Matukio ya kutisha niliyowahi kushuhidia katika maisha yangu ni haya yafuatayo sitokuja kusahau kabisaaa[emoji41]
1. Nikiwa mwanafunz wa primary huko nyanda za juu kusini, maeneo ya nyumbani kwetu nikiwa naishi na shangazi yangu pamoja na wazazi japo wao walikua busy kidgo , shangazi alikua ndo kila kitu kuhusu kushiba usafi wa home nk. baada ya kutoka shule nachukua maji kwenye dish naenda kuoga nsmuacha shangazi Yule pale anapika, baada ya kuoga natoka zangu nashtushwa na sauti ya shangazi akisema maneno ya kiluga chetu akitaja jina langu, mfano, John kimbia mwanangu nyoka huyo anakufuata niliruka nilikimbia adi jikoni ile kugeuka nyuma naona joka la ajabu ambalo sijawahi ona kabisa lilikua ni joka linalovutia kwa kuliangalia kwani lilikua na rangi za aina tofauti tofauti kana kwamba lilichorwa na , lilikua na mistari ya kuvutia Sana baada ya shangazi kuendelea kupga kelele na kulia taratibu lilirudi zake bafuni toka siku hiyo nligoma kabisa kuoga mule.
2. Nikiwa form two usiku bwenini tukiwa tumelala ghafla Kama bluamshwa vile ile kufunua shuka namuona mwanamke akiwa amebeba mtoto mgongoni, Yule mwanamke alikua anatembea tembea mule bwenini kana kwamba Kuna mtu Ana mtafuta lakini hamuoni, nilimuona akiamia chumba kungne baada ya muda kidgo kupita nilimuona akija adi nilipokua Mimi alisimama kwa muda kidgo mm nikajifanya nimelala ili asinigundue baadae aliamua kuondoka zake, asubuhi nlisikia watu wakilalamika wameamka tofauti na waluvyo lala( waliamka kichwa kikiwa upande wa miguu, sio mmoja zaidi ya watatu wali lalamika sikusema nliyoshuhudia.
3. Baada ya kuamia kwenye shule flani huko Ruvuma nikiwa form 4 nikiisha ndgu yangu mwalimu tukiishi Kota za walimu, siku hiyo nikiwa darasani Mara ghafla nilipata uchovu wa ghafla kikiwa na mwalimu darasani niliomba ruhusa ili nikapumzike nliruhusiwa nlipofika ndani nikakaa kitandani MAAJABU ghafla km usingizi mzito Sana wa macho ulinijia na Kuna nguvu ilikua ikinisukuma kwa nguvu kitandani nikiwa miguu iko chini MAAJABU, nliona kiumbe sio kiumbe sijui ni Nini kile alikua km mwanamke akiwa kwenye umbile la maji yanayo cheza cheza ila yakiwa yameform umbile la binadamu kabisa kuanzia kichwa adi chini lakini hayamwagiki, alikukuja akanikalia hapa kiunoni na kuanza kunipa denda na mikono ikinipapasa nyeti zangu kwa nje, nlijitahidi kukwepesha mdomo lakini sikuweza alifanikiwa kudenda, nlipojitahidi kupapasa mikono sikushika maji nilishika vidole ambavyo vilikua sio vya binadamu vilikua Kama vidole vya miguu ya kuku hivi na kucha zake ,nlijilazimisha kumshinda lakini nilishindwa baada ya dakika kadhaa alitoweja Cha AAJABU akili ilirudi vema sio katika uchovu nliotoka nao darasani. .
4. Nikiwa advance level shule flani ya jeshi hapa Tz, siku flani bwenini usiku wanafunzi wamelala , Kama nimeashwa hivi naona Kama mtu hivi akiwa Hana miguu Wala kichwa yaani Kama mavazi meusi yameform umbile la binadamu akiwa ametokea mawingu ya chini aridhini anakuja juu( jitahidi kunielewa ) akaja adi nilipokua nimelala akiwa ameshika fimbo akiinyosha kwangu shingo ikageukia upande wa ukutani kwahiyo sikuelewa alichokua anafanya na nilijaribu kurudisha shingo ili nimuone lakini nilishindwa baadae alipotea , kesho yake nlifukuzwa shule moja kwa moja baada kukutwa asubuhi bwenini muda nliopaswa kua assemble, na ilikua sio kawaida yangu kukaa bwenini muda huo, na nlibaki kwa sababu nlikua nikitafakari kile nilichokiona usiku wake nlipopewa adhabu nlikataa katakata na kumtisha mwalimu, sikua na tabia za watukutu pale shuleni kwani nlikua mwanadini Sana nikihudhuria vipindi vya maombi pasi kukosa SITOSAHAU, nliharibikiwa Sana najitahidi kusahau lakini nishindwa
SITOSAHAU HAYO MAMBO KAMWE
Sent using
Jamii Forums mobile app