Njombe: Mfanyabiashara aliyevamiwa na kujeruhiwa afariki dunia

Njombe: Mfanyabiashara aliyevamiwa na kujeruhiwa afariki dunia

Mfanyabiashara maarufu Mjini Njombe, Godfrey Ndambo (45) ambaye ni Mkazi wa Uzunguni Kata ya Ramadhan Wilaya na Mkoa wa Njombe amefariki wakati akipata matibabu mara baada ya kuvamiwa na Majambazi waliompiga na kitu kizito kichwani nje ya geti wakati akiingia nyumbani alipokuwa akitoka kazini kwake na kisha wakaondoka na Tsh. milioni 47 ambazo alitoka nazo dukani kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Mahamoud Banga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema Mfanyabiashara huyo alivamiwa July 20,2024 saa mbili na nusu usiku wakati akitoka kwenye shughuli zake za biashara ambapo mpaka sasa Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi juu ya tukio.

ā€œNdambo alivamiwa wakati anatoka kwenye shughuli zake za biashara wakati anaingia getini na kupigwa na kitu kizito kichwani na waliompiga ambao bado hatujajua idadi yao waliweza kutoweka na fedha ambazo zinakadiriwa kuwa ni Tsh. milioni 47 kulingana na taarifa tulizozipata kutoka katika biashara yake ya hesabu zilizofungwa lakini majeruhi alitibwa katika Hospitali yetu ya Kibena na baadaye alihamishiwa Mkoa wa Mbeya na wakati matibabu yanaendelea akafarikiā€

RPC Banga ametoa wito kwa Wafanyabiashara ambao wamefunga CCTV camera, muda wote ziwe zinafanya kazi ili kusaidia pia katika uchunguzi kwa kuwa kutokana na tukio hilo wamepata changamoto maana camera ndani ya nyumba ya Mfanyabishara huyo hazifanyi kazi kwa kuwa zilikuwa zimezimwa huku pia akiwaomba wanaofanya shughuli za biashara ya fedha kuweka fedha zao benki kuliko kurudi na fedha nyumbani.
#MillardAyoUPDATES
View attachment 3049165
Inasikitisha Sana..jamani tusikae nyumbani Na pesa nyingi
 
njombe nilikuwa napachukulia poa ila ni sehemu hatari

nasikia kuna tajiri mmoja huko aliitwa bomoa, alikuwa anateka wasichana mikoani anakuja kuwaweka kwenye danguro lake,

baada ya kufa polisi walichunguza nyumba yake wakakuta alikuwa na chumba cha kuchinjia watu
 
njombe nilikuwa napachukulia poa ila ni sehemu hatari

nasikia kuna tajiri mmoja huko aliitwa bomoa, alikuwa anateka wasichana mikoani anakuja kuwaweka kwenye danguro lake,

baada ya kufa polisi walichunguza nyumba yake wakakuta alikuwa na chumba cha kuchinjia watu
Uongo watu wakijijini kuzusha zusha
 
Alivamiwa akiwa getini nyumbani kwake soma vizuri
Nje ya geti wakati akiingia....
Screenshot_20240722-183828.jpg
 
ubatili mtupu! utafute pesa kwa udi na uvumba, usiku na mchana uzipate kiasi, zenyewe tena zikuue!

tumche Mungu ndugu zangu, haya mengine ni ubatili mtupu, na kujilisha upepo.

JESUS IS CHRIST!
Sasa Mungu ndo anataka tuwe masikini walokole bana.

Unasema kuwa na hela ubatili wakati kanisani michango lukuki
 
ubatili mtupu! utafute pesa kwa udi na uvumba, usiku na mchana uzipate kiasi, zenyewe tena zikuue!

tumche Mungu ndugu zangu, haya mengine ni ubatili mtupu, na kujilisha upepo.

JESUS IS CHRIST!
Huyo mungu angeweza kumfanya huyo tajiri awe na pesa na aishi kwa amani, lakini siasa nyingi ooh mpokee yesu, ooh sali sana....

Yaani wewe huna tofauti na watoto wanavyoamini eti walinunuliwa badala ya kutoka kwenye nyuchi
 
Wewe si umeandika ubatili mtupu tumwamini Yesu.

Sasa Yesu ndo katukataza kuwa na hela
kuwa na pesa bila Yesu ni ubatili mtupu. Sisi tuna pesa, na tunaye Yesu. Jambazi akipanga kunidhuru kabla ya kunifikia malaika watakatifu, Jeshi la mbinguni wanakuwa weshamshughulikia. Tunalindwa na nguvu za ajabu. 1PETRO 1:5
 
Back
Top Bottom