Njombe: Viongozi wa CHADEMA pamoja na dalali wa mbao wakamatwa kwa kuhusishwa na mauaji ya Kada wa CCM Emmanuel Mlelwa

Kwa Lissu walisema kuwa wanamsubiri aje atoe ushahidi. Huu wa Njombe wameupata kwa maiti au?
 
Hakuna watu ninaowachukia duniani Kama Wana ccm
 
CHADEMA ikichukua nchi oktoba 28 italifuta jeshi la polisi , huu ujinga wa kuwanunua wagombea udiwani ulipangwa na kwamba wakikataa watapewa kesi yoyote , na hii imevuja tangu wiki 2 zilizopita eti leo ndio inatekelezwa ! Poor Polisi
Mkuu inaonekana unajua vizuri undani wa mauaji haya ya kutisha!! , enheee tueleze ndiyo CHADEMA mkaamua kumuua huyo kijana? Halafu TUNDU anaimba 'haki haki' aibu kubwa!! Roho ya marehemu haitamwacha salama.
 
Hii spidi ndio inatakiwa katika kufanya uchunguzi wa mauaji ambayo yanahusishwa na mambo ya kisiasa. Laiti kama yale mauaji ya Geita kwa mfuasi wa Chama kinzani yangechunguzwa kwa spidi hii, wananchi wangeona haki imetendeka. Yaelekea sasa haki, kama yalivyo maendeleo, ni kwa baadhi tu ya watu katika nchi hii.
 
Polisi wataalamu wa kubambikia watu kesi! Mtu aue, halafu abaki na mkanda, ili iweje? Mola atawahukumu na kuwapa stahiki yenu!
 
Option iliyopo sasa hivi ni kuuawa makada kesi kupelekewa wagombea ili kuongeza wanaopita bila kupingwa
 
Hapo ndipo usanii wa polisi wetu unapojidhihirisha wazi wazi. Usikute mkanda huo uliwekwa tu kama wanavyobambikiziaga watu wengine madawa ya kulevya. Polisi wetu na akina Diamond et al kazini.
 
Mkanda wa marehemu kwenye gari ya mgombea udiwani wa Chadema!! Ebu Polisi kuweni serious basi msilete isidingo kama ya watekaji wa Mo, kumbukeni Rais aliwaambia watanzania sio wajinga.
Kilichotafutwa ni ushahidi...mkanda ukachomekewa duu
 
Vifo vimekuwepo muda mrefu na waliokufa na kupotea ni wengi but polisi mnaposema mkanda kwenye gari hakika mnaanza kuyumba kwa sehemu semeni vitu ambavyo ni critical jamii isione mnaleta siasa maana hao pia ni wagombea wanaweza kuzuliwa jambo la uongo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kesi hii inahitaji wakili makini!
πŸ˜…
πŸ‘Š ✌️✌️✌️πŸ’₯
 
Mbinu mpya zikoje hebu tufahamishe, lazima mchezee kichapo cha kisheria huu ujinga wenue wa kujifanya mko juu ya sheria. Kisanga kikitokea unavuna mwenyewe, tunawaambia acheni ushabiki wa kijinga wa kujifanya mko juu ya sheria. Leo boss wenu lISSU anafundishwa namna ya kuheshimu sheria za nchi, akitoka huko atakuwa amepata digree ya uaminifu. Jinga kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…