elimuplatform
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 1,054
- 462
Rehab ndyo nini tena
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
nazani hata ndugu yangu alikuwa na tatizo kama hilohilo na akashauliwa atumie maziwa ya mbuzi.
Nb: Haya maziwa yatapunguza utumiaji wa pombe na sio kuacha kabsa
enjoy++
Viroba viko kundi gani?
Nikweli kabisa mi hapa niipo nisipokunywa hata 1 usingizi kupata ni tab sana mara unaota ndoto za ajabu ajabu jamani msaada nami niweze kuacha mtungi.ni kweli ndugu yangu, baba yangu aliteswa na pombe sana , tulihusunika sana bila kujua la kufanya maana hata harudi nyumbani bila kunywa kwanza, anaamkia bar bila kujali atafukuzwa kazi ambayo wanawe tulikuwa tunaitegemea, LAKINI KISUKari na BLOOD pressure ni kiboko hataki hata kusikia harufu ya pombe achilia mbali kuona chupa tu anahisi pressure na sukari vinapanda sasa kwa kweli hadhi yake katika jamii imeanza kupanda tena ! poleni sana mnaosumbuliwa na walevi!
Jamii forum dr kuna ndugu yangu anasumbuliwa na tatizo la ulevi wa pombe je ni kitu gani afanye kuacha hiyo kitu?
I have a son, he is growing up.... I dont ever want him to see me this way.
I will work on it.
Help me God.
Mkuu kabla ya kuamua kuacha kunywa pombe kuna maswali ya awali ya kujiuliza.
1. Kwa nini unataka kuacha kunywa pombe? Watu wanaacha kwa sababu mbalimbali kama ukata etc.
2. Mambo gani mazuri yanatokana na wewe kunywa pombe? Muhimu kujua ili kutafuta njia mbadala baada ya kuacha.
3. Mambo gani mabaya yanayotokana na wewe kunywa pombe?
4. Mambo gani mazuri unayategemea baada ya kuacha kunywa pombe?
5. Mambo gani mabaya yanayoweza kutokana na wewe kuacha kunywa pombe?
Kutokana na majibu ya maswali hapo juu, hizi ni baadhi ya hatua unazoweza kuchukua. Zipo nyingi. Hizi ni baadhi tuu.
1. Kama ni mnywaji sana ongea kwanza na daktari wako. Kuacha pombe ghafla kunaweza kukuletea madhara hasa kama ni mnywaji sana. Kuacha ghafla unaweza kusumbuliwa na panic attacks, anxiety, kutetemeka, mapigo ya moyo kwenda mbio, au hata mwili kupungua mwili/uzito. Kwa hiyo, kunaweza kuwa na umuhimu wa kupata ushauri wa kitaalamu kwanza jinsi ya kuacha.
2. Badilisha attitude yako juu ya pombe. Kumbuka hakuna anayekulazimisha kuacha pombe. Pombe ni rafiki yako mkubwa ambaye amekuwa na wewe kwa muda mrefu. Kwa kumwacha siyo rahisi. Ni sawana kutaka kuachana na mpenzi wako unayempenda sana. Panga tarehe za kuacha. Be ambitious but reasonable. Kama ni mnywaji sana punguza kidogo kidogo. Ukiacha gafla unaweza kuugua ghafla. Ndiyo maana wanasizitiza kupata ushauri wa daktari ili aweze kukupangia kitaalamu jinsi ya kuacha pombe. Wanaotaka kuacha kuvuta sigara wanafanya hivyo hivyo, though mzazi wangu aliamka leo na kusema kuanzia kesho sivuti tena sigara na hajavuta tena mpaka leo.
3. Kama una mazoea ya kuhifadhi pombe nyumbani, get rid all of them. Unaweza kusema itabidi uache pombe kidogo kwa ajili ya wageni. Lakini it is perfectly fine kumpa mgeni chai, soda au hata maji. Kama ni mgeni aliyezoea kuja kwako na kunywa pombe ukimwambia kuwa huna pombe ndani kwa sababu una mkakati wa kuacha kunywa, nadhani atakuelewa vyema. Jenga mazingira ya kutohifadhi pombe nyumbani kwa ajili ya wageni. Wanunulie pombe tuu pale ambapo unajua wanakuja kukutembea, but wazoeshe kunywa soft drinks badala ya pombe. Kwa sie wapenda soka tuna kamtindo ka kununua bia za kunywa na kuweka home, halafu unashushia taratibu na washkaji huku tukiangalia mechi. Kama nawe ni mmoja wao, jaribu kuachana na hiyo tabia.
4. Go back to your feelings. Ukijiskia unataka kulia, then lia (specifically kwa @Karucee). Have a laugh, when you want to. Kula ukiwa na njaa. Kunywa maji mara kwa mara ili usikikie kiu. In fact, kunywa maji mengi yanasaidia ngozi yako kuwa laini. Lala ukiwa umechoka. Usitumie ule muda uliokuwa unautumia kunywa pombe kwa kwenda kulala. Haitasaidia. Mwanzoni itaonekana very weird but embrace it. Kuna uwezekano kwa sababu ya pombe hujawahi kujua hisia zako kwa muda mrefu mno. So, you will have to learn to curve.
5. Usifanye kitu ambacho hauko tayari kukifanya. Kama unaenda kwenye sherehe na kuna pombe usinywe pombe kwa sababu wengine wanakunywa. Mwanzoni inaweza kuwa ngumu lakini you will need to rain check. Protecting your sobriety should be your first priority.
6. Note kuna uwezekano mkubwa wa kuachana kwa muda na baadhi ya marafiki zako ambao ulikuwa unakunywa nao. Baadae utakuja kushangaa kuwa in fact marafiki ambao ulikuwa unakunywa nao walikuwa wanakunywa only occasionally, tena bia mbili tuu wakati wewe ulikuwa unakata bia tano mpaka kumi bila kujua.
7. Kama nyumbani unatumia viungo vya kupikia ambavyo vinalazimisha kuwepo kwa bia au wine, then achana navyo. Pia kuna wale wanaosema kuwa nyama choma haipandi bila bia. Itakubidi ukae mbali na nyama choma kwa muda. Wapo ambao wanachoma nyama na kuichanganya na bia wakati inachomwa. Itabidi uache kama unafanya hivyo.
8. Tafuta kibox kidogo cha mbao cha kuhifadhia fedha. Kila unapofikiria kununua pombe, chukua hizo pesa na tumbukiza humo. Baadae utakujashangaa kiasi cha fedha ambazo ulikuwa unapotezea kwenye pombe. Ikishindikana basi tumia hizo fedha kupunguza stress kama kupata massage au jiunge na gym.
9. Nununua ring ya bei rahisi na ivae kila wakati kama kielelezo kuwa haugusi tena pombe. Kama wewe ni Mkatoliki unaweza kuvaa Rozari kama kielelezo kuwa hutakunywa pombe wakati ukiwa umeivaa. Ukisikia hamu ya pombe tuu look at the ring au hiyo Rozari.
10. Kunywa maji kwa wingi. Hata kama ni kutembea na chupa za maji barabarani usiogope.
11. Omba msaada kutoka kwa ndugu zako, mme/mke, na marafiki wa karibu wasiokunywa kuhusu what you are going through and nini unachotaka ku-achieve.
12. Kama kuna chama chochote cha watu wanaotaka kuacha pombe, jiunge nacho. Kama ukikuta chama chenyewe hakina mshiko, don't feel guilty. Its not your fault. Nakukumbuka hapo nyuma kulikuwa na chama cha kimataifa cha watu wasiokunywa pombe, makao yake makuu yalikuwa Sweden. Kama bado kipo, au kuna chama kininge cha aina hiyo unaweza kuwasiliana nao kwa nia ya kuanzisha tawi hapa Tanzania.
13. Baada ya siku 90 ya kuwa sober, mwonekano wako utabadilika sana na mwili wako utakuwa in full recovery mode. Utakuwa mtu tofauti na ulivyokuwa na kuna uwezekano ukapungua pia. Don't worry.
14. Tengeneza list ya vitu ambavyo umefanya bila kutumia pombe then celebrate maana list itakuwa ndefu sana
15. Furahia how it feel unapokwenda kulala jioni bila kupoteza network.
16. Usijaribu kuwaelezea watu kuhusu kuacha kwako pombe. Watu wengi hawanywi pombe kama walivyokuwa wakinywa zamani. Hawapo kama wewe na hawataweza kukuelewa kuwa una tatizo la kunywa pombe. Of course, wako ambao wana hilo tatizo. Either way kuna uwezekano wakakuambia huna tatizo. Mtu akitaka kukukaribisha pombe mwambie asante lakini nitakunywa soda; najaribu kupunguza weight. Kama ni watu wa karibu ipo siku wataujua ukweli wataku-appreciate kwa kuamua kuachana na pombe.
17. Kubali na kumbuka kuwa pombe sio kitu muhimu maishani mwako kupita vyote.
18. Kuwa na sababu nzuri ya kuacha pombe. Ni muhimu sana kuwa na sababu tena iwe ya msingi. Kama sababu ni pesa imepungua, kuna uwezakano ukarudia tena pombe kama pesa ikiongezeka. So ni bora kuwa na strong and valid reason.
18. Usikwepe kwenda sehemu ambazo utakunywa pombe, kama kwenye sherehe, bar, club, n.k. Badala yake nenda kwenye hizo sehemu ukiwa na attitude nzuri na kumbuka kuwa na good time bila hata kunywa pombe. You can have a good time bila kunywa pombe. Yes, you can from my personal experience. Tena utashangaa jinsi watu na heshima zao wanavyo-behave baada ya kulewa. Kwangu hii ndio sababu pekee iliyonifanya nisinywe pombe until recently baada ya kujihakikishia kuwa I can control when and how much I should drink.
19. Memorize a prayer, shairi, nk then rudia kulisema pale unapokuwa katika hatihati za ku-loose your control. It will keep your heard together. Kwa mfano mtu ambaye anataka kuacha kuchukua rushwa anaweza ku-memorise baadhi ya sentensi kwenye speeches za Mwalimu Nyerere kama "Rushwa ni adui wa haki". Tafuta misemo ambayo inahusina na ulevi.
20. Jipe mwenyewe zawadi kila siku au kila saa kwa kutokunywa. Sio lazima iwe zawadi kubwa. Just a simple treat kujipongeza.
21. Nasistiza tena. Ongea na daktari wako. Kuacha pombe gafla kunaweza kukuletea madhara makubwa hasa kama ni mnywaji wa kupindukia.
22. Fanya mazoezi. Mazoezi yatakufanya u-deal the stress na pia yatasaidia kutuliza ubongo wako na kuboresha afya yako kwa ujumla.
23. Kulingana na ushauri wa daktari, meza vitamin B supplements kila siku kwa wiki ya kwanza ya kuacha pombe. Pombe inaadhiri uwezo wa mwili wako kupokea hivi. Upungufu wa Vitamin B unaweza kusababisha cognitive impairment. So, ongea na daktari wako juu ya hili na hasa kama unatumia medication nyingine.
24. Kama ni mlevi sana jaribu ku-visualize jinsi unatakavyokuwa wakati ukiwa umelewa na jiulize kama unataka kuendelea kuwa vile.
25. Kama unatoka kazini na kwenda moja kwa moja bar kunywa, jaribu kubadilisha routine kwa kufanya shughuli nyingine kama kutembelea ndugu na jamaa, kwenda gym au kanisani/msikitini. Ikishindikana kabisa then, jikite JF. JF is never boring na utafaidika zaidi ya kunywa pombe. Ni heri uwe mlevi ya JF kuliko mlevi wa pombe.
26. Kula kwanza kabla ya kunywa. Hii itapunguza interest ya kutaka kunywa.
27. Siku za mwanzoni punguza kiasi cha pombe unayokunywa. Halafu jaribu ku-imagine kutokana na kunywa mno jinsi unvyopoteza network, unavyojitapikia, kichwa kinauma asubuhi, nyumba inanuka harubu ya pombe uliyokunywa jana yake, unachelewa kazini, nk.
28. Don't give up. Wapo wanaosema wamekuwa wakinywa kwa muda mrefu sana kwa hiyo hawawezi kuacha, sijui wamejaribu kuacha mara nyingi lakini wakashindwa, n.k. Hakuna age limit ya kuacha kunywa pombe. Unaweza kuacha katika umri wowote. bado hujachelewa kuacha pombe.
29. Kama wewe ni mtu wa club sana, kuna strategy alikuwa anatumia rafiki yangu na ilimsadia sana. Kwamba yeye atakuwa dereva kila tukienda out. Kwa hiyo, hatagusa pombe kabisa ili aturudishe nyumani salama salimini. Ilimsaidia sana kutokunywa pombe. Kama una-drive try your best kuto-drive wakati umelewa.
29. Kumbuka kuacha kunywa pombe kutakuongezea urefu wa maisha yako hapa duniani. Pamoja na magojwa yanayosababishwa directly na unywaji wa pombe kupita kiasi, ukiwa mlevi kupindukia unaweza kufanya mambo ya ajabu na kusabisha sio kifo chako tuu bali vifo kwa watu wengine pia kama ku-drive wakati umelewa.
30. Don't let guilty affect you. Unaweza kuji-feel mshamba au guilty kwa kutokunywa pombe lakini usijilaumu mwenyewe au mtu mwingine. Hakuna kitu muhimu kama wewe. You are of no use to anyone kama ukifa na magonjwa yanayosabishwa na ulevi. Lazima ukubali kupambana ili kuipindua the oppressive rule of alcohol na kuanza maisha upya, just as any country in revolution. Jiulize Libya waliweza kuachana na Gadaffi wewe kweli utashindwa kuachana na pombe? It will be hard and you must learn from the past, lakini kumbuka kuwa umedanganywa na pombe kwa muda mrefu. Sasa ni muda wa kuanza kuyaishi maisha yako. Those around you will appreciate it too.
Pombe siyo mbaya kama ukiweza kui-control nadala ya pombe kuku-control. Lakini note kuna hasara za kuacha pombe pia. Kwanza, utaipunguzia serikali mapato ikizingatiwa kuwa mlipaji mkuu wa kodi ni TBL. Pili, @Asprin anaweza akaleta shida.
Goodluck.
pole sana Karucee watu mnataka kuacha wakati wengine ndo tunapanda vyeo!. nimeandika kitabu kinaitwa ifahamu pombe kina sura zifuatazoEMT, you are such an inspiration. I will fight to divorce my 'Forever Fathful'
I believe am a strong woman na sijafika point of no return.
Thank you for your time and effort.
God willing nitakupa feedback.
Good Day.
tulivyo umbwa sio wote tunaaweza kutawaliwa na pombe. pia ipo tofauti ya kunywa kupindukia na kutawaliwa na pombe.Mimi nilikuwa mlevi mbwa kwa zaidi ya miaka 10,haiwezi kupita siku 1 bila kunywa tena ile bwii.lakini sasa naweza pita miezi 6,3,4,7 yaani kunywa naamua mm nikanywe cio pombe inaniamuru nanikitaka kuacha naacha ila sitaki kuna kitu nakipenda kwenye pombe sitaacha pombe ila siiruhusu inikontroo yenyewe.
Ha ha ha! We jamaa ni noma, umenikumbusha wakati najaribu kupunguza pombe, ilikuwa inabidi nilale na vikopo 2 vya safari.
Ila inawezekana, unaanza kwa kutokunywa katikati ya wiki, then baadaye unaskip baadhi ya weekends mwisho unashangaa mwezi unapita.
Mind you! Ni rahisi kuacha pombe kama hutumii pombe za kienyeji, ukishaanza kutumia pombe za kianyeji ujue wewe kuacha pombe tena ni issue. (Zile pombe ni kama zinawekewa dawa ili uendelee kuwa mteja)
nikuuzie kitabu hicho hapo juu?nami pia nahitaji msaada, nimeombewa sana, na naweza pita wiki kabisa sina hamu nayo, ila siku inatokea tu nimekaa na marafiki basi kiu kinakuja na nikipiga hapo mpaka kreti liishe au grants za kutosha, ninapenda sana kuacha, tena sometime hata kama hela huna ulishawazoesha kuwatoa washikaji basi na wao wanakutoa pia.