Njia zipi unaweza kuzitumia kuondoa sonona?

Njia zipi unaweza kuzitumia kuondoa sonona?

Una ugonjwa wa akili seek for medical helps Muhimbili hospital kama huko psychiatric department ukaonane na specialist wa masuala mental health na psychologists wote wako pale especially kama uko dar na kama mkoani NENDA hospital ya wilaya uliyopo au mkoa uliopo.
Sina ugonjwa wa akili by the way nashukuru for concern. Ungejua kinachoendelea ungeniambia am sorry
 
Shida ni zipi kwani?unaweza kuziweka hapa?naamini hapa utapokea zaidi ya pole

Binafsi ningekuwa naweza kuonana na mtu ningekuomba tuonane tuongee
Binadamu tumeumbwa kwa mfano wa mpira, sometimes mpira ukijaa sana unapasuka hivyo ndio tulivyo sasa ili usipasuke inabidi upate pa kupumulia ili kupunguza hewa iliyopo ndani ya mpira nazungumzia depression,

Sasa unapokosa mtu wa karibu wa kumwambia Mambo yako ya ndani yanayokusibu au hata ukashindwa kushea na jamii kwa hofu kwamba jamii itakuonaje it means upepo unaendelea kubaki ndani na unaendelea kuongezeka na unahisi kupasuka

Ila ukipata mtu wa kumwelezea situation yako, ukapunguza upepo na akakupa nafuu ya mlango wa kutokea kwamba hapa fanya hivi na hapa itakua hivi angalau unapata nafuu ya ndani, hapo mpira unarudi katika hali ya kawaida na depression inaacha ku-exist you're happy now it's all about happiness & sadness
✍️
 
Nimewahi kuwa kwenye situation kama yako, nilikuwa nina mengi yananisumbua at once yaani ile mengi haswaa, kilichonisaidia ni hakukuwa na kidonge hata kimoja humo ndani maana ndiyo hatua niliyokuwa nimefikia..!!

Niamini girlie, utavuka hapo na kila kitu kitakuwa sawa kabisa, sikuya-solve yote wala, ila I thank God kuwa time heals very quickly, sahii hata nikipitia changamoto lakini huwa sifikirii yale maamuzi tena..!!

Just talk to someone you trust, usimfiche kitu muambie ukweli wa kila kitu huwa inasaidia sana sana.!

Kubwa zaidi talk to God, talk to Him like you're talking to your very closest friend, huwa ninamuambia kila kitu mpaka nazima huko huko usingizini kwa kilio, hayatatulika at once ila mzigo utapungua na utashangaa one after another hayo matatizo yanatafuta njia ya kupungua kwenye maisha yako..!!

Nikipata nafasi ya kuwa na furaha huwa siichezei, I know how it really feels to not have one..!
Wishing you the best new gal ❤️❤️
 
Sina ugonjwa wa akili by the way nashukuru for concern. Ungejua kinachoendelea ungeniambia am sorry
Kama hujui depression ni dalili za ugonjwa wa akili afya YAKO ya akili INGEKUWA timamu usingesema kwenye thread yako "USIONE WATU WANAJIUA"SASA ENDELEA KUBISHA ILA YOU THAT PROBLEM NA NAKUSHAURI UENDE HOSPITAL UGONJWA WA AKILI NI KAMA UGONJWA MWINGINE TU NA SI UKICHAA WALA NINI NDIO MAANA NAKUSHAURI IVYO ,UKIAMUA. FUATA USHAURI UKIONA HAUKUFAI SAWA
 
Aisee unajua tunasikiaga watu wanajiua tunawaona wajinga sana ila ukweli labda sababu hayajatufikia.

Tuombeane aisee hivi depression inaweza kutoka kwa njia zipi. Unajaribu kulala havilaliki, washa TV huelewi unachoangalia, unaweka mziki unaona kama kelele. Yani vururu vururu nimelia wee usku kucha mpaka macho yamevimba.

No shoulder to cry on, no one to sit pemben yako akakusikiliza na kukufariji.

Nyie aisee tuombeane its hard.
Hiyo hali ume-experience kwa muda gani??

wengine ndio life letu hilo,tumezoea hivo na siku tukikutana na hali ya furaha ina bidi tuwe makini kuona ikiwa kweli ni furaha au ni mtego.

Watoto wadogo tu lakini tayari tuna makovu yasiyopona.

Ndio maisha,sio lazima wote tucheke kila siku.
 
Back
Top Bottom