Njombe: Juma Kyando, adaiwa kumuua mke wake kisha kumkata vipande na kwenda kumtupa mtoni

Njombe: Juma Kyando, adaiwa kumuua mke wake kisha kumkata vipande na kwenda kumtupa mtoni

Tumaini Luvanda (35) mkazi wa Dombwela wilaya ya Makete mkoani Njombe ameuawa kwa kukatwa na panga vipande kisha kutenganishwa kichwa na kiwiliwili na baadhi ya viungo kutupwa kwenye mto jirani na nyumbani katika eneo la Kabinda wilayani humo ambapo tayari Polisi inamshikilia Juma Kyando (36) ambaye ni mume wa Tumaini (Marehemu) kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.
View attachment 2866248
Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Iwawa ambaye pia ni mwenyekiti wa mtaa wa Dombwela Joseph Mbilinyi amesema tukio limetokea usiku wa kuamkia January 8,2024 ambapo alifika nyumbani kwa mtuhumiwa mara baada ya kupigiwa simu na majirani na kumkuta Kyando akiwa na Panga jambo lililomfanya apige simu Polisi ili kuomba msaada.
View attachment 2866247
"Baada ya Polisi kuja alikuwa ameshamuua mkewe na kumuweka kwenye mfuko wa kisarufeti na kwenda kutupa kwenye mto,kwenye uwanja wake tuliuona Moyo wa mwanadamu ndio tukaanza kufuata kwenye mto kwasababu alikuwa anavuta sarufeti lakini kufika kwenye mto tukaona kisarufeti kinaelea kwenye maji tukakiopoa na kuendelea kufuata tena mto tukakiona kiungo kingine ambacho ni ubavu upande wa titi na shingo nacho tukakiopoa tukaanza kutafuta kichwa ambacho kimetusumbua kwa muda mrefu"amesema Mwenyekiti

Mkuu wa Polisi wilaya ya Makete mrakibu mwandamizi wa Polisi Assel Mwampamba amesema tukio hilo si la kawaida na kutoa ushauri kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuwa na namba za jeshi la Polisi ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza "Hili lingezuilika sasa ametoka na Panga mkakimbia wote na wanaume acheni uwoga yaani mtu yuko mmoja anacharanga mtu ninyi mmekimbia mngekuwa mnamrushia mawe asingeendelea kukata mtu pale"
View attachment 2866246
Kwa upande Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Njombe Mrakibu wa Polisi Joseph Malongo akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe mara baada ya kufika eneo la tukio amesema kuwa ni lazima mtuhumiwa aweze kuchukuliwa sheria "Niwape pole kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe,mwenzetu bwana Juma amejichukulia sheria mkononi jeshi la Polisi lazima tumchukulie hatua stahiki na tumpeleke Mahakamani haraka iwezekanavyo"

Medrick Kyando ni ndugu wa Mtuhumiwa wa mauaji ya mkewe pamoja na baadhi ya majirani wamesema Kyando ni fundi wa kujenga alikuwa hana makundi pia hana historia ya kuwa na matatizo ya akili na alikuwa anaishi vizuri na mke wake lakini wanashangaa kuona ametekeleza tukio hilo la kikatili lililowashtua ambapo kwa sasa anaacha watoto wadogo watatu akienda Polisi na mkewe akiwa amefariki.
Hivi hapa Tanzania kuna mikoa iliyolaanika zaidi ya Njombe, Mbeya, na Iringa? Kila kukicha ni wao tu wakisaidiwa kwa mbali na ndugu zao wa Mara na Geita
 
Hiki kizazi chetu sijui hata kina nini. Ni kama vile uzao wa 80 kuja juu ni kama kuna laana imepita.

Nawaza kama wazazi wetu na sisi wangekuwa na fikra na maamuzi kama ya kizazi hiki sijui hata kama wengi wetu tungezaliwa.
Kizazi hiki kimezidi kuchepuka na kuchapiana
 
Aisee ndoa ni changamoto sana kwa sasa , kuna mtu aliandika uzi humu kwamba ametukanwa na mke wake tusi zito ,mke wake akimtukana ":unadhani mimi nafirwa kama wewe ? "
Yeye anadai hii ni baada ya kumuuliza mbona umechelewa ,ulikuwa wapi ?
Huyo mkewe ndio kamjibu hivyo
Sasa najaribu kufikiria kama mtu mwenye hasira za karibu kama mimi ,aisee yawezekana ningefanya kama alichofanya huyu jamaa wa Njombe
Imagine una mke kichwa panzi kama huyo ,kwanini usiende kununua panga na gunia la mkaa kuja kumfanya nyamachoma ?
Tunaishi nyakati mbovu sana wakuu ,Mungu tu atusaidie
Tujifunzi kuwaacha wapenzi wetu waende kwa amani. Hakuna hati miliki ya binadamu.
 
Aisee ndoa ni changamoto sana kwa sasa , kuna mtu aliandika uzi humu kwamba ametukanwa na mke wake tusi zito ,mke wake akimtukana ":unadhani mimi nafirwa kama wewe ? "
Yeye anadai hii ni baada ya kumuuliza mbona umechelewa ,ulikuwa wapi ?
Huyo mkewe ndio kamjibu hivyo
Sasa najaribu kufikiria kama mtu mwenye hasira za karibu kama mimi ,aisee yawezekana ningefanya kama alichofanya huyu jamaa wa Njombe
Imagine una mke kichwa panzi kama huyo ,kwanini usiende kununua panga na gunia la mkaa kuja kumfanya nyamachoma ?
Tunaishi nyakati mbovu sana wakuu ,Mungu tu atusaidie


Jifunze kuzitawala hisia zako.

Stop taking things too personal.


Tabia mbaya ya mwenza wako sio uhalisia wa utu wako, ni kipimo cha uvumilivu wako, kujitoa kwako na umadhubuti wako.

Ndoa sio jela na binaadam sio bidhaa.



Suluhisho la tatizo lolote lile sio kuondoa uhai. Hata mlinzi wa Amani haui mtu ila kwa sheria na taratibu maalum kinyume na hapo anawajibika.
 
So kwa upande wa pili hatujui story ilikuwaje kiuhalisia ,ila wanawake wa sasa ,wengi hawajui jinsi ya kutumia midomo yao na kuishi na mwanaume , unakuta anamjibu mwanaume as if anaongea na mpuuzi mwenzake ,hapo lazima uamshe mashetani yaliyopo kwenye kichwa cha mwanaume Rijali wa kiAfrica ,kiufupi unakuwa umeyatimba , midomo ya wanawake imekuwa chanzo kikubwa cha uharibifu na majanga ndani ya ndoa
Sijui hawafundwi ?
Au ndio akili zao zimeshaharibiwa na maisha wanayoyaona kwenye movies na series za Hollywood ? Na kutaka kureplicate katika maisha ya kiAfrica ,kitu ambacho hakiwezekani
Kiufupi hili ni bomu


Uzuri wa uhalisia wa maisha, haswaa ya ndoa, hayaangalii jinsia, rangi wala kabila.

Tujitahidi kuepuka kujipa mamlaka kwenye maisha ya wenzetu kiasi kuhisi tunawamiliki Kama viatu vya msalani.

Tujifunze kuishi katika uhalisia na kujua kuzisoma alama za nyakati.

Kikubwa zaidi tukumbuke Uanaume sio Uungu.

Binaadam hana mamlaka juu ya uhai wa mwingine na hata wake mwenyewe na ndio maana ukiponea chupuchupu katika kutaka kujiua unashtakiwa na Serikali.
 
Ugomvi wa mapenzi ni wa kukaa nao mbali kabisa.

Unaweza ukaingilia ukaumizwa then baada ya muda watu wanarudiana na maisha yanaendelea kama kawaida

Uko sahihi.

Lakini kuna tofauti kati ya kuingilia ugomvi na kusuluhisha ugomvi. Wengi wetu tunapenda kuingilia ugomvi na kuchagua upande kabisa.
 
Halafu mnasema wanawake wanamidomo?! Hii ni nini? Dustbin?
Mkuu usibishane na asili, ni ukweli mtuptu wanawake wana midomo mirefu, ukibisha kwa hili "hongera" unathibitisha urefu wa midomo yenu lakini pia unathibitisha ufinyu wa hoja zenu.

SIUNGI MKONO mauaji yaliyotekelezwa na ndugu Kyando naamini kulikua na njia bora zaidi za kutatua mkwamo uliokua baina yao.
 
Back
Top Bottom