Njiwa

Njiwa

Njiwa
Njiwa peleka salamu
Oo kwa yule wangu muhimu
Mueleze afahamu
Kwamba ninapata taabu
Hali yangu mahamumu
Oo maradhi yameni siibu

Chorus
Eewe njiwa x2
Peleka salamu
Kwa yule x2
Wangu muhimu

Usiku kucha nakesha
Oo na yeye ndiye sababu
Ewapo haji maisha
Itamfika aibu
Pendo langu halijesha
Oo ndilo lino niadhibu

Njiwa usi hadhaike
Oo nenda ulete majibu
Nenda upesi ufike
Mkimbilie swahibu
Mbele yake utamke
Oo ni yeye wa kunijibu


Ukifika tafadhali
Oo sema naye taratibu
Ukisema kwa ukali
Mambo utayaharibu
Kamwabie sina hali
Oo kufariki si ajabu



View attachment 361967
My favourate favourate
 
Back
Top Bottom