Njombe: Mfanyabiashara aliyevamiwa na kujeruhiwa afariki dunia

Njombe: Mfanyabiashara aliyevamiwa na kujeruhiwa afariki dunia

Mfanyabiashara Maarufu mjini Njombe bwana Godfrey Ndambo amevamiwa na kujeruhiwa vibaya na watu Wasiojulikana usiku wakati akirenea nyumbani kwake ambapo baadae alifariki kutokana na majeraha hayo,Polisi wamethibitisha.

Baada ya kuvamiwa walimpora pesa kiasai Cha Milioni 47 na kutokea kusikojulikana.Polisi wanaendelea na uchungywa.msako.
---
Mfanyabiashara maarufu katika mji wa Njombe, Godfrey Ndambo (45) aliyevamiwa na majambazi maeneo ya nyumbani kwake wakati akitokea kwenye biasharab zake na kupigwa na kitu kizito kichwani kilichosababisha majeraha, amefariki dunia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Julai 22, 2024 amesema tukio hilo lilitokea Julai 20, 2024, saa 2:30 usiku katika eneo la Uzunguni, Kata ya Ramadhani, Halmashauri ya mji wa Njombe.

Banga amesema wahusika wa tukio hilo ambao idadi yao haijafahamika, walimpiga mfanyabiashara huyo na kutoweka na fedha zinazokadiriwa kuwa ni Sh47 milioni.

"Baada ya kujeruhiwa alitibiwa katika Hospitali ya Kibena na baadaye alihamishiwa mkoani Mbeya wakati matibabu yakiendelea akafariki dunia," amesema Banga.

Amesema jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi wa kina na baadaye watatoa taarifa ya watu watakaoshikiliwa kuhusika na tukio hilo.

Kamanda huyo amewataka wafanyabiashara mkoani Njombe kufunga kamera maeneo wanayoishi na ziwe wazi muda wote, kwani linapotokea tukio ni rahisi kwa polisi kuanza kufanya uchunguzi kupitia kamera hizo.

My Take
Ni very risk kutembea na pesa nyingi kiasi hicho, unakwepa TRA huku unahatarisha maisha yako.

R.I.P mpambanaji Ndambo sijui kama ndio yule wa Ndambo Construction au ni ukoo tuu.
Kuku alidonoa punje ngapi za mahindi?
 
RIP mfanyabiashara...najiuliza tuu karne ya leo ambapo mifumo ya kibenki na Mpesa iko every where mtu anaondokaje dukani na 47milion Cash??
Inaonekana jamaa hata hujajisumbua kusoma taarifa na michango ya members wenzako we umekimbilia tu ku comment. Ngoja nikusaidie maana hata shule/vyuoni Kuna watu hawakutoboa bila kuegezea. Huyo mhanga ni mfanyabiashara wa fedha za mitandao ya simu, na icho kiasi cha pesa kilichopelekea auwawe ni mtaji/mauzo yake ya siku, sasa swali lako la sijui angeweka mpesa au bank limekufa.
 
Apumzike kwa Amani ndugu yetu.. Kufanya biashara ya miamala bora uwe na float nyingi kuliko Cash..!! Yanii huyu itakuwa kuna mtu alimchoreshaaa.. Dunia haipo fair ukiwa maskini tabu Ukipata helaa pia tabuu daah.
 
😀😀yupo stable sana mke wake nurse. japo kifo hakizungumzi ila mjomba najua kawaacha vizuri sana familia sasa hio ni 47m in cash ushawahi waza bank ana shilingi ngapi
We acha tu Maisha ni fumbo zito sana kwa hio 47M zimemchukua Jamaa na hapo utakuta alikua hataki kuachia maana wale mabwana wakikutaiti ukiwa Mbishi ndio kwakheri
 
Apumzike kwa Amani ndugu yetu.. Kufanya biashara ya miamala bora uwe na float nyingi kuliko Cash..!! Yanii huyu itakuwa kuna mtu alimchoreshaaa.. Dunia haipo fair ukiwa maskini tabu Ukipata helaa pia tabuu daah.
Noma sana ukiwa Tajiri inabidi uwe na Watu wengi wanaokulinda usiishi kizembe ili ufe kizembe
 
Hakuna kitu kama hicho.

Mpaka leo madukani Ulaya kuna ma cash register chungu nzima, na foleni ya cash ni ndefu kuliko electronic.

Ukisema hupokei cash hakuna mtu atakuja na hata huko Ulaya sijawahi kuona biashara inakataa cash money.
Umeishi ulaya nchi gani?
 
Hakuna kitu kama hicho.

Mpaka leo madukani Ulaya kuna ma cash register chungu nzima, na foleni ya cash ni ndefu kuliko electronic.

Ukisema hupokei cash hakuna mtu atakuja na hata huko Ulaya sijawahi kuona biashara inakataa cash money.
Cash money Ulaya sio kama kwetu. Nilikua Ulaya last month, yaani almost kila mtu anatumia card.
 
Ifikie wakati sasa tuende na mfumo wa Cashless, huko ni salama zaidi kwa fedha na UHAI wetu
 
Back
Top Bottom