Njia za kushinda soko la ushindani kibiashara

Njia za kushinda soko la ushindani kibiashara

mangiTz

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2019
Posts
1,820
Reaction score
3,062
Habari wakuu,

Niende kwenye mada Moja kwa Moja : tufahamu biashara kwa Sasa Kila unachokifanya haufanyi peke yako Kuna mwingine nae anafanya inafanya na yako inaweza ikawa tofauti ndogo, vitu ambavyo vinachangia kufanya vizuri kwa bidhaa yako(kupata wateja) ni pamoja na:

1) Brand name hii sielezei inafahamika mf. Mdogo Mtu akitaka tv ni Samsung/LG/Hisense kwanini ni sababu brandname

2) price(Bei) ya bidhaa huchangia kupata wateja pia, hizi niachane nazo kwasababu hizi Kila mtu analelewa.

Kuna vitu viwili ambavyo Mimi naviona huenda wengine hawavipi uzito ila vinachangia uendelee kuongeza wateja au uendelee kuwapunguza

1) Kutatua changamoto za wateja wako kwa haraka, mfanyabiashara anaetatutua shida ya mteja wake kwa haraka mteja huridhika na hiyo huduma hivyo humfanya akuamini hata siku nyingine atarudi kwa kigezo wale jamaa hawana longo longo hata bidhaa ikiharibika ndani ya warranty mteja anatengenezewa kwa wakati bila kusukamana(epuka kusumbuana nae pasipo sababu) usimtengenezee uadui.

2) Mapokezi(customer care). Hapa namaanisha msikilize anachohitaji pia jali muda wa mteja amekuja nataka hiki mfanyie huduma yake umalizie uendelee na kingine, Kuna watu akianza mara afanye hiki mara naenda kununua vocha mara apokee simu anaongea afu anavyoongea hata sio vya msingi vimechanganyika na umbea , hichi kitamfanya mteja siku nyingine atayafuta sehemu ya kwenda kufanya huduma yake akipokelewa vizuri huko harusi tena.

Hivi vitu ni vizuri kuwatrain watu unaowasimamia kama biashara ni yakwako kama ni mfanyakazi utaviona vya kawaida ila vimebeba credit kubwa

Vingine tuongezee
3, 4,5
 
Back
Top Bottom