Njiapanda: Mtoto wa mke wangu niliyemlea tangu ana miaka 2 ameenda kutoa mahari bila kunishirikisha

Tenda wema uende zako,
Usitegemee shukrani, endelea na maisha wakikumbuka watakufuata kukushukuru, kwa sasa pambana na wanao.
 
Waite wote wawili mzungumze kinaga ubaga,waambie ulivyofadhaishwa na yanayoendelea!,kutoshirikishwa katika mipango ya harusi ni sawa ile waswahili wanasema "akunyimae mbaazi,kakupunguzia mashuzi"..na mfanyie junguz apoteze kazi akili imkae sawa shenz zao.
 
 
Hili swala lako limenikumbusha jamaa yangu flani na yeye yalimtokea kama haya. Yeye alipoona yamezidi alimtimua mkewe na vitisho tele, kilichomtokea amwanamke akampeleka Polisi ila waliyo maliza.

Tumia busara ongea na mkeo myaweke sawa, kikubwa nikuweka majadiliano baina ya wewe na mkeo.
 
Watu mnachunguza aisee ile story sio ya ukweli mkuu nikimanisha kwamba sio ya kwangu ni ya mtu wangu was karibu SAS nikawa natafuta mawazo aliniomba ushauri nikaona nipate mawazo nikijifanya ni ya kwangu ila hii in kweli ya kwangu..
Hata ningekuwa mimi ningejibu kama wewe ulivyojibu hapo...ningemsingizia mtu wa karibu ule uzi,huu wa leo ndo ungekuwa wangu

Kimsingi watu wachache kama nyie ndio mnafanya wengi wanaohitaji msaada kweli humu JF kupuuzwa wakianzisha nyuzi zao za kuhitaji msaada

Tafuta pesa mkuu ama kama ni mwanafunzi soma
Mwanaume hutakiwi kutafuta attentions zisizo za msingi kama hizi
 
Ukimlaumu huyo dogo utakuwa unemuonea amini kwamba tatizo ni mamake ndo kamjaza huo ujinga.We unauona moshi juu unasahau chini kuna moto ndo unasababisha.
 
Ulitumwa ? Single mother atakiwi kuolewa labda mjane!!!!
 
Story za kutaka ushauri kwenye mambo tata ya uhusiano,ndoa na malalamiko zimekuwa nyingi sana na zinapata wachangiaji wengi. Kwa vile zinapata wachangiaji wengi, members wengi wanajitahidi kubuni story za aina hii. Hii pengine ni ''chai'' nyingine japo sina uhakika.
 
Tuliza akili muuite aje kama inawezekana japo wiki mpe haki yake vizuri kabisa. Ukitulia na akitulia muulize shida nini mara nyingi utakuta ana hasira za miakaaa hiyoo sema hajui ulichepuka kumbe mwenzio ameweka kiporo. Pole sana yatapita
 
Jamaan pole kwa kweli umeongea kwa simanzi mnoo japo umelalamika kweli pole Sana...Cha msingi siku ukipata kajiholiday ka kwenda home mwite wife mchane live mwambie bila kupepesa macho....
 
MTOto kakua uyo na KAZI anayo na anajua kabisa uyo sio baba ake,baba uwe mkali kwa mtoto wa kambo especially ambaye amesha Anza jitegemea...naona unatafuta kuanbiwa live kuwa "kwanza we sio baba yangu"Bora u deal na uyo mkewe mana yeye ndo anaye mjaza ujinga
 
Sisi wanawake tunashida moja watoto wakikua wakapata kazi tunaanza kuwalisha sumu kua baba zao (hata kama ni baba mzazi) wanatutesa/walitutesa.

Maneno kama haya apewe kijana wako ambae anajua wew sio biological father ndio anakuchukia mara mbili . Pole sana . Hapo deal na mkeo akueleze ana tatizo gani na wewe.
 
Duuh!! Ila JF Ni kiboko.
Mkuu umefukuwa makaburi!!!?
 
Pole sana, mambo yao waachie wenyewe...
 
Kamata mwizii meeeeeeen
Shida naiona hapo ni ubinafsi.

Japo nimemuhurumia

lkn inaonekana naye pia pengine alishajichanganya na mwanamke mwingine mama kaona mbelen kutanuka harufu mbaya hivo ameamua kujenga mapema siku kukinuka achanganye miguu Kwa kasi...

Ni vile tatizo tunalisikia toka kwa upande mmoja
 
Mchane apasuke. Anafanya watu kama mapopoma humu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…