza kunywa kupita kiasi na mwisho hujikuta wametawaliwa na pombe. lakini ikumbukwe kuwa si watu wote wanaoanza kunywa pombe watafikia kunywa kupita kiasi au kutawaliwa na pombe. Na pia ikumbukwe kuwa sio watu wote wanaokunywa pombe kupita kiasi wanakuwa wametawaliwa na pombe. kuna mambo mengi yanachangia watu kunywa kupita kiasi au kutawaliwa na pombe. utafiti unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 50 ya unywaji kupita kiasi unasababishwa na kurithi na chini ya asilimia 15 inatokana na sababu za kimazingira. Utafiti mmoja ulionyesha kwamba watoto waliozaliwa na wazazi/mzazi walevi wana uwezekano mara mbili zaidi ya kuwa walevi kuliko wale ambao wazazi wao sio walevi. Pia watoto waliozaliwa na wazazi/mzazi walevi walikuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa walevi hata kama wamelelewa na walezi wasio walevi. Inasemekana kuna aina mbili za unywaji wa kurithi. Ya kwanza ni ile ambayo haina matatizo sana. Aina hii hujionyesha zaidi mtu anapokuwa mtu mzima na anaweza asiwe mlevi akilelewa katika mazingira yafaayo. Aina hii hutokea kwa wanawake na wanaume. Aina ya pili ni ile yenye matatizo sana na huanza mapema ujanani. Ni ngumu mazingira kumbadilisha mtu aliyerithi ulevi wa aina hii.
30
Aina hii hutokea kwa wanaume tu. Pia kuna baadhi ya watu hasa wajamii ya kiasia wamerithi kutopendwa na pombe. watu kama hawa wakinywa hata pombe kidogo hupata madhara na kukosa raha ambayo watu wengine huipata watumiapo pombe. Madhara hayo hujumuisha kichefuchefu na mapigo ya moyo kwenda mbio. Watu wa namna hii huwa ni vigumu kuwa wanywaji wa kupitiliza kiasi na wengi wao hawanywi kabisa.
Sababu zingine zinazoweza wafanya watu watumie pombe sana ni pamoja na msukumo wa marafiki, matatizo ya kifamilia na kiuchumi. Pia jinsi jamii inavyoichukulia pombe nayo ina changia sana. Mfano hapa Tanzania kuna baadhi ya makabila watu wanaanza kutumia pombe tokea wadogo. Jamii hizi huchukulia unywaji wa pombe kama kitu cha kawaida tu. Watu wa kutoka jamii hizo wana hatari ya kuwa wanywaji wa kupindukia. Sababu za kisaikolojia pia zinahusika. Mfano mtu anaweza kuwa anatumia pombe ili kutoa hasira au huzuni. Mtu huyu hasira ikimuisha au huzuni ikimtoka mara baada ya kutumia pombe kuna uwezekano mkubwa wa kutumia tena pombe hata akipata hasira/huzuni kidogo. Kitendo hiki kinaweza mfanya awe mlevi wa kupindukia. sababu nyingine ni magumu ya maisha. Watu waliopitia magumu ya maisha kama vile kukosa kazi, kubakwa, kunyanyaswa utotoni na mambo kama hayo wanauwezekano mkubwa wa kuwa wanywaji kupita kiasi. Magonjwa ya akili nayo yanachangia kwa kiasi kikubwa watu kutumia pombe kupita kiasi. Magonjwa kama sonona (ugonjwa wa huzuni na kuhisi upweke) au kuchanganyikiwa (schizophrenia) yanachangia sana unywaji wa pombe.
31
wagonjwa hawa mara nyingi hutumia pombe ili kupunguza madhara ya magonjwa yao. Mfano mtu mwenye sonona anaweza akajisikia upweke umemtoka na huzuni imemtoka baada ya kutumia pombe. kitendo hiki kitamfanya awe anatumia pombe mara kwa mara. Baada
ya
 
Baada ya kuona vitu vinavyosababisha unywaji wa kupindukia hebu tuone jinsi ya kumtambua mtu mwenye tatizo la unywaji wa pombe. Kama we ni mnywaji wa pombe hebu jaribu kujibu maswali yafuatayo: 1.je umewahi kufikiria kuacha pombe? (a). ndiyo (b). hapana 2. je umewahi chukizwa na watu kukusema/kukushutumu kuhusu unywaji wako wa pombe? (a). ndiyo (b). hapana 3. je umewahi sutwa na dhamira au kujutia unywaji wako wa pombe? (a). ndiyo (b). hapana 4. je umewahi kunywa pombe asubuhi ili kutoa hangover? (a). ndiyo (b). hapana
Kama umejibu ndiyo kwa maswali mawili au zaidi hapo juu basi ujue unywaji wako wa pombe una matatizo. Ujue unakunywa
32
kupita kiasi lakini sio lazima uwe umetawaliwa na pombe. watu wenye unywaji wenye matatizo/unywaji kupita kiasi wanakuwa na dalili zifuatazo. 1. huendelea kunywa hata kama unywaji wa pombe unasababisha mtu ashindwe kutimiza majukumu yake. Majukumu hayo yanaweza kuwa ya kifamilia, kikazi au kishule/chuo. Mtu anaweza asifike kazini au anachelewa kwa sababu ya unywaji wa pombe. 2. kuendelea kutumia pombe hata katika mazingira ya hatari. Mfano mtu anaweza kutumia pombe huku akijua anatakiwa kuendesha gari au kufanya kazi inayohitaji umakini mkubwa. 3. kuendelea kutumia pombe hata kama inamletea matatizo ya kisheria. Mfano mtu anaweza kupelekwa polisi kwa sababu ya ugomvi uliosababishwa na ulevi zaidi ya mara moja lakini asiache au kupunguza kunywa. 4. kuendelea na unywaji wa pombe hata kama unakuletea matatizo katika familia na jamii kwa ujumla.
Hapa tumeona watu ambao wanakunywa kupita kiasi. Watu wengi wakitoka katika hatua ya kunywa kupita kiasi huingia hatua ya kutawaliwa na pombe (utumwa wa pombe). watu hawa ni kana kwamba hawawezi kuishi bila pombe. mtu aliye tawaliwa sana na pombe kwakweli anaweza kufa iwapo akiikosa kwa muda mrefu. Watu hawa huhitaji uangalizi wa karibu wa daktari pindi wanapotaka kuacha pombe. kuna aina kuu nne za kutawaliwa na pombe.
33
1. aina ya kwanza ni ile mtu kuwa na hamu kubwa sana ya pombe. mtu anakuwa anatamani pombe kiasi kwamba anakuwa anashindwa kufanya majukumu mengine bila kuipata. Mtu wa aina hii atafanya juu chini kuhakikisha anapata pombe. 2. aina ya pili ya kutawaliwa na pombe ni kushindwa kujizuia. Watu wa aina hii wakishaanza kunywa ni vigumu kuacha mpaka wawe wamezima au wameishiwa hela. Hii inaweza pelekea kusababisha kifo. Sababu kadri unavyokunywa sana ndio unajisahau kwamba unapitiliza kipimo. Watu wengi wa aina hii hufa kutokana na moyo kushindwa kufanya kazi na kushindwa kupumua. 3. aina ya tatu ni ile hali ya pombe kutawala mwili. Hapa ni kwamba mwili wa mtu hauwezi kufanya kazi kama kawaida bila pombe. mtu akikosa pombe anakuwa kama anaumwa. Dalili ambazo humtokea mtu wa aina hii akikosa pombe ni pamoja na: kichefuchefu, kutoka jasho kwa wingi, kutetemeka na kutototulia ( kuwa na mawenge). Watu wa aina hii ndio huhitaji uangalizi wa karibu zaidi wa daktari pindi wanapotaka kuacha pombe. 4. aina ya nne ni ile hali ambayo mtu anakua sugu wa pombe. mtu wa aina hii huwa anahitaji kiasi kikubwa zaidi cha pombe ili kulewa kadri siku zinavyoenda. Baada ya kuona aina zakutawaliwa na pombe hebu sasa tuone sifa/dalili anazoonyesha mtu aliyetawaliwa na pombe.
 
Watu wengi wamefanikiwa kuacha pombe kwa juhudi zao wenyewe na wengine kupitia msaada wa wataalamu mbalimbali. Kuna watu wanaojiunga ili kusaidiana katika kuacha pombe. moja ya kikundi maarufu ambacho kimeenea duniani kinaitwa alcoholics anonymous (AA). Katika kikundi hiki watu wanaotaka kuacha pombe hukutana na kubadilishana uzoefu na mbinu za kuacha pombe. kuacha pombe linaweza kuwa jambo gumu hivyo inashauriwa kulifanya taratibu. Unaanza kwa kupunguza kiasi unachokunywa taratibu mpaka unafikia kuacha kabisa. Usikatishwe tamaa ukiona unarudi nyuma mara kwa mara kwani ni jambo la kawaida katika kuacha tabia au zoea lolote lile. Ukishindwa kuacha basi unaweza kupunguza kwani unywaji kiasi huwa hauna madhara isipokuwa ukiwa mjamzito au ukishauriwa na mtalaamu wa afya. Zifuatazo ni mbinu mbalimbali ambazo zinatumika kupunguza au kuacha kabisa unywaji wa pombe. 1. tafuta kinywaji mbadala wa pombe kama vile chai au kahawa.
38
2.tafuta vitu mbadala vya kufanya kwa wakati ambao unakuwa unakunywa pombe kama vile kusoma vitabu, kuangalia filamu, kushiriki katika michezo au mazoezi. 3.tumia pesa ambazo unaziokoa kutoka kwenye pombe kwa kujiburudisha kama vile kula vizuri au kununua vifaa vya nyumbani. Hii itakusaidia sana katika kuona umuhimu wa kuacha pombe. 4.jiwekee mkakati kabla ya kwenda kunywa kuhusu kiasi utakachoenda kunywa na pesa utakayotumia. Usibebe pesa zaidi ya uliyopanga kutumia. 5. tumia glasi ndogo wakati wa kunywa na tumia vinywaji vyenye nguvu ndogo. Utafiti unaonyesha watu hunywa zaidi wakitumia glasi kubwa kuliko wakitumia glasi ndogo. 6.kunywa maji kabla hujaanza kunywa pombe. na unavyokuwa unakunywa pombe hakikisha unakuwa na maji ya kunywa karibu na uyatumie mara kwa mara. 7.jaribu kuepuka vishawishi vya kunywa. Watu wengi huwa tunashawishika kunywa kwenye mazingira fulani au tukiwa na watu fulani. Unachotakiwa ni kugundua ni vishawishi vipi hukufanya unywe na uanze kuviepuka.
8.kuwa na msimamo. Watu wengi ambao hujaribu kuacha pombe hukutana na wakati mgumu wanapopata ofa toka kwa marafiki. Njia sahihi ni kukataa bila kusitasita. Kusitasita kunaweza kukufanya uteteleke katika msimamo wako. Ni vizuri ukatafuta sababu ya kukataa ofa mapema kabla hata ya
39
kukutana na ofa. Mfano, unaweza ukasema sinywi au siongezi pombe nyingine kwa sababu nataka kupunguza uzito au sababu nyingine ambayo utakuwa umeitengeneza kama ulinzi wako. 9.epuka kunywa pombe ukiwa na kiu au njaa. Hii inapunguza kiasi cha pombe ambacho kitaingia kwenye damu hivyo utapunguza madhara yake. Pia inasaidia kupunguza kasi ya mtu kuwa mraibu/teja wa pombe. 10.hakikisha ndugu na marafiki wanajua kwamba umedhamiria kuacha pombe. hii itasaidia kupata msaada kutoka kwao pia hawatakuwa wanakushawishi sana unywe. Pia hili linaweza kukusaidia kupata marafiki wapya kwani changamoto mojawapo ya kuacha pombe ni kupoteza marafiki. 11. kama unakunywa kwa kutumia glasi hakikisha kinywaji kimeisha kabisa ndo uongeze tena. Hii itakusaidia kujua ni kiasi gani cha pombe ulichotumia. Kuna watu ambao mbinu hizo hapo juu zimeshindwa kabisa kuwasaidia kuacha pombe. msaada pekee ambao hubaki kwa watu hao ni kutumia dawa. Mara nyingi watu hawa ni wale ambao wanakuwa wametawaliwa sana na pombe na hupata madhara mara waachapo. Matibabu ya watu hawa hufuata hatua tatu muhimu.
1.hatua ya kwanza ni kutibu madhara yatokanayo na kuacha pombe. tumeshaona baadhi ya dawa zitumikazo kutibu madhara yatokanayo na kuacha pombe huko juu.
40
2.hatua ya pili ni kumsaidia mtu huyu kutotumia pombe. hatua hii ndio mara nyingi hutumia dawa. Tutaona dawa hizo hivi punde. Kumbuka kwamba dawa za kumsaidia mtu kutotumia pombe ni tofauti na zile za kutibu madhara yatokanayo na kuacha pombe. 3.hatua ya tatu ni kumsaidia mtu huyu asirudie tena kunywa pombe. Kuna dawa nyingi ambazo hutumika kusaidia watu kuacha pombe. baadhi ya dawa hizo ni kama disulfiram, fluoxetine ambayo kwa kawaida ni dawa ya sonona(depression). Dawa zingine ni pamoja na ondasentron, acamprosate, setraline na topiramate. Katika dawa zote disulfiram ndio imetokea kuwa maarufu sana na ndio tutakayo izungumzia sana katika kitabu hiki. Disulfiram ni dawa ambayo mtu akiitumia halafu akatumia pombe hupata madhara ambayo yatamfanya asitumie/asitamani pombe. ni kama vile kula yamini. Mtu anayetumia dawa hii huelezwa kwa undani madhara yatakayo mpata akitumia pombe. kwa kuogopa madhara mtu huyu hawezi kutumia pombe. toka mtu atumie dawa hii hatakiwi kutumia pombe hata kidogo ndani ya siku kumi na nne (wiki mbili) vinginevyo atapata madhara. Pombe hata inayopatikana kwenye vipodozi vya kupaka na mouth washes (dawa za maji za kusafisha kinywa) inaweza kusababisha madhara makubwa. Uzuri ni kwamba madhara haya hayaui na huisha yenyewe japokuwa mtu anaweza hitaji uangalizi wa mtaalamu wa afya kumpunguzia madhara ayapatayo.
41
Madhara yanayoweza mpata mtu akitumia pombe na disulfiram ni kama yafuatayo. Kuvimba uso, maumivu makali ya kichwa, kupata tabu kupumua, kichefuchefu, kutapika sana, kutoka jasho kwa wingi, kiu kali, maumivu ya kifua, moyo kwenda mbio, kushindwa kuona vizuri na kuchanganyikiwa. Watu wenye magonjwa ya moyo na magonjwa ya akili hawapaswi kutumia disulfiram kwa sababu inaweza sababisha madhara yanayoweza kuhatarisha maisha yao. Pia tuliona mwanzoni kuwa watu waliotawaliwa sana na pombe wakiacha ghafla wanaweza pata madhara yanayoweza kuhatarisha maisha yao. Watu hawa wanapaswa kutumia dawa hii kwa uangalifu wa karibu sana wa wataalamu wa afya. Pamoja na madhara ambayo mtu anaweza kuyapata atumiapo disulfiram na pombe pia disulfiram peke yake kama dawa ina madhara yake. Disulfiram inaweza kusababisha hali ya kuchoka na kujisikia kulala lala, kizunguzungu, matatizo ya tumbo, kuhisi ladha kama ya chuma mdomoni, harufu ya mwili na pumzi. Pia dawa hii ilionyesha kwamba inaweza punguza uwezo wa kufanya tendo la ndoa. Lakini pia utafiti ulionesha kwamba utumiaji wa pombe kupita kiasi unamadhara zaidi ya disulfiram katika kupunguza uwezo wa kufanya tendo la ndoa.
Pia madhara kama yatokanayo na kutumia disulfiram na pombe mtu anaweza akayapata akitumia dawa nyinginezo na pombe. dawa hizo ni kama metronidazole ambayo Tanzania hujulikana zaidi kwa jina la fragyl na dawa za kisukari kama chlopropamide, tolbutamide na tolazamide. J
 
Ha ha ha! We jamaa ni noma, umenikumbusha wakati najaribu kupunguza pombe, ilikuwa inabidi nilale na vikopo 2 vya safari.

Ila inawezekana, unaanza kwa kutokunywa katikati ya wiki, then baadaye unaskip baadhi ya weekends mwisho unashangaa mwezi unapita.

Mind you! Ni rahisi kuacha pombe kama hutumii pombe za kienyeji, ukishaanza kutumia pombe za kianyeji ujue wewe kuacha pombe tena ni issue. (Zile pombe ni kama zinawekewa dawa ili uendelee kuwa mteja)

Hata hiyo katikati ya wiki unaanzaje kuacha? Mimi nimejaribu sana angalau kuacha katikati ya wiki bado sijafanikiwa.
 
Alcoholism ni ugonjwa tena ni ugonjwa mbaya sana pengine kuliko mengine yote. Binafsi nilikuwa na hilo tatizo, na kilichonisaidia wakati naishi ughaibuni kuna siku nilipatwa na DUI. Nikawekwa ndani kwa masaa 24. Judge aliamuru ni-attend alcohol class. Elimu niliyoipata huko ilinisaidia sana. Namshukuru Mungu hilo darasa lilinisaidia sana.
Kumbuka: mtu yoyote yule anaweza akawa alcoholic! Haijalishi uwe maskini, tajiri, mwanaume ama mwanamke.
Dawa ya alcoholism ni kuacha pombe. Period! Kama huwezi fomrmula yake ni 1, 2, 3 = 14
The magic number is 14.
Kama huwezi unatakiwa kunywa 2 drinks, one after one hour and not more than 2 drinks a day=14 a week.
Nitarudi kwa elimu zaidi
 
nami pia nahitaji msaada, nimeombewa sana, na naweza pita wiki kabisa sina hamu nayo, ila siku inatokea tu nimekaa na marafiki basi kiu kinakuja na nikipiga hapo mpaka kreti liishe au grants za kutosha, ninapenda sana kuacha, tena sometime hata kama hela huna ulishawazoesha kuwatoa washikaji basi na wao wanakutoa pia.
 
Du! apa naona mnapeana mbinu za kupunguza mapato ya serekali!!, ila ata mm mbinu izi nitazutumia nipunguze kilaji
 
nami pia nahitaji msaada, nimeombewa sana, na naweza pita wiki kabisa sina hamu nayo, ila siku inatokea tu nimekaa na marafiki basi kiu kinakuja na nikipiga hapo mpaka kreti liishe au grants za kutosha, ninapenda sana kuacha, tena sometime hata kama hela huna ulishawazoesha kuwatoa washikaji basi na wao wanakutoa pia.
nikuuzie kitabu hicho hapo juu?
 
Back
Top Bottom