Njoo PM niku Assist

Njoo PM niku Assist

Labda alikabwa akaona no way! Mkumbuke magu alisema atakayetoboa July huyo kidume.

Acheni bwembwe uliyepigwa ndiyp unaijua dasalaam ni zaidi ya uijuavyo.
 
MATAPELI wa JF ni pamoja nae. Mpe hela akuagizie kutoka nje, imekula kwako








UTETEZI WAKE HUU HAPA
Wana jamii,

Nadhani mnakumbuka miezi kadhaa iliyopita tulikuwa na biashara ya bidhaa toka nje Ughaibuni na kwingineko duniani.

Biashara yetu ilidumu kwa miezi kadhaa ambayo na tuliweza ku trend japo changamoto zilikuja kutokea za hapa na pale, ambazo nyingine ni binafsi na nyingine ni ambazo ziko nje ya uwezo wangu, au wetu kiujumla, kutokana na report mbali mbali za hapa JamiiForums na kusababisha kusambaa kwa habari ambazo si nzuri kwa kampuni yangu, ikaamuliwa kufungwa na taasisi husika,
kufungwa kwa ofisi kulipelekea matatizo makubwa sana na kukajenga hofu kwa baadhi ya wateja ambao walikuwa wameweka order ya mizigo yao ilipelekea kuzuka kwa nyuzi (threads mbali mbali ) kuwa;
KEVIN ISAYA TAPELI,
KEVIN ISAYA MDHULUMAJI
KEVIN ISAYA MUONGO
Na hii ilikuwa haki ya wateja kusema hivyo maana walikuwa hawajapata haki yao, huwezi kujitetea kama hujatimiza kitu ambacho mteja anataka haswa, kusema kweli hiyo ilipelekea mpaka msuko suko kazini kwangu maana jumuiya za kimataifa na usalama zilifika na kunihoji juu ya suala ilo ila kwakuwa nilikuwa na proof ya nini kinaendelea haikuleta matatizo sana nilieleweka, japo nilieleweka baada ya muda mrefu sana sana sana takriban miezi mitatu niki chini ya ulinzi nakumbuka tokea January 18-april sikuwa huru.

Hali hiyo ilipelekea kwanza kupotea kwenye mtandao kwakuwa sikuwa na access ya simu, na baadhi ya nyenzo za kuniwezesha kuwasiliana.

Najua wengi mtapuuza na kusema TAPELI, na wengine kutoelewa kabisa ninachoeleza ila anayejua ukweli ni mimi na Mungu.

Tuhuma za ID nyingi za JF, sina ID zaidi ya mbili nyinginezo ni za watu waliokuwa wananifanyia marketing na sales, siyo zangu na sizijuhi, nakumbuka mara kadhaa nimepata malalamiko kuwa kuna anayetumia ID nyingi kutangaza biashara kama yako, niliwauliza wenzangu na kusema ni wao, hivyo ID yeyete hapa iliyotumia ni ya watu wangu wa sales, ila sikuwa mimi direct, hata kama hazikuwa na matatizo, maana kuna mtu alisema nina account nne, jambo ambalo si kweli kabisa, mi natumia account ya Kevin Isaya, as verified user.

Kuna mda kama binadamu nilikuwa na hasira juu ya watu wengine hawadai wanachochea tu, ila samahanini nitakamilisha kila kitu soon as possible,
NATAKA KUWEKA KUMBUKUMBU SAWA KEVIN ISAYA SIYO TAPELI NI MTANZANIA SAFI, zilizotokea ni changamoto za kibiashara tu, ambazo kila mfanyabiashara hupitia ila kwa kiwango tofauti.

PILI nataka kutanguliza shukrani kwa uvumilivu wa wateja wote hata kama imepita miezi kadhaa kumbuka haki ya mtu haipotei kabisa, hata iwe lini huwezi kupata amani ya moyo au utulivu kama unajua kuna jambo muhimu hujalikamilisha.

HATUA NINAZOCHUKUA JUU YA WANAO NIDAI NA AMBAO WALIKUWA WAMEAGIZA MZIGO
Kwanza ieleweke kuwa kwasasa sina mpango wa kuendelea na biashara hii karibuni mpaka nifute madeni yote, na pili ikitokea nikaanza tena SITAKUJA KUPOKEA HELA YA MTU KABLA YA MZIGO hatua moja wapo nimekuwa nawasiliana na mteja mmoja mmoja kwa njia ambayo ni rahis kumpata.

Baada ya kuwasiliana nao naeleza bayana si rahisi kulipa hela kwa mkupuo wakati hukuitumia, wala hukuiwekeza mahali popote, hivyo basi ninalipa taratibu taratibu najua na ninavyoongea hapa kuna watu ambao mnasoma hapa mmeshalipwa, nilitaka niweke contact zenu na majina lakini mpaka mtoe idhini ya kufanya hivyo.

Wapo ambao hawajagusgwa kabisa hata shillingi mia, lakini ukweli ni kwamba hata iwe lini you will get what youn deserve, tuwe wavumilivu now am free to full fill everything, lakini kwa uhakika wa mambo nimeomba muda wa miezi miwili, mtakuwa na ya kusema mengine hapa.

THEN TUTUMIE KAMUSI TUSIPINDISHE MAANA YA TAPELI, KUNA TOFAUTI KUBWA KATI YA TAPELI NA ALIYECHELEWESHA HUDUMA KUTOKANA NA CHANGAMOTO.

TUKIO MUHIMU AMBALO SITASAHAU
Hata ukiwauliza wafanyakazi niliokuwa nawatumia ni kwamba watu tuliowatumia hela kudeliver mzigo baadhi walikimbia na hawajulikani walipo, ila tumefuatilia mpaka kwa wanasheria kule hasa Dubai wametuambia kufungua kesi is possible na malipo ndo changamoto maana wanasheria wale wanalipwa kwa saa, yaani wakili anayesimama kukutetea analipwa kwa saa, ambayo ni dollar 11,000 per hour, is better to pay people who demands instead of going in prolonged processes at high costs.

Pamoja na hayo naomba wafuatao wanisamehe kabisa wamepata usumbufu kipindi siko hewani na pengine kupata kashfa zisizo wahusu
1. Baba yangu mzani na ndugu kwa ujumla wamesumbuliwa sana kwa simu,
2. Wafanyakazi wangu wote, nawataja shania, angle na jacob wanisamehe sana,
3. Sarah Enock wa Morogoro,
4. Mr. Shuli ambaye alinirecomend
5. Mr Mdemu wa Arusha

Mawasiliano yangu ni;

+971523328490
+372557689780
kevinmulisa@gmail.com
 
Naona mods wamefuta nyuzi zote zinazomtuhumu tapeli Raimundo,vizuri.

Sasa endapo uzi wowote wa kumsafisha huyo bwana ukianzishwa na kuachwa hewani JF wajiandae kujibu hoja nzito,na haitokuwa tena kuhusu Raimundo bali JF yenyewe.
 
HAHAHAHAHA MAKINIKIA KWAHIYO HATA WEWE UNAMDAI?


MTU MZITO


Wanabodi salam.
Kuna memba humu anajiita Mtu mzito ambae amejitambulisha katika uzi wake huu Una swali kuhusu uchawi na uganga? Uliza ujibiwe.

Mimi ni mhanga wa utapeli ambao nimefanyiwa na huyu Jamaa.

Ilikuwa ni mwaka jana Decemba ambapo baada ya kusoma uzi wake nilishawishika na kufanya taratibu za kumtafuta baada ya kujihisi inawezakuwa nimelogwaa kutokana na maelezo yake.

Nilifanya mawasiliano naye kwa namba zake ambazo amezitoa kwenye huo uzi wake. Aliniambia yupo Tanga hivyo nikifika nimtafute .

Nilifanya safari hadi Tanga, nikashukia kwa rafiki yangu. Nilimtafuta asubui yake akanieleza anapatikana Mabawa hivyo nipande gari la Mikanjuni nishukie Mabawa msikitini na nikifika atamtuma mtu kuja kunichukua.

Nilifika pale na kweli nikamweleza nimeshafika, ndipo akasema nisubiri kuna mtu atakuja kunipokea na kunipeleka anapo patikana.

Kweli baada ya kama dakika 5 akaja binti kama wa miaka 18 ambaye alipo fika akanipigia na kuweza kujuana na kuongozana mpaka kwa huyu Jamaa.

Ni nyumba flani mbovumbovu ya familia ambayo jamaa amepanga chumba kwa ajili ya shughuli zake, kwani nilikuta watu wengine kwenye nyumba hiyo wakiendelea na shughuli za mapishi na wengine wanafua.

Yule binti akanieleza niingie hicho chumba na nivue viatu. Nilipo ingia humo ndani sikumkuta mtu. Ni chumba ambacho kimepambwa kiganga. Ni kweli niliona cheti cha mganga kikiwa kimebandikwa ukutani.

Baada ya muda ndipo akaja huyu jamaa Mtu mzito , nikijana wa miaka 24-28 hivi, mweupe na urefu wa wastani tu, tukasalimiana na akaanza kubadilisha nguo na kuvaa mavazi ya kiganga ambayo yalikuwa yametundikwa ukutani.

Ndipo baada ya kuvaa jamaa aka kaa chini na kuanza kuongea lugha yake, akasali kiislam na kuchukua pembe la ng'ombe na kuanza kupuliza na kuongea maneno yasio ya kawaida.

Ndipo niliposhangaa Jamaa anaanza kubadilisha lafudhi na kuanza kuongea lafudhi ya kimasai. Yaani ni kiswahili hikihiki lkn inakuwa kwa lafudhi ya kimasai.

Jamaa akaanza kunieleza nieleza eti nina matatizo kwenye mapenzi, kwamba kila ninae date nae tunaachana au tunagombana kila mara. Nikweli hii ilikwisha nitokea huko nyuma lkn haikuwa kipindi kile.

Nikasema ngoja niendelee kumsikiliza. Jamaa akasema eti nikishika ela huwa haikai, na huwa sijui naitumia vipi.

Lakini cha kushangaza, Jamaa akaniuliza nina matatizo mengine ni mweleze? Nilishtuka kidogo kwani kwanza tatizo langu kubwa nilitegemea angenieleza.

Ikabidi nifunguke, nikamweleza. Akaanza kunijibu ni kweli hilo tatizo unalo na pia huyo jamaa anaekufanyia hivyo kailoga familia yenu wote. Akasema jamaa anampango wa kukuua baada ya wiki mbili akutoe msukule. Pia umelogwa usifanikiwe, nyota yako imechafuliwa na hutopata kazi.

Ndipo nikamweleza tunafanyaje akanijibu kuna taratibu za kufanya ili kwanza kumfanya huyu mtu akome kukufuata, pili kusafisha nyota yako ili mambo yako yafanikiwe.

Akanieleza ili kufanikisha zoezi hilo inanibidi nilipia laki na nusu ambayo itahitaji kufanya kafara ya kuku, kwenda kununua madawa.
Kiukweli sikuwa na kiasi hicho cha pesa kwani nilisikiaga waganga wa ukweli huwa hawapendi kiasi kikubwa cha pesa katika kazi zao.

Ndipo nikamweleza sina kiasi hicho, ndipo akanieleza kama huna basi itabidi nikupe dawa tu ya muda uwe unaoga nayo ambayo itamfanya jamaa anaekuloga akusahau na nyingine utaweka kwenye maji ya vuguvugu uwe unakunywa na kunuia matatizo yako.

Akaniuliza nina kiasi gani nikamwambia nina 30,000 akaniambia niziweke kwenye sahani hapo mbele.

Ndipo akanipa hizo dawa na kuniambia nifuate masharti hayo then baada ya siku saba mambo yangu yatakua sawa. Niliondoka zangu.

Niliishi pale tanga kwa mwezi nzima nikitumia zile dawa kwa kufuata mashart yale. Lakini cha kushangaza hakuna kilichobadilika.

Ndipo Nikampigia akanieleza nitafute ela ili aingiee deep zaidi kwani tatizo langu ninkubwa. Ilinibidi niende maeneo karibu na ofisi yake na kuanza kupeleleza watu wa eneo lile.

Ndipl nikabahatika kuonana na mzee mmoja na kuanza kumpeleleza kuhusu Huyu Mtu Mzito. Yule mzeee akanieleza kuwa anamfahamu huyu kijana na ukweli ni kwamba huyu kijana alikuwa ni mtu wa dini na alikuwa yupo vizuri sana kwenye dini.

Akanieleza kuwa alishangaa alipo muona anajiingiza kweyw Uganga wa kutibu watu. Ikabidi nimweleze kisa kizima ndipo akanijibu mimi sio mtu wa kwanza kumweleza haya.

Yule mzee akanieleza pale hakuna mganga bali ni tapeli tu. Kama ninataka mganga wala nisihangaike na waganga wa mjini. Akanieleza sifa kubwa ya mganga ni yule anaekupa tiba na malipo hufanyika baada ya matokeo ya tiba.

Nilisikitika sana kwa utapeli huu wa waziwazi, kwani nilifunga safari yangu Dar mpk Tanga.

Nachotaka kuwaeleza wana JF tuepuke na matapeli kama hawa. Sisemi kwama hakuna waganga, bali waganga wanaokuja humu mitandaoni au wanao bandika mabango barabarani kuweni makini nao.

Nipo tayari hapahapa Mtu mzito akanushe kama nasema uongo
 
Matapeli wote twendeni kibiti mmeandaliwa makao mema ya MILELE
 
Back
Top Bottom