Ikumbukwe kuwa yeye si mtu wa kwanza kujijengea kaburi in advance, hilo jambo alijifunza kutoka kwa mzee Lutengano wa Mtwango, Mzee Lutengano aliwahi kuwa mkuluma maarufu miaka hiyo akimiliki tractor aina ya Ford iliyokuwa ikitumia kerosene na alidumu nayo kwa miaka mingi hadi late 80s, inasadikika kampuni ya Ford ilipata habari juu ya uwepo wa tractor hiyo kongwe kinyume na matarajio yao, hivyo kitendo cha kukitunza chombo hicho kwa miaka mingi na hata kuipa kampuni hiyo sifa kuwa inatengeneza vitu imara, kiliwafanya watengenezaji wa Ford kumpa zawadi.