ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Mfanyabiashara Maarufu mjini Njombe bwana Godfrey Ndambo amevamiwa na kujeruhiwa vibaya na watu Wasiojulikana usiku wakati akirenea nyumbani kwake ambapo baadae alifariki kutokana na majeraha hayo,Polisi wamethibitisha.
Baada ya kuvamiwa walimpora pesa kiasai Cha Milioni 47 na kutokea kusikojulikana.Polisi wanaendelea na uchungywa.msako.
---
Mfanyabiashara maarufu katika mji wa Njombe, Godfrey Ndambo (45) aliyevamiwa na majambazi maeneo ya nyumbani kwake wakati akitokea kwenye biasharab zake na kupigwa na kitu kizito kichwani kilichosababisha majeraha, amefariki dunia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Julai 22, 2024 amesema tukio hilo lilitokea Julai 20, 2024, saa 2:30 usiku katika eneo la Uzunguni, Kata ya Ramadhani, Halmashauri ya mji wa Njombe.
Banga amesema wahusika wa tukio hilo ambao idadi yao haijafahamika, walimpiga mfanyabiashara huyo na kutoweka na fedha zinazokadiriwa kuwa ni Sh47 milioni.
"Baada ya kujeruhiwa alitibiwa katika Hospitali ya Kibena na baadaye alihamishiwa mkoani Mbeya wakati matibabu yakiendelea akafariki dunia," amesema Banga.
Amesema jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi wa kina na baadaye watatoa taarifa ya watu watakaoshikiliwa kuhusika na tukio hilo.
Kamanda huyo amewataka wafanyabiashara mkoani Njombe kufunga kamera maeneo wanayoishi na ziwe wazi muda wote, kwani linapotokea tukio ni rahisi kwa polisi kuanza kufanya uchunguzi kupitia kamera hizo.
My Take
Ni very risk kutembea na pesa nyingi kiasi hicho, unakwepa TRA huku unahatarisha maisha yako.
R.I.P mpambanaji Ndambo sijui kama ndio yule wa Ndambo Construction au ni ukoo tuu.