Njombe: Mfanyabiashara aliyevamiwa na kujeruhiwa afariki dunia

Njombe: Mfanyabiashara aliyevamiwa na kujeruhiwa afariki dunia

Nahisi alikuwa anajihusisha na miamala ya benki na mitandao ya simu, na huenda ni makusanyo ya siku kadhaa. Wahuni huwa wanatabia wakijua una circulation nzuri ya pesa wanakuja kuweka hard cash nyingi ili iwe rahisi kwao kukufanyia umafia coz wanajua una cash on hand kiasi cha kutosha.
Inasikitisha Gentleman.
 
ni kweli,,alikua wakala mkubwa sana mjini,kwa banks zote na mitandao yote ya cm.
Biashara za namba hii mara nyingi unakuwa unazunguka na Israeli mtoa roho muda wote. Lakini kwa hapo suspects wa kwanza ni wateja walioweka kiasi kikubwa kwa siku hizo karibia na tukio kutokea. Wanaweza kuwa hata 10 ili wapoteze upelelezi ila ni kukusanya wote maelezo ni mbele chuya na mpunga vitajitenga
 
Mfanyabiashara Maarufu mjini Njombe bwana Godfrey Ndambo amevamiwa na kujeruhiwa vibaya na watu Wasiojulikana usiku wakati akirenea nyumbani kwake ambapo baadae alifariki kutokana na majeraha hayo,Polisi wamethibitisha.

Baada ya kuvamiwa walimpora pesa kiasai Cha Milioni 47 na kutokea kusikojulikana.Polisi wanaendelea na uchungywa.msako.
---
Mfanyabiashara maarufu katika mji wa Njombe, Godfrey Ndambo (45) aliyevamiwa na majambazi maeneo ya nyumbani kwake wakati akitokea kwenye biasharab zake na kupigwa na kitu kizito kichwani kilichosababisha majeraha, amefariki dunia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Julai 22, 2024 amesema tukio hilo lilitokea Julai 20, 2024, saa 2:30 usiku katika eneo la Uzunguni, Kata ya Ramadhani, Halmashauri ya mji wa Njombe.

Banga amesema wahusika wa tukio hilo ambao idadi yao haijafahamika, walimpiga mfanyabiashara huyo na kutoweka na fedha zinazokadiriwa kuwa ni Sh47 milioni.

"Baada ya kujeruhiwa alitibiwa katika Hospitali ya Kibena na baadaye alihamishiwa mkoani Mbeya wakati matibabu yakiendelea akafariki dunia," amesema Banga.

Amesema jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi wa kina na baadaye watatoa taarifa ya watu watakaoshikiliwa kuhusika na tukio hilo.

Kamanda huyo amewataka wafanyabiashara mkoani Njombe kufunga kamera maeneo wanayoishi na ziwe wazi muda wote, kwani linapotokea tukio ni rahisi kwa polisi kuanza kufanya uchunguzi kupitia kamera hizo.

My Take
Ni very risk kutembea na pesa nyingi kiasi hicho, unakwepa TRA huku unahatarisha maisha yako.

R.I.P mpambanaji Ndambo sijui kama ndio yule wa Ndambo Construction au ni ukoo tuu.
Kabisa
 
Biashara za namba hii mara nyingi unakuwa unazunguka na Israeli mtoa roho muda wote. Lakini kwa hapo suspects wa kwanza ni wateja walioweka kiasi kikubwa kwa siku hizo karibia na tukio kutokea. Wanaweza kuwa hata 10 ili wapoteze upelelezi ila ni kukusanya wote maelezo ni mbele chuya na mpunga vitajitenga
Ndo wamuue sasa si wangempora tu waende zao huko,,,na ni mbaya sana mtu ukiwa unamfaham na kanihudumia sana tu.
 
Hii sijui inakuwaje, watu wa akili za kufanya biashara na kukuza mitaji yao.
Lakini kuna maeneo wanakuwa na udhaifu.

Kutembea na kiasi kkubwa cha pesa hivyo ni hatari
Jamaa watakua wamesoma nyendo za marehemu na kwamba wameona ni kawaida yake.
au aliofanya nao biashara mara ya mwisho ndio hao hao wahusika
 
Mfanyabiashara maarufu Mjini Njombe, Godfrey Ndambo (45) ambaye ni Mkazi wa Uzunguni Kata ya Ramadhan Wilaya na Mkoa wa Njombe amefariki wakati akipata matibabu mara baada ya kuvamiwa na Majambazi waliompiga na kitu kizito kichwani nje ya geti wakati akiingia nyumbani alipokuwa akitoka kazini kwake na kisha wakaondoka na Tsh. milioni 47 ambazo alitoka nazo dukani kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Mahamoud Banga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema Mfanyabiashara huyo alivamiwa July 20,2024 saa mbili na nusu usiku wakati akitoka kwenye shughuli zake za biashara ambapo mpaka sasa Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi juu ya tukio.

“Ndambo alivamiwa wakati anatoka kwenye shughuli zake za biashara wakati anaingia getini na kupigwa na kitu kizito kichwani na waliompiga ambao bado hatujajua idadi yao waliweza kutoweka na fedha ambazo zinakadiriwa kuwa ni Tsh. milioni 47 kulingana na taarifa tulizozipata kutoka katika biashara yake ya hesabu zilizofungwa lakini majeruhi alitibwa katika Hospitali yetu ya Kibena na baadaye alihamishiwa Mkoa wa Mbeya na wakati matibabu yanaendelea akafariki”

RPC Banga ametoa wito kwa Wafanyabiashara ambao wamefunga CCTV camera, muda wote ziwe zinafanya kazi ili kusaidia pia katika uchunguzi kwa kuwa kutokana na tukio hilo wamepata changamoto maana camera ndani ya nyumba ya Mfanyabishara huyo hazifanyi kazi kwa kuwa zilikuwa zimezimwa huku pia akiwaomba wanaofanya shughuli za biashara ya fedha kuweka fedha zao benki kuliko kurudi na fedha nyumbani.
#MillardAyoUPDATES
FB_IMG_1721662001984.jpg
 
View attachment 3049165
fedha "zinakadiriwa" kuwa milioni 47. huyo mkadiriaji ni nani
 
Back
Top Bottom