Njombe: Juma Kyando, adaiwa kumuua mke wake kisha kumkata vipande na kwenda kumtupa mtoni

Nawe nitolee stress zako. Wapi nikemtaja shetani? Pumbavu wahead wewe.
stori za mungu huendana na shetani.

Ulijibu mtu aliyesema taasisi imeingiliwa na shetani, ukasema mungu atusaidie.

Pumbavu ni kushindwa kuelewa.
Hivyo wewe ni mpumbavu sababu hata Polisi na ndugu wanashangaa na Hawajui Kwanini kafanya hivyo
ILA wewe unayo majibu yako.
 
mkuu tofautisha kati ya Njombe na makete.Makete ipo mkoa wa njombe,yawezekana umeishi njombe mjini hujaingia makete.Makete kule kwenye milima ya kulima ngano,bangi ilikuwa inaota yenyewe.Hata mking'oa huu mwaka,mwakani ipo tena.
kale ka ukanda ka kutoka pale makete mjini kwenda bulongwa,unakujua kisajanilo?then utapita masalala,uje utanziwa,uitafute ilolo,uende igalula,uende madege,uitafute ndamba then ije ikusi uione bulongwa🙂
ingawa sijarudi mitaa ile zaidi ya miaka 11 sasa,labda mambo yamebadilika
Ahaaa😅😅😅 e bwana hyo kule milimani nilikuwa napaona kipindi nasoma busokelo,mbeya karibu na milima livingstone sasa ukiwa upande wa mbeya usawa kuanzia kyela mpaka busokelo na baadhi ya vijiji vya wilaya ya rungwe unayaona mashamba ya ngano kwa juuuu milimani.

Kwenda kule juu nakumbuka tulikuwa tunapita kwenye madaraja ya kamba yaliyojengwa na mjerumani. Zile kamba za nyaya zinasaidia mpaka leo watu wa makete hupitia njia hyo kama njia ya mkato kwa mguu kwenda mbeya.
 
Tumaini Luvanda (35) mkazi wa Dombwela wilaya ya Makete mkoani Njombe ameuawa kwa kukatwa na panga vipande kisha kutenganishwa kichwa na kiwiliwili na baadhi ya viungo kutupwa kwenye mto jirani na nyumbani katika eneo la Kabinda wilayani humo ambapo tayari Polisi inamshikilia Juma Kyando (36) ambaye ni mume wa Tumaini (Marehemu) kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.
View attachment 2866248
Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Iwawa ambaye pia ni mwenyekiti wa mtaa wa Dombwela Joseph Mbilinyi amesema tukio limetokea usiku wa kuamkia January 8,2024 ambapo alifika nyumbani kwa mtuhumiwa mara baada ya kupigiwa simu na majirani na kumkuta Kyando akiwa na Panga jambo lililomfanya apige simu Polisi ili kuomba msaada.
View attachment 2866247
"Baada ya Polisi kuja alikuwa ameshamuua mkewe na kumuweka kwenye mfuko wa kisarufeti na kwenda kutupa kwenye mto,kwenye uwanja wake tuliuona Moyo wa mwanadamu ndio tukaanza kufuata kwenye mto kwasababu alikuwa anavuta sarufeti lakini kufika kwenye mto tukaona kisarufeti kinaelea kwenye maji tukakiopoa na kuendelea kufuata tena mto tukakiona kiungo kingine ambacho ni ubavu upande wa titi na shingo nacho tukakiopoa tukaanza kutafuta kichwa ambacho kimetusumbua kwa muda mrefu"amesema Mwenyekiti

Mkuu wa Polisi wilaya ya Makete mrakibu mwandamizi wa Polisi Assel Mwampamba amesema tukio hilo si la kawaida na kutoa ushauri kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuwa na namba za jeshi la Polisi ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza "Hili lingezuilika sasa ametoka na Panga mkakimbia wote na wanaume acheni uwoga yaani mtu yuko mmoja anacharanga mtu ninyi mmekimbia mngekuwa mnamrushia mawe asingeendelea kukata mtu pale"
View attachment 2866246
Kwa upande Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Njombe Mrakibu wa Polisi Joseph Malongo akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe mara baada ya kufika eneo la tukio amesema kuwa ni lazima mtuhumiwa aweze kuchukuliwa sheria "Niwape pole kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe,mwenzetu bwana Juma amejichukulia sheria mkononi jeshi la Polisi lazima tumchukulie hatua stahiki na tumpeleke Mahakamani haraka iwezekanavyo"

Medrick Kyando ni ndugu wa Mtuhumiwa wa mauaji ya mkewe pamoja na baadhi ya majirani wamesema Kyando ni fundi wa kujenga alikuwa hana makundi pia hana historia ya kuwa na matatizo ya akili na alikuwa anaishi vizuri na mke wake lakini wanashangaa kuona ametekeleza tukio hilo la kikatili lililowashtua ambapo kwa sasa anaacha watoto wadogo watatu akienda Polisi na mkewe akiwa amefariki.
Kuishi katika ndoa ni kugumu kuliko maelezo. Tuayoyaona kwaana ndoa Kwa nje in maigizo tu, kiuhalisia ndoa no mapambano ya kudumu. Bila busara na hekima kutumika, maisha ya ndoa hayawezekani kwa wengi
 
Njombe ishu ya migogoro ya ndoa ipo juu sana na jamaa wa huko wana ukatili sana...daah unaikata pisi yako na kwenda kuitupa vipande huo ni ukatili ambao Simba mnyama anasubiri mbali mno...
Inawezekana pisi ilikuwa inamjibu sheet jamaa,kumletea dharau
Mwamba kachoka kavurugwa kachizika
Mambo ya ndoa ya mabalaa sana
Mkuchokana ni off off tu
Bora kila mtu achukue 50 zake

Ova
 
Kuishi katika ndoa ni kugumu kuliko maelezo. Tuayoyaona kwaana ndoa Kwa nje in maigizo tu, kiuhalisia ndoa no mapambano ya kudumu. Bila busara na hekima kutumika, maisha ya ndoa hayawezekani kwa wengi
Ndoa siku hizi hazina uvumilivu

Ova
 
nadhani ARUSHA..GEITA,NJOMBE NA IRINGA ni mikoa inayoitaji maombi mazito sanaa na kukombolewa na pepo la mauaji sio kawaidaa kabisaaa...!! hili ni pepooo sio KAWAIDA HATA KIDOGO.
Arusha umeiweka ili ku balance au? Yaani uifananishe Arusha na Geita,njombe,simiyu,Mara,au Rombo ya kilimanjaro?utakuwa uko mbali na akili zako,Arusha kesi zake ni zile za kimjini mjini,ambazo zipo kwenye majiji yote,zile za deal gone wrong etc, siyo za kuchinja mke.
 
Tumaini Luvanda (35) mkazi wa Dombwela wilaya ya Makete mkoani Njombe ameuawa kwa kukatwa na panga vipande kisha kutenganishwa kichwa na kiwiliwili na baadhi ya viungo kutupwa kwenye mto jirani na nyumbani katika eneo la Kabinda wilayani humo ambapo tayari Polisi inamshikilia Juma Kyando (36) ambaye ni mume wa Tumaini (Marehemu) kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.
View attachment 2866248
Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Iwawa ambaye pia ni mwenyekiti wa mtaa wa Dombwela Joseph Mbilinyi amesema tukio limetokea usiku wa kuamkia January 8,2024 ambapo alifika nyumbani kwa mtuhumiwa mara baada ya kupigiwa simu na majirani na kumkuta Kyando akiwa na Panga jambo lililomfanya apige simu Polisi ili kuomba msaada.
View attachment 2866247
"Baada ya Polisi kuja alikuwa ameshamuua mkewe na kumuweka kwenye mfuko wa kisarufeti na kwenda kutupa kwenye mto,kwenye uwanja wake tuliuona Moyo wa mwanadamu ndio tukaanza kufuata kwenye mto kwasababu alikuwa anavuta sarufeti lakini kufika kwenye mto tukaona kisarufeti kinaelea kwenye maji tukakiopoa na kuendelea kufuata tena mto tukakiona kiungo kingine ambacho ni ubavu upande wa titi na shingo nacho tukakiopoa tukaanza kutafuta kichwa ambacho kimetusumbua kwa muda mrefu"amesema Mwenyekiti

Mkuu wa Polisi wilaya ya Makete mrakibu mwandamizi wa Polisi Assel Mwampamba amesema tukio hilo si la kawaida na kutoa ushauri kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuwa na namba za jeshi la Polisi ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza "Hili lingezuilika sasa ametoka na Panga mkakimbia wote na wanaume acheni uwoga yaani mtu yuko mmoja anacharanga mtu ninyi mmekimbia mngekuwa mnamrushia mawe asingeendelea kukata mtu pale"
View attachment 2866246
Kwa upande Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Njombe Mrakibu wa Polisi Joseph Malongo akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe mara baada ya kufika eneo la tukio amesema kuwa ni lazima mtuhumiwa aweze kuchukuliwa sheria "Niwape pole kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe,mwenzetu bwana Juma amejichukulia sheria mkononi jeshi la Polisi lazima tumchukulie hatua stahiki na tumpeleke Mahakamani haraka iwezekanavyo"

Medrick Kyando ni ndugu wa Mtuhumiwa wa mauaji ya mkewe pamoja na baadhi ya majirani wamesema Kyando ni fundi wa kujenga alikuwa hana makundi pia hana historia ya kuwa na matatizo ya akili na alikuwa anaishi vizuri na mke wake lakini wanashangaa kuona ametekeleza tukio hilo la kikatili lililowashtua ambapo kwa sasa anaacha watoto wadogo watatu akienda Polisi na mkewe akiwa amefariki.
Njombe on the beat once again , Geita na Njombe ,hii mikoa hii ni as if wanaishi subhuman creatures tu
Kila siku matukio ya ajabu ajabu ,aisee
Hizi ziwe kanda maalumu ,na ni mikoa mipya iliyomegwa ila kila siku vituko haviishi
 
Back
Top Bottom