The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Askari 3 wa Jeshi la Polisi mkoani Njombe wamefariki dunia na wengine 9 kujeruhiwa baada ya gari la polisi kugongana na basi la abiria la Sharon linalofanya safari zake Njombe-Arusha.
Tukio hilo limetokea leo Februari 3, saa 12 asubuhi.
Njombe. Polisi watatu wamekufa na wengine tisa kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wamepanda kugongana na basi na kampuni ya Sharon linalofanya safari zake kati ya Njombe na Arusha.
Akizungumza leo Jumatatu Februari 3, 2020 mganga mfawidhi wa Hospitali ya Kibena-Njombe, Dk Anord Mtega Maganga amethibitisha kupokea miili ya askari polisi hao, kwamba wengine tisa ni majeruhi.
Ajali hiyo imetokea leo alfajiri eneo la kituo cha Polisi cha Mkoa wa Njombe.


