Njombe: Wanafunzi watoro walipishwa Tsh. 5,000 kwa kila siku wasiyofika shuleni

Njombe: Wanafunzi watoro walipishwa Tsh. 5,000 kwa kila siku wasiyofika shuleni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wakazi wa kata ya Mavanga iliyopo wiliya ya Ludewa mkoani Njombe wamewalalamikia walimu wakuu pamoja na Afisa elimu wa kata hiyo kwa kuwalazimisha kulipia fedha kwa mtoto atakayeshindwa kufika shuleni pamoja na kuwalipa walimu wa kujitolea.

Wakitoa malalamiko hayo mbele ya mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga alipofanya ziara katika kijiji cha Mavanga, Mbugani pamoja na kitongoji cha Luhuhu getini wananchi hao wamedai kuwa walimu hao wamekuwa wakiwatoza kiasi cha shilingi elfu tano kwa siku na endapo mwanafunzi hatofika shuleni siku tano basi wanatakiwa kulipa elfu 25,000.

Melania Mtweve ni mmoja wa wananchi hao ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mavanga amesema wanashindwa kuelewa hizo fedha wanazitoa kwa malengo gani kwani wasipolipa watoto hurudishwa nyumbani mpaka aende na hiyo fedha.

" Kwa elimu ya mtindo huu ni bora watoto wangu wakaage nyumbani maana shule sasa hivi imekuwa ni mradi unaojitegemea ambao unawanufaisha walimu kwasababu mara nyingine mtoto anashinda shule kwa mambo ya msingi si kwa makusudi", Alisema Mtweve.

Sanjari na suala hilo pia wazazi hao wameiomba serikali kuajili walimu wa kutosha kwani wamekuwa wakilazimishwa kuchangia kiasi cha shilingi elfu 10,000 kwa kila mwanafunzi ili kuwalipa walimu wanaojitolea.

Akizungumza hayo mmoja wa wakazi wa kitongoji cha Luhuhu getini David Mgaya amesema kuwa michango hiyo inawapa tabu sana kwani endapo mzazi anakuwa na watoto watano analazimika kulipa elfu 50, 000.

Mgaya ameiomba serikali kulichukulia suala hilo kwa uzito kwani wananchi wanahali ngumu na wanaposhindwa kulipa fedha hizo walimu wamekuwa wakiwasumbua watoto mashuleni ikiwemo kuwakamata wazazi na kuwapeleka katika ofisi za kijiji.

Akijibu hoja hizo afisa elimu wa kata hiyo Hosea Chaula amekiri kuwepo kwa malipo hayo ya kutofika shuleni na kuwalipa walimu wa kujitolea na kudai kuwa hayo yote yanatekelezwa kwa makubaliano kati ya kamati ya shule na wazazi.

Ameongeza kuwa wazazi na kamati hiyo ilikubaluana kuwalipisha fedha endapo watoto hawatafika shuleni ili kukomesha tabia za utoro kwa wanafunzia hao na kuwafanya wazazi wawe wanawahimiza watoto kufika shule.

Amesema kwa upande wa kuwalipa walimu wa kujitolea ni njia mojawapo ya kuwasaidia wanafunzi kupata elimu bora kutokana na uhaba wa walimu huku akitoa mfano wa shule ya msingi Ushindi ambayo ina wanafunzi 436 huku walimu walioajiliwa wakiwa sita hivyo wamelazimika kuongeza walimu wawili ambao hulipwa na wazazi hao.

"Haya yote tunatekeleza kwa mujibu wa makubaliano na wazazi na kwakuwa ni makubaliano nasi tunahakikisha tunafuatilia michango yote ambapo fedha ya walimu wa kujitolea hulipwa kwa awamu tatu kwa mwaka mwezi wa tatu, saba na tisa", Alisema Chaula.

Aidha kwa upande wa mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga amewataka viongozi hao wa elimu kufuata utaratibu wa utungaji sheria ndogo ndogo ambapo zinatakiwa kupitishwa na baraza la madiwani kwani ukusanyaji wa fedha kiholela ni sawa na kuiba.

Amesema kila malipo yaliyo halali yanapaswa kukatiwa risiti hivyo kama kunaulazima wa kutoza faini kwa mtoto asiyefika shule basi wapitishe sheria hiyo na wananchi wapewe risiti wafanyapo malipo hayo ikiwezekana ijulikane fedha hizo zinapikwenda.

Ameongeza kuwa suala la wazazi kuajili walimu hata bungeni amewahi kulizungumzia sambamba na kuiomba serikali kuleta walimu ambapo mpaka sasa tayari walimu 140 wameajiliwa wilayani Ludewa na bado anaendelea kupambana ili kupata walimu wengine zaidi.Hata hivyo amesema kuwa fedha hizo wanazotozwa wazazi kwaajili ya kuwalipa walimu wa kujitolea ni nyingi sana hivyo wanapaswa kupunguza kiwango cha malipo hayo.

"Nikweli serikali ina wajibu wa kuajili walimu lakini pia kwa nafasi yangu nitaendelea kuishauri serikali iajili walimu hao wanaojitolea ili waweze kuwa wakudumu na kuingizwa katika mfumo na hiyo ya kutofika shule kuanzia leo naizika haitakuwepo tena kama watawadai waambieni waje wachukue kwangu na mnapokuja kwangu hakikisheni mnanipa na risiti", Alisema Kamonga.

MICHUZI BLOG
 
Kama walikubaliana kwenye kikao rasmi... Nn tatizo?
na kwann mtoto asiende shule?
na kama wanajua hizo fedha ni za kulipa walimu wa kujitolea kwann wanalalamika kwamba hawajui hao fedha ni za nn?
kuna shida pahala
 
Sanjari na suala hilo pia wazazi hao wameiomba serikali kuajili walimu wa kutosha kwani wamekuwa wakilazimishwa kuchangia kiasi cha shilingi elfu 10,000 kwa kila mwanafunzi ili kuwalipa walimu wanaojitolea.
Hongereni wazazi labda mkipaza sauti nyie serikali itawaelewa
 
Mi nashauri mtoto mtoro mzazi alipe 10,000 kila siku ambayo mtoto hakufika shule.

Najua lengo la mbinu hii nikuwafanya wazazi wasimamie vizuri mahudhurio ya watoto wao. Kuna mizazi ikisha andikisha mtoto shule ndo hutakaa umuone mpaka akisikia kuna mahafali shuleni.

Naamini hii ni miongoni mwa makubaliano ya vikao vyao wenyewe sema wazazi baadhi wanaona shule kama vita
 
Kama walikubaliana kwenye kikao rasmi... Nn tatizo?
na kwann mtoto asiende shule?
na kama wanajua hizo fedha ni za kulipa walimu wa kujitolea kwann wanalalamika kwamba hawajui hao fedha ni za nn?
kuna shida pahala
Hii sio kuhusu makubaliano.

Hii ni nchi na inaendeshwa na serikali moja na sio kila mtu kuamua anavyotaka.
Walimu wameajiliwa na serikali sio wananchi hivyo ni wajibu wa serikali kulipa walimu na ni wajibu wa walimu kufundisha na sio vinginevyo.
Kama hutaki basi acha kazi.

Wewe umeona nchi gani wanafanya huu utumbo?
 
Are you even serious or you're just tripping?
Yaani unaandika kama unaishi peke yako duniani hufikirii consequences wala negative effects.

Bila shaka wewe ni mwalimu sasa kama mwalimu una fikra dhaifu kama hizi unategemea wanafunzi wako wawe vipi?

My desperation is immeasurable for my country's future generations.
 
Binafsi naunga mkono hii itawasaidia kuzuia UTORO mashuleni

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
that's nice critical thinking right there.

Na vipi kuhusu wazazi ambao ni masikini ila watoto wa ni watukutu?
I mean technically asilimia kubwa ya watoto ni watukutu na wasiosikia pia na asilimia kubwa ya watanzania ni masikini.

Je ulifikiria hilo na unajua hasara zake ndani ya miaka 20?

And what would you do under that circumstance?
 
Mi nashauri mtoto mtoro mzazi alipe 10,000 kila siku ambayo mtoto hakufika shule.

Najua lengo la mbinu hii nikuwafanya wazazi wasimamie vizuri mahudhurio ya watoto wao. Kuna mizazi ikisha andikisha mtoto shule ndo hutakaa umuone mpaka akisikia kuna mahafali shuleni.

Naamini hii ni miongoni mwa makubaliano ya vikao vyao wenyewe sema wazazi baadhi wanaona shule kama vita
Kama walikubaliana kwenye kikao rasmi... Nn tatizo?
na kwann mtoto asiende shule?
na kama wanajua hizo fedha ni za kulipa walimu wa kujitolea kwann wanalalamika kwamba hawajui hao fedha ni za nn?
kuna shida pahala
5000/= bado ni hela ndogo sana.

Huwezi kukuta Wazazi wa Kilimanjaro, Arusha, Kagera au Mbeya wanajitetea kipumbavu hivi

Wazazi wa hii mikoa hawajui umuhimu wa elimu, hata Mtoto akitoroka Miezi 6 wataona ni sawa tu

Ndio maana mikoa hii inakuwa nyuma kielimu

Wanawatumia hao watoto kupalilia Shamba na kuvuna wakati ni wanafunzi
 
Unajua maana ya walimu wa kujitolea? Hawajaajiriwa na serikali na hawalipwi na serikali. Shule darasa la kwanza mpaka la saba af ina walimu sita tu walioajiriwa hapo Kuna mwl mkuu ambaye kwa Majukumu yake Mara nyingi Hana vipindi manake walimu wapo watano. Manake walimu Wana mzigo mkubwa Sana usiobebeka Yan walimu watano wafundishe madarasa Saba masomo sita. Na bado wafatilie utoro na maendeleo ya mtoto mmoja mmoja. Hiz kaz nyingine lazma zifanywe na wazazi.

Na ili mzazi afanye Majukumu yake lazma awekewe mkakati wa kumlazimisha afanye kazi yake. Kwanin mtoto asiende shule? Kama Kuna dharura kwanini asiombewe ruhusa? Hiv makazini kwetu tunaweza kuacha kwenda siku nzima bila kutoa taarifa au vile wazazi hawajui umuhim wa elimu. Hata huyo mbunge wao alipaswa kwanza kukemea utoro wa watoto. Na Kama mbunge kaumia Sana alipaswa kujitolea kuwalipa hao walimu wa kujitolea. Vinginevyo watoro wasiopenda shule wawasomeshe wanaopenda shule Kama inawauma wabadilike au waache shule kabisa hapo shule itabidi watafute namna nyingine ya kupata hela Ila angalau tatzo la utoro limeisha.

Hizi shule za serikali hazitaendelea Kama wazazi watabakia wakidhan kufaulu kwa mtoto na jitihada za walimu tu. Wao wakae tu wasifatilie watoto wao. Wazazi hao ni wajinga wasiojua umuhimu wa elimu. Mbunge watoto wake wanasoma private kwake hata shule ikikosa walimu kabsa Hana hasara.
Hii sio kuhusu makubaliano.

Hii ni nchi na inaendeshwa na serikali moja na sio kila mtu kuamua anavyotaka.
Walimu wameajiliwa na serikali sio wananchi hivyo ni wajibu wa serikali kulipa walimu na ni wajibu wa walimu kufundisha na sio vinginevyo.
Kama hutaki basi acha kazi.

Wewe umeona nchi gani wanafanya huu utumbo?
 
Wazazi wajinga kabisa... Mbunge nae ni wauongo alipaswa awape ukweli hao wazazi
 
Hii sio kuhusu makubaliano.

Hii ni nchi na inaendeshwa na serikali moja na sio kila mtu kuamua anavyotaka.
Walimu wameajiliwa na serikali sio wananchi hivyo ni wajibu wa serikali kulipa walimu na ni wajibu wa walimu kufundisha na sio vinginevyo.
Kama hutaki basi acha kazi.

Wewe umeona nchi gani wanafanya huu utumbo?
Mwalimu wa kujitolea analipwa mavi ako?
 
Mlipe tu maana mmezidi uzwazwa. Kama ningekuwa mimi huko mnalipishwa 10000 na mnachapwa viboko wote mzazi na mtoto wake ili muwe serious.

Kwa wanakijiji kama wewe msioppenda kusomesha na msio fatilia mahudhurio ya watoto wenu ni kutiwa mikwaju plus fine.
Are you even serious or you're just tripping?
Yaani unaandika kama unaishi peke yako duniani hufikirii consequences wala negative effects.

Bila shaka wewe ni mwalimu sasa kama mwalimu una fikra dhaifu kama hizi unategemea wanafunzi wako wawe vipi?

My desperation is immeasurable for my country's future generations.
 
Mkuu nimesoma shule za Kata mbaka nilipohitimu,nilijionea mwenyewe Kuna baadhi ya sehemu usiposhurutisha jitu kwenda shule ndio basi Tena Kuna baadhi ya wazazi usipotumia nguvu mtoto aende shule na lenyewe litakenua meno na kuona Bora asaidie kulima mashambani nk

Huo upupu unalemeza Sana kielimu hapo naona waongeze faini na hao wazazi wanaolia Lia wale mboko na mikwaju wasilete upuuzi kwanini mtoto asiende shule bila sababu halafu alipishwe faini aanze kulia Lia kupumbavu hivyo?

Mimi nakumbuka tunavyoanza form one kulikua na mijinga mingi Sana Kuna ticha alihamia sisi tunaanza form one hapo shule na alikua anasifika Kanda nzima kua ni mkora haswa pande la jitu ukilizingua linakuvunja kiuno akapewa darasa letu afundishe kingereza jamaa alikua Hana utani yaani akimaliza kipindi chake ana attendant yake ukidoji tu utajuta kuzaliwa Kuna wazazi wakawa wanalalamika Kama hao matokeo yake matoto mazembe yakakacha shule,
Yule ticha alitublash English mbaka tukawa vichwa Kanda nzima yaani utasoma tu vitabu vyote utachambua bila kupenda nashukuru tulimaliza na tukawa njema Sana Sina haja ya kwenda Kwa Ras Simba kusoma kozi Tena niliyopata Toka Kwa yule mwamba ni konk mengine najazia tu kidigitali

Nachomaanisha elimu bila mkazo na msisitizo Kwa maeneo Kama hayo mtoto hatoboi!
 
Mwalimu wa kujitolea analipwa mavi ako?
Oh no I wouldn't give a shit about it.

Amejitolea yeye na hakuna aliyemlazimisha non of my business kama hataki basi aache kazi kuliko kulete unscheduled things.

Jinsi unavyoandika ni evidence tosha ya kwanini unafikiria nonsense.

Now acha utoto na ujibu lile swali.
 
Mkuu nimesoma shule za Kata mbaka nilipohitimu,nilijionea mwenyewe Kuna baadhi ya sehemu usiposhurutisha jitu kwenda shule ndio basi Tena Kuna baadhi ya wazazi usipotumia nguvu mtoto aende shule na lenyewe litakenua meno na kuona Bora asaidie kulima mashambani nk

Huo upupu unalemeza Sana kielimu hapo naona waongeze faini na hao wazazi wanaolia Lia wale mboko na mikwaju wasilete upuuzi kwanini mtoto asiende shule bila sababu halafu alipishwe faini aanze kulia Lia kupumbavu hivyo?

Mimi nakumbuka tunavyoanza form one kulikua na mijinga mingi Sana Kuna ticha alihamia sisi tunaanza form one hapo shule na alikua anasifika Kanda nzima kua ni mkora haswa pande la jitu ukilizingua linakuvunja kiuno akapewa darasa letu afundishe kingereza jamaa alikua Hana utani yaani akimaliza kipindi chake ana attendant yake ukidoji tu utajuta kuzaliwa Kuna wazazi wakawa wanalalamika Kama hao matokeo yake matoto mazembe yakakacha shule,
Yule ticha alitublash English mbaka tukawa vichwa Kanda nzima yaani utasoma tu vitabu vyote utachambua bila kupenda nashukuru tulimaliza na tukawa njema Sana Sina haja ya kwenda Kwa Ras Simba kusoma kozi Tena niliyopata Toka Kwa yule mwamba ni konk mengine najazia tu kidigitali

Nachomaanisha elimu bila mkazo na msisitizo Kwa maeneo Kama hayo mtoto hatoboi!
Now tell me where did that get you?
 
Mi nashauri mtoto mtoro mzazi alipe 10,000 kila siku ambayo mtoto hakufika shule.

Najua lengo la mbinu hii nikuwafanya wazazi wasimamie vizuri mahudhurio ya watoto wao. Kuna mizazi ikisha andikisha mtoto shule ndo hutakaa umuone mpaka akisikia kuna mahafali shuleni.

Naamini hii ni miongoni mwa makubaliano ya vikao vyao wenyewe sema wazazi baadhi wanaona shule kama vita
Ujinga mtupu. Kwahiyo mzazi awe kila siku anaenda shule na mtoto aache shughuli za kujiingizia kipato? Mtoto anatoka nyumbani kwenda shule anafika njiani anaingia mitini.

Vinginevyo kwa mawazo finyu kama haya utakuwa mwalimu tu ndo IQ huwa ndogo kama hivi.
 
Mlipe tu maana mmezidi uzwazwa. Kama ningekuwa mimi huko mnalipishwa 10000 na mnachapwa viboko wote mzazi na mtoto wake ili muwe serious.

Kwa wanakijiji kama wewe msioppenda kusomesha na msio fatilia mahudhurio ya watoto wenu ni kutiwa mikwaju plus fine.
Yeah mkuu hiyo mikwaju utapiga wajinga tu labda kama kazi yako umeichoka then give it a try.

Tell me what're the consequences of that act in 20 years?

I thought tulishatoka huku kumbe bado kuna africans wenye mindset za nyani.

Nguvu nyingi ubongo mdogo.
 
kuna watu hata ukitumia logic kiasi gani hawataelewa! ni kwasababu wameamua katika kufikiria katika mlengo mmoja tu!

waalimu ni watu ambao wana kazi sana hususani pale anapotaka wanafunzi wafaulu!

kuna shule nyingi za serikali saivi waalimu wamekata tamaa yaan mwanafunzi aje au asije hiyo ni juu yake akiingia darasani wanafunzi wameelewa au hawajaelewa watajua wenyewe! maana ukichapa bakora tu! kesi unayo ya kujibu!

Hao waalimu ambao wamefikia hatua ya utoro kulipishwa 5000 ni ili kumuhamasisha mzazikufatilia mwanae! imagine shule ya darasa la 1 mpaka la 7 lenye mikondo miwili kila darasa na kila mkondo una wanafunzi karibu 70-100 halafu waalimu wenyew wako 7 tu, mwalimu ataweza kufatilia maendeleo individually ya kila mwanafunzi!? maanahata huyo mwalimu ana majukumu yake mengine nk!

kama mtu ambae amesoma hizi shule za kijijini, i hope ataelewa kwanini wanafanya hivyo! mwalimu mkuu akiamua kukaa kimya na kukausha hao wanafunzi wataishia kusema tulisoma ila hakuna elimu kichwani!

mimi binafsi nlimaliza darasa la saba hata kuandika tu ilikua mtihani sana maana darasani nlikua siendi na hamna mtu wa kutusimamia na shule maskani kwahyo ilikua uende usiende utajua mwenyewe! ..nwaka unaofata baada ya kumalizala saba mavuno ya mpunga yalitoka vizuri ikabidi nipelekwe hizi private! na nlirudia darasa la 4 imagine umemaliza la 7 unarudi hadi la 4[emoji16][emoji16][emoji16] huko private ndo mpaka namaliza la 7 tena nkawa najua vitu na kung'amua kua mi nlikuaga jembe[emoji16] hata mzazi wangu hakujuta kabisa!

mi nashauri ni sawa tu hiyo tozo ya utoro kua 5000 itahamasisha mzazi afatilie maendeleo ya mwanae kwa umakini! maana bila hvyo mzazi kufatilia maendeleo ya mwanae inakua ni mengineyo!
 
Back
Top Bottom