Asprin
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 68,223
- 96,083
Hii ya watu kuzuka PM na kuomba kukopeshwa hela za ada... nimeshazizoea sana.Nakumbuka mwaka 2008 kuna jamaa mmoja hivi alikuwa maarufu sana humu na tulikuwa tumezoeana kiasi [kiJF].
Siku moja akaomba nimkopeshe dola 1,200 ili aweze kulipa ada yake ya shule huko USA.
Ilibidi nicheke kwanza kwa kuwa hata na huo uthubutu wa kuomba nimkopeshe hizo hela.
Nadhani alijutia sana hicho kitendo na muda si mrefu akaacha kabisa kuchangia.
Ila nahisi bado yupo humu lakini kwa jina jingine na mara nyingi huwa anajitokeza kwenye nyuzi akiona kuna watu wananiponda. Huwa anaunga tela na kuanza kuniponda sana. Bado ana hasira na mimi😀.
Uzuri PM za namna hiyo wala hata sihangaiki kuzijibu...
kwangu mimi ni bora mtu aombe msaada, naweza kumsaidia.... Lakini mkopo??? Nehi!!