Njombe: Juma Kyando, adaiwa kumuua mke wake kisha kumkata vipande na kwenda kumtupa mtoni

Hivi hapa Tanzania kuna mikoa iliyolaanika zaidi ya Njombe, Mbeya, na Iringa? Kila kukicha ni wao tu wakisaidiwa kwa mbali na ndugu zao wa Mara na Geita
 
Hiki kizazi chetu sijui hata kina nini. Ni kama vile uzao wa 80 kuja juu ni kama kuna laana imepita.

Nawaza kama wazazi wetu na sisi wangekuwa na fikra na maamuzi kama ya kizazi hiki sijui hata kama wengi wetu tungezaliwa.
Kizazi hiki kimezidi kuchepuka na kuchapiana
 
Tujifunzi kuwaacha wapenzi wetu waende kwa amani. Hakuna hati miliki ya binadamu.
 


Jifunze kuzitawala hisia zako.

Stop taking things too personal.


Tabia mbaya ya mwenza wako sio uhalisia wa utu wako, ni kipimo cha uvumilivu wako, kujitoa kwako na umadhubuti wako.

Ndoa sio jela na binaadam sio bidhaa.



Suluhisho la tatizo lolote lile sio kuondoa uhai. Hata mlinzi wa Amani haui mtu ila kwa sheria na taratibu maalum kinyume na hapo anawajibika.
 


Uzuri wa uhalisia wa maisha, haswaa ya ndoa, hayaangalii jinsia, rangi wala kabila.

Tujitahidi kuepuka kujipa mamlaka kwenye maisha ya wenzetu kiasi kuhisi tunawamiliki Kama viatu vya msalani.

Tujifunze kuishi katika uhalisia na kujua kuzisoma alama za nyakati.

Kikubwa zaidi tukumbuke Uanaume sio Uungu.

Binaadam hana mamlaka juu ya uhai wa mwingine na hata wake mwenyewe na ndio maana ukiponea chupuchupu katika kutaka kujiua unashtakiwa na Serikali.
 
Ugomvi wa mapenzi ni wa kukaa nao mbali kabisa.

Unaweza ukaingilia ukaumizwa then baada ya muda watu wanarudiana na maisha yanaendelea kama kawaida

Uko sahihi.

Lakini kuna tofauti kati ya kuingilia ugomvi na kusuluhisha ugomvi. Wengi wetu tunapenda kuingilia ugomvi na kuchagua upande kabisa.
 
Halafu mnasema wanawake wanamidomo?! Hii ni nini? Dustbin?
Mkuu usibishane na asili, ni ukweli mtuptu wanawake wana midomo mirefu, ukibisha kwa hili "hongera" unathibitisha urefu wa midomo yenu lakini pia unathibitisha ufinyu wa hoja zenu.

SIUNGI MKONO mauaji yaliyotekelezwa na ndugu Kyando naamini kulikua na njia bora zaidi za kutatua mkwamo uliokua baina yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…