sawima
JF-Expert Member
- Jul 9, 2019
- 5,496
- 8,491
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]duhMzee anasimulia Zamani za Kale, Kipindi katoka akumuoa Mama yangu alitoka Kupata Kilaji Kidogo kwenye Kasenta Ketu hako ( Mji wetu) around 1960s.
Sasa ile anarudi home, yaani Kufika Junction ambapo kupafikia Nyumbani ni Kama Mita 200, akakutana na huyo Jamaa Mrefu. Mshua alikuwa anakula Fegi, anakwambia Fegi Ikadondoka Palepale, ile Kukimbia, aisee anakuta Karibia Kunapambazuka ndiyo akili inamrejea yupo takribani 25Kms toka home. Ndiyo akaanza Kujikongoja Kureje home karibia Kumepambazuka tayari.
Nawapa story ilimtokea Aunt yangu kabisaa ni member wa jf pia, (i'm sorry Aunt nashare story yako, usinachambe, lol)
Siku moja yupo mitaa ya kariakoo anashangaa shangaa madukani ghafla akatokea mzee mmoja wa makamo akamsabahi kwa bashasha sana, akamuita jina lake na ubin wake, Aunt alijaribu kuvuta kumbu kumbu ni nani huyu kabla hajapata jibu yule mzee akajitambulisha majina yake yote matatu, mmh Aunt akakumbuka mbona huyu niliambiwa alishafariki ila akashindwa kumwambia hilo, kwa hiyo na yeye akamchangamkia na kukumbushana mawili matatu ya watu waliowafahamu,
Yule mzee akamwambia Aunt yeye anafanya kazi duka la muhindi akamuonesha duka lilipo halikua mbali na pale, akamwambia akiwa anahitaji chochote kariakoo afike pale dukani amuulizie kwa jina X (akamtajia a.k.a yake) atampata na kumpa msaada, basi Aunt akashukuru na kuondoka zake.
Lakini alikua bado ana wasiwasi, akampigia simu dada yake (mama yangu), hivi fulani bin fulani unafahamu habari zake? Dada yake akamwambia looh mbona alifariki miaka mingi sanaaaa, tushaanza na kumsahau,
Aunt alitetemeka, alishindwa kwenda kwake akaenda kwa dada yake, akamuhadithia alichokiona, dada yake akampigia simu ndugu wa karibu kabisa na yule mzee akauuliza habari zake jibu ni lile lile ushasahau kama fulani alifariki na tukazika miaka takribani 10 sasa, aliugua kichwa tu akafariki, na alizikwa mkoa wa mbali na pale Aunt alipomuona,
Waliogopa kumwambia yule ndugu aliyoyaona Aunt, lakini shoga angu mimi alishikwa na homa kali wiki nzima, alibaki mdogo akajuta ile safari yake ya kariakoo, hahaha
Uchawi upo kama ambavyo Corona ipo.
Boost your Immune System to fight a Covid-19.
Miaka ya 90 somewhere hapa Tz katika harakati za kimaisha nilikuwa nalazimika kukatiza msitu mnene mida ya sanne hadi satano usiku nikiwa peke yangu karibu kila siku.
Basi ilikuwa kwamba kila ninapofika katikatii ya msitu huo nilikuwa nakuta joka kubwa (unene wake kipenyo sentimita 20) limelala kukatizaa barabara. Mimi si mwoga, sikuwai kumkimbia yule nyoka badala yake huokota mawe na kumshambulia hadi anatokomea.
Hii ilikuwa karibu kila s
Sent using Jamii Forums mobile app
DuhMiaka ya 90 somewhere hapa Tz katika harakati za kimaisha nilikuwa nalazimika kukatiza msitu mnene mida ya sanne hadi satano usiku nikiwa peke yangu karibu kila siku.
Basi ilikuwa kwamba kila ninapofika katikatii ya msitu huo nilikuwa nakuta joka kubwa (unene wake kipenyo sentimita 20) limelala kukatizaa barabara. Mimi si mwoga, sikuwai kumkimbia yule nyoka badala yake huokota mawe na kumshambulia hadi anatokomea.
Hii ilikuwa karibu kila s
Sent using Jamii Forums mobile app
Walikuwa misukule nini?Nakumbuka nilipokuwa na miaka kati ya 5 au 6,tulienda kijijini na wazazi wangu kuwatembelea Bibi na babu,kwavile Mimi ndo nilikuwa mjukuu wa kwanza kwa babu alikuwa anapenda kutoka na Mimi kila akiwa na mizunguko yake pale kijijini,siku moja tumeenda kwa rafiki yake mmoja alitukaribisha kwenye nyumba yake ilikuwa ni zile nyumba za nyasi za mviringo,Basi akatuacha ndan mm na babu Kuna kitu Kama alifuata nje,zile akili za utoto kuangalia juu ya ile nyumba nikaona watu wamekaa wanatuangalia huku wakiwa wamejipaka kama unga usoni,nilivyomstua babu ili na yeye aangalie juu sikuwaona tena wale watu pale juu mpka tunaondka na babu kwa yule rafiki yake.
Nakumbuka nilipokuwa na miaka kati ya 5 au 6,tulienda kijijini na wazazi wangu kuwatembelea Bibi na babu,kwavile Mimi ndo nilikuwa mjukuu wa kwanza kwa babu alikuwa anapenda kutoka na Mimi kila akiwa na mizunguko yake pale kijijini,siku moja tumeenda kwa rafiki yake mmoja alitukaribisha kwenye nyumba yake ilikuwa ni zile nyumba za nyasi za mviringo,Basi akatuacha ndan mm na babu Kuna kitu Kama alifuata nje,zile akili za utoto kuangalia juu ya ile nyumba nikaona watu wamekaa wanatuangalia huku wakiwa wamejipaka kama unga usoni,nilivyomstua babu ili na yeye aangalie juu sikuwaona tena wale watu pale juu mpka tunaondka na babu kwa yule rafiki yake.
Ndio,kwa maana walipotea ghafla na hii nilikuja kugundua baada ya kupata akili,kwa kipindi nilichukulia kawaida tu,Ila baada ya kuondka kwa yule mzee babu alikuwa ananiuliza umeona kwel watu, nikajibu ndio tena wamechafuka uson na unga
Ilikuwa misukule ile kwa maana tulienda kwa yule asubuh baada ya kunywa chaiBila shaka misukule au wachawi , aiseh inatisha
Sent from my iPhone using JamiiForums
Boya Sana wewe uliogopa nini..?Ilikuwa mwaka 2009,Kuna siku nimelala nikawa naota kuwa nimepanda daladala kituo cha mwenge naelekea posta basi nikawa nimekaa siti ya nyuma ya Costa. Basi kufika kituo cha Victoria akapanda mdada mmoja akaja kukaaa karibu yangu siti ya nyuma,tukaendelea na Safari kufika kituo cha mbuyuni yule dada wa ndotoni akaniachia kikaratasi kina namba za simu akashukia kituo cha mbuyuni,baada ya mda nikastuka kutoka ndotoni kucheki saa ya simu mda huo ni saa tisa za usiku. Basi nimestuka kila kitu kwenye ndoto nilikuwa nakumbuka mpka namba za siku,kesho yake nawahadithia ndugu zangu nilichoota ndotoni na mpka namba za siku zilizokuwa kwenye karatasi nazikumbuka,wakaniambia tujaribu kuzipiga. Baada ya kupiga anapokea msichana ana lafudhi ya kiarabu anaitwa Nasrat na anaishi sinza,nilichofanya ni kuvunja laini na kutafuta line nyingine mpka leo sielew ile ndoto na coincidence zake
Hili lina ukweli na pia lina ukakasi kidogo. Hapo kuna mambo mawili huenda huyo dada akawa ni miongoni mwa majini wale wanaopendaga kuishi na binaadam.Boya Sana wewe uliogopa nini..?
Ungechukua toto hilo nyie kila kitu mnaonaga negative tu kwanini usiseme bwana kakuonyesha kimwana wa kuoa!
Mkuu Kama unaikumbuka namba yake nitumie halafu ntakupa mrejesho nimemfanya nini!
Hili lina ukweli na pia lina ukakasi kidogo. Hapo kuna mambo mawili huenda huyo dada akawa ni miongoni mwa majini wale wanaopendaga kuishi na binaadam.
Pia huenda ikawa ni mdada ambae ameenda kwa mganga kutafuta mchumba labda there fore ndo wachumba wanapatikana kishirikina kwa njia hiyo ya kuwaotesha wachumba wakiwa ndotoni😀
Nimejaribu kudadavua tu.. Jamaa kaogopa bure aisee mi nikipata bingo kama hilo silazi damu.. 😀😀
Daaa ila we jamaaNimejaribu kila njia ya kukutana na haya mambo lakini wapi
Nikisikia huyu bibi mchawi au huyu mzee ni mshirikina mimi kazi yangu ni kuwauliza tu hivi mnapata faida gani kuroga?
Yote hiyo natafuta huo wanga
Sina woga labda ndio sababu nao wananipuuza
Nikaona isiwe shida nikawa naenda kukaa makaburini manane ya usiku maana nikuambiwa ndio mda wa wawangaji kuwanga
Napo sikuambulia kitu zaidi ya mara mbili jamaa kunikimbia huku wanapiga yowe [emoji23][emoji23]
Yaani mpaka haunted house nimeingia sana zaidi ya baadhi ya vyumba kuwa baridi la kufa mtu lakini hakuna kitu cha kunifanya nikimbie
Kuna kizee Fulani waliniambia huwa kanapaa usiku
Nikakauliza naomba lift
Kakasema ya wapi tena nikakaambia kwenye ungo kalisonyaa mpaka kanapotea [emoji23][emoji23]
Sent from my iPhone using Tapatalk
Shenzyy kabisa uoga tu chukua namba mkuuBoya Sana wewe uliogopa nini..?
Ungechukua toto hilo nyie kila kitu mnaonaga negative tu kwanini usiseme bwana kakuonyesha kimwana wa kuoa!
Mkuu Kama unaikumbuka namba yake nitumie halafu ntakupa mrejesho nimemfanya nini!
Acha nami nishee story yangu japo si mzuri sana katka uandishi.
Ilikua 2010 Dar es salam enzi hizo nikiwa mwanafunzi wa chuo kimoja hapo. Ukweli sikukutana nakiumbe cha kutisha bali ni binaadam alienifanya nibaki na sintofaham na maono tofauti ktk maisha.
Sikubahatika kupata chumba ktk hostel za chuo ikanibidi nipange kitaa flan uswahilini karibu na mwenge hapo. Maisha yalikua fresh tu fadha house alikua na wake wawili na watoto kadhaa hapo kijana mkubwa wa mwenye nyumba alitokea kua mwanangu sana story za hapa na pale, jamaa alikua mstaalabu sana na anasura ya upole by that time alikua kama ana 30 yrs nakuendelea.
Tukio lilotokea lilinifanya nibaki mdomo wazi ni siku moja mida ya saa tisa kasoro huyo bro aliniamsha kwa kugonga mlango nlisita kuitika lkn mwisho nilifunua nakumkuta amemkamata kijana mmoja wa makamo. Jamaa akanambia kwamba huyu ni mwizi na huwa anaibia watu hapo mtaani. Nikamuuliza vp ushahidi unao akadai hana ila amemkuta na kisu mfukoni. Nilitaka kuacha kumpa ushirikiano ila nikaona nimsaidie huyo kijana asijedhurika kwani hakukua na ushahidi wowote. Nilimshauri jamaa kua tuamshe majirani au ndg zake jamaa akawa mbogo. Ilibidi nimfate kwanyuma akiwa amemkamata yule kijana shingoni tukielekea nyumba iliokua opposite na hii tunayokaa. Nilipata bahati ya kumuuliza jamaa akakubali ni kweli hapo aliwahi iba shati na sendoz. Nilijua itakua kesi ndogo lkn tulipofika kwa huyu jirani aligonga mlango mara mbili tatu huyo mzee akafungua na kuelezwa dhumuni la sie kuwepo hapo. Alimtazama yule kijana kwa macho ya dharau na kuulizia mimi kwani hakuwahi niona maeneo hayo ndo jamaa akanitambulisha kama mpangaji wao. Yule mzee haraka bila uoga alitupa jukumu tumuue huyo dogo then tukimaliza tumchome moto hapo hapo. Nilihisi kuogopa nikaona ni kama mzaha vile kwani tulikua wawili tunaopewa jukum hilo. Alipomaliza kufunga mlango wake mzee yule nilimwambia huyu mshkaj kwanini tusimteme tu dogo coz vitu alivyoiba nividogo sana. Msela alinifokea sana na kunipolomoshea matusi makali. Ilibidi niwe mtazamaji asikwambie mtu kifo ni kitu rahisi sana, dogo alishushiwa kipigo hevy ngumi na mateke mpaka akazimia ndipo jamaa alipoanza kutumia mawe yaliyokua pembeni . Ilifika muda dogo alipiga mayowe maskini it was too late, jamaa alihitaji kuua siku hiyo. Baada yakama dakika saba dogo alivuta nikimshuhudia alimsihi yule jamaa akimtaja kwa jina kua unaniua bure bro mimi ni mdogo wako, haikusaidia kitu dogo alipigwa taili mbili na kumwagiwa mafuta ya taa. Aliwaka mpaka mwisho. Niliogopa sana na usiku huo sikulala tena taswira ya kile kipigo ilikua ikinijia kichwani. Niliogopa sababu dogo alouwawa na huyu jamaa ni wa pale mtaani vp mimi mgeni. Nakwanini jamaa hakutaka watu waamshwe na dogo mbona hakua amemuibia huyu jamaa kitu.
Ilibidi iwe siri yangu mpaka nilpokuja kufahamishwa na majirani wengine juu ya kuokotwa mara kwa mara maiti zisizo julikana mtaani. Ilibidi nihame kimya kmya na kujiapiza kua sintokuja kupanga uswahilini tena na hawa binadam wenye sura nzuri za upole niishinao kwa tahadhari kubwa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kiroho safi tu mzee namkabidhi mtimanyongoUnaweza kuibuka na jini wewe😄