Njiapanda: Mtoto wa mke wangu niliyemlea tangu ana miaka 2 ameenda kutoa mahari bila kunishirikisha

Njiapanda: Mtoto wa mke wangu niliyemlea tangu ana miaka 2 ameenda kutoa mahari bila kunishirikisha

Usimind sana, uliwakilishwa na baba mzazi
 
Sawa inawezekana ikawa hivyo lakini stori yako imejaa chumvi

Huyu mke uliyemuoa 2013 anakubania papuchi ni mke huyu wa uzi wa leo ama ni mke wa pili?


Hahahaaa! Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu!!
 
Hapa ndipo unaposikiaga baba kaua mama na mwanaye wa kufikia.

Anachofanya mkeo ni ushenzi wa grade A.

Huenda kijana hana kosa ni msukumo wa mama yake tu.

Bahati nzuri wewe ni mjeshi, na huyo mwanao ni mjeshi, bado una nafasi ya kumkanya huyo step son wako iwe kama baba ama kama senior wake.

Akileta jeuri ongea na wakubwa zake wampige chini. Asilete dharau hapa, eboooh!
Hivi unadhani kupigwa chini ni kirahisi hivyo kama unavyofikiria?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Hata ningekuwa mimi ningejibu kama wewe ulivyojibu hapo...ningemsingizia mtu wa karibu ule uzi,huu wa leo ndo ungekuwa wangu

Kimsingi watu wachache kama nyie ndio mnafanya wengi wanaohitaji msaada kweli humu JF kupuuzwa wakianzisha nyuzi zao za kuhitaji msaada

Tafuta pesa mkuu ama kama ni mwanafunzi soma
Mwanaume hutakiwi kutafuta attentions zisizo za msingi kama hizi
Nimejifunza kitu hapa
 
Narudia usemi wangu wanawake ni viumbe vya ajabu kweli, never trust hawa viumbe hata kidogo, pole sana mkuu.
 
Umejifunza nini mkuu ili na mie nijifunze(japo nimeandika mimi hayo maneno)
Nimejifunza mambo matatu
Moja kuna watu ktk jamii forum wapo wenye matatizo na wanaitaji msaada
Pili kuna watu wengi wapo katika jamii forum kufurahisha watu kwa stori nzuri
Tatu Kuna watu kazi yao kupinga jambo hata kama hawana ushahidi
 
Kijana ameishakuwa, ameishatafuta utambulisho wake(baba mzazi) ameishampata anaenda kuowa atatambulisha Baba 2 ??
Hapa hekima ya mama (mkeo) ilihitajika sana yeye ndiye angeweza kumpanga kijana introduction ikafanyika na nyote 2 mkahusika ktk kubariki shughuli ya kijana kwa wepesi

Child Alienation ni kitu cha kawaida ktk familia hata zisizo na watoto wa kambo. Wanawake huji feel secured zaidi akishapata mtoto ambaye anaweza mlisha matango pori dhidi ya baba.wahanga wakubwa wanakuwa watoto wa kiume

Cha msingi jitayarishe kiakili, huyu Mwanamke uliye naye anaweza kuwakoleza hata hao 6 ukiacha huyo stepson akawa upande wake

Hili tatizo ni LAO sio LAKO don't stress yourself. Usikubali tabia mbovu za wengine zikaharibu Tabia zako endelea kujipamba kwa wema (pambo jema kuliko yote)waachie wenyewe jiondoe taratibu kwa njia chanya kabisa ktk mafungamano yote ya mali na biashara

Tafuta MUDA MWINGI kuwa karibu na wanao ili uwatambue yupi ni pumba yupi ni mchele IN A POSITIVE WAY. Kumbuka Moo Dewji sio wa kwanza kuzaliwa ktk familia ya mzee Ghulam ila through deeper observation ya Mzee aligumdua kuna potentials /Madini kwa kijana Moo kuliko wenzie na akapewa privilege kubwa kuliko wenzie na ndio mwokozi wa familia hivi sasa

Haya mambo yapo mengi yanaendelea kwenye familia nyingi sio wewe pekee. Wewe sio wa mwanzo na wala hutakuwa wa mwisho Ukiona kwako kunaungua kwa mwenzio kuna teketea kwa hiyo huna haja ya kuhuzunika.Changamoto ni utatuzi

Waulizeni Wajuao, Ikiwa Hamjui,
Tafuta ushauri kwa weledi ambao unawaamini kama Wazee wa Kanisa, Wanasaikolojia hata watu wa Ustawi wa Jamii

Na mwisho ingawa sio kwa umuhimu. Mshirikishe Mungu ktk machungu haya yeye ni Omniscient anajua kila kitu, muombee mkeo na watoto wenu wote

Regards
 
Chunga kuzubaa, utazikwa ukiwa hai.
ANZA KUISHI BILA YEYE, JIFUNZE KUAMINI KUWA FURAHA YAKO HAITEGEMEI MTU.

ANZA KUFANYA UPELELEZI BILA FUJO ILI UJUE KAMA KUNA MIPANGO OVU DHIDI YAKO.

POLE KWA MOYO WA HURUMA
 
Ingewezekana ukamharibia dogo ajira yake itakuwa poa sana japo najua ni ngumu, ila ukitumia umafia inawezekana, mpandikizie nadawa ya kulevya au silaha nyumbani kwake, kwa kutumia mafia afukuzwe kazi akili zitawakaa sawa.
Ukatili
 
Baba ake uliambiwa amekufa unalalama nn umkamue mama na mitoto kibao ndani ya miaka 19 watoto 6 bado unataka heshima gani

Mie kitendo chakupotea miezi mitatu unadhani huo muda baba wa Huyo mtoto anakua wapi mana ndo mshauri mkuu kwasasa wamkeo

Kwasasa pambana na wanao hao 6 huyo wa 7 achana nae
 
Habari wana jamvi!

Natumaini ni wazima wa afya, ni hivi niende kwenye mada husika hapo juu mimi ni kijana mwenye umri was miaka 39, nina
Pole mwamba.
Hilo hukulijua ulipooa mke mwenye mtoto, lakini asante kwa ushuhuda huu, wengine pia watajifunza.
Kwanza shika hili: stepson si mwanao, hata umfanyeje atamtafuta babake hata kama huyo baba ni taahira. Hata kama ataambiwa alitokana na ubakaji, atamtafuta.

Na kama kwa bahati yake nzuri alitambulishwa huyo babake mapema tangu utotoni, wataendelea na uhusiano mzuri tu, na wewe utakuwa baba wa nyongeza, bwege mtozeni! Utalisha weee, utafundisha, utaonya, utapatia kazi kama ulivyofanya, lakini haitagusa mtima wake. Yale ya muhimu atahusishwa anayehesabika ndiye wa muhimu, japo vyako vyaliwa.

Huo mpango wa kwenda kuoa bila kukuhusisha amepanga na mama yake, na akishatoka hapo nyumbani kwako ndiyo nitolee, imeisha hiyo. Yote uliyomfanyia anayahesabu kuwa tayari mama yake alishakulipa, hamdaiani. Pole kamanda wangu.

Lakini mshukuru Mungu, jivike ujasiri, endelea kutunza hao wa kwako 6, pengine Mungu atakulipa mara 6 kupitia hao. Samehe upate amani.
 
Habari wana jamvi!

Natumaini ni wazima wa afya, ni hivi niende kwenye mada husika hapo juu mimi ni kijana mwenye umri was miaka 39, nina mke na watoto 6 ila mke wangu nilimkuta akiwa na mtoto wa kiume wakati tunaoana mwaka 2002, jumla ukijumlisha tuna watoto 7 kiukweli huyo kijana mtoto wa mke wangu my step son nimemtafutia kazi Serikalini now anafanya kazi vizuri, alipata
Anza kuishi kama mwanaume kuanzia unapousoma huu uzi.

Story ni ndefu lakini mwachie Mungu atakulipia. Usiumie moyo kaka.

Wanawake ni zaidi tunavyowanfahamu.
 
Nyongeza. Ukiwa na uhusiano na mwanamke mwenye mtoto, hasa wa kiume, siku zote yule mtoto anakuona kama mvamizi kwenye maisha yake na mama yake. Na akikua kidogo akajua unamnyandua mama yake, ujue atakuchukia kishenzi, wivu kabisa ule wivu wa kiume. Atakuvumilia tu kwa kuwa unampa mama yake hela, lakini hakupendi. Chochote utakachompa anakihesabu kama hongo kwa kuwa unamkula mama yake, usitegemee shukurani yoyote kwa sababu umeshaipata kwa mama yake na ujue hapendi unavyomkula.

Usitarajie kuwa ukija kumuoa huyo mama eti na huyo mtoto atakupenda, hilo nakuhakikishia halitatokea hata umfanyie nini. Na atakapopata mawasiliano na baba mzazi, basi hao watatu (mtoto, mama yake na baba yake) watakugeuza chumo, bwege mtozeni. Utalea mtoto wa mwenzio, akifikia kujimudu mwenyewe ataondoka kwako kama vile hakujui! Ataanzisha makazi yake mapya na kuendeleza ule wimbo wa "nani kama mama", wewe utatelekezwa.

Hata yule baba yake uliyekuwa unadanganywa kuwa hamjali mtoto utakuja kushangaa kujua kuwa kumbe alikuwa anamjali! Watakuwa wanakutana na mkeo kwenye shughuli za huyo mtoto wao! Ataitwa kuja kutoa jina la mjukuu, wewe utawekwa kando. Unahitaji kuwa na ngozi ngumu sana kuvumilia mambo kama haya uzeeni.
 
Pole sana kaka
Habari wana jamvi!

Natumaini ni wazima wa afya, ni hivi niende kwenye mada husika hapo juu mimi ni kijana mwenye umri was miaka 39, nina
Pole sana kaka huo Ndo ukubwa,kibaya zaidi Hawa wenzetu huwa hawasomeki ata ufanyeje,Cha msingi mshukuru mungu wewe ni mzima Ila kuwa na hekima na pia taadhari maana bado kijana mkifika uzeeni unaweza jikuta mwenyewe ata mfaliji ukakoswa kumbuka watoto ni wa mama asilimia Mia na wanawasikiliza kuliko sisi wanaume.

Cha msingi meombe sana mungu kwani update kuutuliza moyo wako na uendelee kuishi kwa amani,James husikate tamaa.Mkubwa wangu pia yalimkuta ya kwako baada ya kijana wa make wake kuwa mjeshi aliamua kumuachisha mama take kwa kaka na wanakaa kivyao.Hawa huwa ni marafiki tu na urafiki una muda wa kuisha
 
Back
Top Bottom