Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

duhh!! noma sana,, lile ziwa la kilozi ilikuwa lipite na ww mzebaba, pole sana, yan wachawi na wezi hawakutakiwa kbs kuwepo duniani hapa.
Nimeandika hapo na usingizi mwenyewe umekata maana hata chumba nilichopo nakiogopa ila mambo haya ni nguvu ya kishirikina na ninadhani ule ulikuwa ndio mwisho wangu ila Mungu mwenyewe alinipigania ila uchawi upo na unafanya kazi vizuri sana ile kitu ilikuwa planned na walioplan mmoja akiwa ni jirani yetu japo kwa umri sasa hivi ni mzee sana na wenzake walishatangulia mbele ya haki ila kiukweli mambo ni mengi mie ilikuwa ikifika usiku ujue raha sina maana najua kumekucha hakuna kulala moja ya tukio kuna siku pale home baada ya tukio hilo ilikuwa jmos asubuhi nikaambiwa nikateke maji mtoni nikazingua nikaendekeza kucheza kuja kustuka bi mkubwa ananiita huwezi nikakimbilia porini kwa kuogopa kuchapwa toka saa nne aasubuhi ajabu ni kuwa nilikuwa sijui polini nimeenda kutafuta nini na kumbuka tabora kunaoongoza kuwa na nyoka koboko basi mie ndio nikaenda huko zungunga sana jua la saa nane nipo huko nakula matunda pori tu nikawa nimesikia joto katika kuzunguka zunguka nilitokea sehemu kuna maji mengi kama ziwa na lile joto nililokuwa nalo nikasema ngoja nivue nguo nioge nikavua ila roho ikasita kuoga nikavaa nikaondoka nikajikuta sijui njia ya kunirudisha nyumbani na kigiza kinaingia Mungu saidia kuna mzee mmoja wa kijiji cha pili alikuwa anachunga ng'ombe akaniaona na anawajua pale home ndio kunirudisha nyumbani ajab mama hakunichapa na alikuwa ameshanitafuta kwa washikaji wangu wote hakunipata hivyo baada ya kuniona kwanza nimepauka nilipewa tu maji ya moto kuoga na kula nikashida nikaenda kulala sasa cha ajabu asubuhi ambayo ilikuwa j2 nikawasimulia sehemu nilipoona lile ziwa la maji ile sehemu hakuna historia ya kuwa ziwa la maji hata bwawa kuna miti ya Milumba na mitundu kwa wingi kama unaijua, wazee nao ikabidi waanze kuhangaika ndio mambo kutulia ila hii dunia ina mambo sana ukijiona mzima unalala vizuri unaamka salama hakuna wenge lolote mshukuru sana Mungu mie wazazi walikuwa watu wa dini sana walikuwa hawaamini uchawi ila waliamini
[/QUOTE]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah imenikumbusha miaka ya 90s nikiwa Tabora wilaya moja hivi kijijini nikichukua elimu ya msingi shule yetu ilikuwa upande wa magharibi kuna makaburi halafu shule ina miti kibao ya mikaratusi,mikorosho mijohoro mizambarawe na miti fulani hivi inatoa ubani upepo ukipiga inavuma kama gari, dah nakumbuka hiyo siku niliamka kwenye kigheto changu pale home kama saa nane hivi mabalamwezi imekubali nje maana ilikuwa wiki ya mwalimu mmoja hivi kusimamia usafi na wechelewaji na ukichelewa unapata bakora za miguuni na lile baridi la kijijini balaa mwanaume mbalamwezi ile nikajua kumekucha nikanawa faster faster hata sikuwastua wazazi ambapo sio kawaida huwa lazima niwaamshe kwenye gheto lao mzee nikanyanyua ufagio mkononi na kidumu cha maji mbio kwenda kabla ya kufika shule kuna kipori flani lazima ukipite ndio ufike shule mwanaume sikujari japo njiani sikuona mtu yeyote hiyo haikunistua mie nilijona mshindi leo nawahi namba shule, aisee nimepita chini ya mikorosho na hiyo miti mingine bila kujari nahisi akili haikuwa yangu nakumbuka nafika shule nikakimbilia darasani nafika mlangoni nilichokishuhudia acha niliona moto mkubwa unawaka mule na kuna watu wamekaa kama wako kwenye kikao halafu wote wakaniangalia ila sura sikuziona hapo ndio akili ikarudi kwamba nimezingua niligeuka mbio kurudi home halafu ule upande wa makaburi nilishuhudia watu wakiwa na mguu mmoja wanaruka ruka kwa mstari mbio zangu nilikuwa nahisi kuna kitu nyuma kinanifata kugeuka nyuma niliona mtu mrefu sana kichwa hakionekani ila kavaa vazi refu linag'aa kama mbaramwezi ilivyokuwa inag'aa mwanaume niliongeza speed nilienda nikaingia na mlango mpk ndani yule jini sijui nini nilipokaribia nyumbani nilisikia msonyoo mmoja hatari sana wazazi wakaamka kufungua mlango kuja kunikuta sijitambui wakanichukua nikaenda kulala kwao asubuhi ndio kuwaelezea ni moja ya tukio ambalo huwa sipendi kabisa kulikumbuka maana baada ya hapo mpk leo kuna vitu huwa naviona ambavyo sio vya kawaida na niliwasumbua sana wazazi baada ya hapo . nimejaribu kufupisha ila kuna mambo mengi sana kwa ule usiku na miaka ile niliyashuhudia baada ya ilo tukio.
Mkuu hiyo shule ya msingi sio Mwenge huko Tabora
 
[emoji44][emoji12]
Baby nawe umo..?
Ntakuja unifanyie maombi maalum ili nami nianze kuamini haya mambo!

Kuna sehemu nilikuwa nalala kwenye hicho chumba kila siku nalala vizuri tu!..
Kuna kipindi akaja anko wangu nikampisha akawa analala humo,siku ya siku naamka asubuhi jamaa sauti imemkauka kuuliza ati alikabwa usiku akaanza kufanya maombi tena kwanguvu!!,wengine walikuwa wakimsikia ili mhuni hata sikumsikia[emoji23][emoji23]
Mi niliona kama mzinguaji tu! We mi ndo nilikuwa doni nalala kwenye hicho chumba na sikuwahi kukabwa Wala nini!!
Yeye mgeni ana siku kadhaa ati wamemdanda![emoji23]
Dah! Wakati wengine wakisikia kitu juu ya bati ndo wanajifunika shuka zaidi,kenge Mimi ndo nilikuwa natoka nione kuna nini..?
Wakubwa walinikataza ila kenge sijawahi kuacha hiyo tabia na hata ukitoka unakuta ni linyau tu linadili na yake sometime huoni kitu!

Nyinyi hayo mauzauza huwa mnaonaje..??

Kuna mtu wangu wa karibu alishawahi sumbuliwa na hayo mambo ya kichawi sana tu! Na hivyo ndivyo tulikuwa tukiamini.. tembea sana kwa waganga lkn wapi matatizo ndo palepale! Mpaka walivyochoka wakaacha hayo maswala mbona mtu alirejea ktk hali yake ya kawaida kabisa!! Afya ikaimarika hata kuongea kukaingezeka n.k
Alipona akawa normal kabisa!

Haya mauchawi mi nahisi mtu yanaweza kumtesa mtu kisaikolojia tu akadhoofika mpk ukahisi huyu mtu anatatizo kweli!! Yapo mengi tu mtu usipochubguza lzm uamini ni uchawi n.k kumbe sometimes ni mauzauza ambayo yanaweza tengenezwa na ubongo!!
Wengi Sana wanasumbuka kisaikolojia ila hawajui...

Hayo mengine ntawaachia wahusika[emoji12][emoji12]
Ila natamani sana kuujua ukweli kuhusu hilo li ulimwengu la kiroho na kichawi!.

NB: Leo ntakuja kukuweka mguu pande[emoji12][emoji6]
mimi pia sijui ni miongoni mwa hao watu ambao macho yamefungwa, sijui ndio nini mm huwaga ni mgumu sana kulala usingizi ila nikilala huwa nimelala, jambo lolote la hatari watu wengine wanaweza kulisikia mi nisisikie, kuna mwaka nikiwa young kama darasa la 5 hivi Bundi aliliaga mti ambao uko pembeni kabisa na dirisha langu sikusikia hata robo wakati huo karibu mtaa mzima wanamsikia.

haya mambo ya sijui kumwagwa mchanga juu ya bati, watu kutembea wataskia wote mimi nalala sisikii hata tone.

Labda ujanja wa ndoto, nikiota kitu au kusema (foresee) inakua hivyo hivyo imepelekea watu wangu wa karibu hawatakagi nitie neno kwenye jambo lolote wanalotaka kufanya maana neno langu haliangukii chini
 
Mimi nitasimulia kisa kimoja tu, tena cha utotoni maana kiliniogopesha sana kwa umri ule wa miaka isiyofika hata kumi. Hiki ni kisa kati ya visa vingi vya nguvu za giza nilivyovishuhudia, na ninavyoendelea kuvishuhudia mpaka kesho. Mnivumilie na mnisamehe mdogo wenu maana nitaandika kurasa ndefu.

Picha linaanza pale marehemu mama(PKA mama yangu mzazi, na Mungu akurehemu kwa rehema zake) alipoolewa na baba yangu. Kwa miaka zaidi ya mitatu, mama hakuweza kukaa na ujauzito zaidi ya miezi mitatu, na badala yake mimba ziliharibika.
Mama aliisha kwa masimango, na kuonekana sawasawa na papai linalobeba corona badala ya vitamin! (Ni mchezo uliokuwa ukichezwa na majirani zetu, wenyej wa Kigoma, na Ukweleni hapo)....Lakini mama hakuchoka kuvumilia, na kumwomba Mungu.

Hatimaye mama akashika ujauzito wangu, haukutoka tena, na nikazaliwa pale MNH, na nikaitwa jina la "dawa ya Mungu", maisha yakaendelea kijijini kwetu Boko.

Katika makuzi yangu, utotoni wazazi wangu walikumbana na matukio na changamoto nyingi za kukatisha tamaa. Kuna wakati usiku mama alimka na akakuta sipo kitandani, ananitafuta kwa mda mrefu wakiwa na mzee, hatimaye wananikuta chini ya uvungu wa kitanda nalia, au wananikuta kwenye pembe ya nyumba, mama alikuwa akilia weee, hatimaye maisha yanaendelea. Ilifika mda nikiwa na umri wa mwaka na nusu, nililishwa nyama ya kisigino ya maiti, niliumwa sana kutikana na hili chupuchupu nilambe udongo, wazazi walipambana, Mungu akasaidia, nikatoka salama.

Balaa kwa macho yangu, lilikuwa hapa sasa. Nikiwa darasa la pili, miaka hiyo ya tisini nilitokewa na tukio la kwanza, mubashara ambalo lilinitisha sana maana hapa niliona kwa macho na akili zangu. Usiku nikiwa nimelala ghafla nywele nikahisi zinasisimuka, damu inaenda mbio, na mwili unachemka....ghafla nikashtuka na kuamka paaap! Uso kwa uso na mwanaume aliyeshika kitanda changu, miguuni mwangu nywele zake zinawaka moto mkubwa ila haziteketei, macho yake yanawaka moto kama mkaa wa moto, na mikucha mirefu.

Kulia kwangu, wanawake wanne wakiwa uchi kabisa, wamebeba vyungu kichwani vinawaka moto. Kushoto kwangu wanaume watatu wapo uchi nao wamebeba vyungu, nao vinawaka moto, na mtu mmoja wa kiume(jini) mrefu akikaribia kugusa paa, mweupe kwa rangi(mwarabu) amevaa miwani mweupe, kanzu ndefu, nyeupe mpaka chini, na alikuwa na ndefu ndefu kiasi.

Tukakaziana macho sana, nikawa nawageukia wote mithili nataka niamke niwarukie ila nahisi nazuiwa, nataka kupiga kelele sauti haitoki. Baada ya dakika kama 3 au 4, nikaanza kuuona ukuta kwenye pembe ya nyumba, mubashara unafunguka na wanaanza wanawake kutoka nje kinyumenyume, wakifuata wanaume, na yule jini anakuwa wa mwisho. Hatimaye ukuta unajifunga tena baap! Na hatimaye ndo sauti inatoka mamaaaaaaa........!!!

Mama na baba wanakuja, wananikuta nalia na nimeloa jasho mwili mzima. Hatimaye nawasimulia, mama analia sana, ananikumbatia, na anamlilia Mungu, ananichukua ananipeleka chumbani kwake kwenda kulala nao chumbani kwao. Mama akaniambia watoto ni malaika, huona majini na wachawi ila ukikua hutowaona. Ila haikuwa hivyo mimi mpaka kesho hawa washenzi hawakatishi anga zangu.

Asubuhi ikafika, nikajiandaa kwenda zangu shule, na mama akaniambia kwa sasa hali ilipofikia itabidi niwe nalala na mbwa chumbani kwangu, yaani mbwa anafungwa kwenye mguu wa kitanda changu. Hii ilinisaidia ila hawa washenzi walimuua mbwa wetu(PKA Jeck) ni mbwa aliyepambana sana na hawa washenzi, ila usiku mmoja alipiga kelele kushtuka damu zinamtoka puani na mdomoni ndo ukawa mwisho wake Jeck wangu.

Hili ni tukio mojawapo kati ya matukio mengi niliyokumbana, na ninayokumbana nayo. Ila kama ukilala unaamka tu flesh bila kuona haya mavitu, muombe Mungu akujalie hivyo hivyo. Haya mavitu yanatisha sana.
Asanteni, na poleni kwa kuwachosha!

Nakumbuka siku moja usiku niko na mama jikoni(majiko ya nje) nikawa nasinzia mama akanambia niende ndani nilale ataniamsha msosi ukiiva. Kulikuwa na mvua inanyesha.
Ile nipo njiani naelekea ndani nilikutana na mwanga mkali wa kutisha ukanirusha nikaanguka chini nikawa nimezubaa sielewi nini kinaendelea ndo baadae kama sekunde kadhaa nikasikia muungurumo wa kutisha tena ndo nikagundua ni radi mama akaja kunichukuwa pale siku hiyo hata sikula na nililala kwa kuweweseka kila nikifumba macho nakiona kile kitu cha ajabu. Hakielezeki kwakweli.
Kesho yake tunaamka tukakuta mfenesi unaanza kunyauka kumbe ile radi iliupiga ule mfenesi.

Siku nyingine niko nyuma ya nyumba kwenye saa 1:30 usiku napaki gari(nilikuwa natengeneza gari za magome ya mgomba) so nilikuwa nimetengeneza kaeneo nyuma ya nyumba kakuzitunzia gari zangu nikimaliza kuzichezea
Nikiwa naendelea kuzipanga kulitokea kitu kama mshale/mkuki unamwanga kwa mbele mithili ya wekundu wa chuma kilichochemshwa kwa moto mkali. Hiki kitu kikapita juu kidogo ya nyumba kikaenda kuishilia migombani mpaka upeo wa macho ulipoishia. Cha ajabu ni kwamba kilipita karibu sana kiasi kwamba mtu ungeweza kuruka ungekikamata so haikuwa kimondo ila pia pamoja na kupita migombani ambapo hua imeota zigzag hakikugonga mgomba hadi kinaishilia

Siku nyingine tumetoka kuchunga mbuzi nafungua mlango wa nyumba ya mbuzi mwenzangu kanishikia kibatari kwa ajili ya kunimulikia wakati wa kuwafunga kwenye mambo zao zilizopigiliwa chini mule ndani mwenzangu akaona vitu viwili vinang'aa darini kwenye kona akanionyesha anauliza vilikuwa vitu gani si ndo kumulika vizuri tunakutanisha uso kwa macho na bundi mweusii. Aisee asikwambie mtu huyu ndege ana sura ya kutisha, nilijikuta mkojo unapita huku napiga kelele wakaja wakubwa wakamfukuza. Kwa kweli ile sura ilikuwa inaniijia kichwani karibu wiki nzima nikiwa sehem yenye giza
 
Mi sijawahi shuhudia mauzauza yoyote ila hadi leo nashangaa kuna siku nimeota mama flani hapa mtaani (namjua) alikuwa ananilazimisha kula nyanya,nyanya zilikuwa nyingi sana ananisokomezea mdomoni mimi nameza tu....ajabu nilipokuja kushtuka nikajikuta nimeshiba halafu tumbo limejaa kishenzi yaani
 
Shukuru Mungu kama hujawahi kutana na hayo mambo,
Mambo hayo husababishwa na Kama kuna Ndugu wana michezo hiyo, Majirani au watu wanaokuzunguka maeneo unayoishi na husababishwa na Husda,michezo,mazoea
Hayo Mambo bwana mkubwa yapo sana sana tu, kama hayajakukuta utayadharau na kupuuza, Kuna muda unakutana na majaribu mpaka unajiuliza hivi kweli mm huwa nasali, kama nasali mbona bado siko imara huyu Mungu ninae miomba ni wa wapi,mbona wengine hawakumbani na hizi zahama..

Mfn: Sumbawanga unaweza sikia vitimbi vingi sana ila wewe ukapangiwa kazi huko ukaishi vzr na ukakataa kuhama kabisa, ila mwinhine anaweza pangiwa huko mwezi mmoja tu akakutana na vitimbi vya hatari haya mambo yanaendana na Ukoo sometimes
 
Dah imenikumbusha miaka ya 90s nikiwa Tabora wilaya moja hivi kijijini nikichukua elimu ya msingi shule yetu ilikuwa upande wa magharibi kuna makaburi halafu shule ina miti kibao ya mikaratusi,mikorosho mijohoro mizambarawe na miti fulani hivi inatoa ubani upepo ukipiga inavuma kama gari, dah nakumbuka hiyo siku niliamka kwenye kigheto changu pale home kama saa nane hivi mabalamwezi imekubali nje maana ilikuwa wiki ya mwalimu mmoja hivi kusimamia usafi na wechelewaji na ukichelewa unapata bakora za miguuni na lile baridi la kijijini balaa mwanaume mbalamwezi ile nikajua kumekucha nikanawa faster faster hata sikuwastua wazazi ambapo sio kawaida huwa lazima niwaamshe kwenye gheto lao mzee nikanyanyua ufagio mkononi na kidumu cha maji mbio kwenda kabla ya kufika shule kuna kipori flani lazima ukipite ndio ufike shule mwanaume sikujari japo njiani sikuona mtu yeyote hiyo haikunistua mie nilijona mshindi leo nawahi namba shule, aisee nimepita chini ya mikorosho na hiyo miti mingine bila kujari nahisi akili haikuwa yangu nakumbuka nafika shule nikakimbilia darasani nafika mlangoni nilichokishuhudia acha niliona moto mkubwa unawaka mule na kuna watu wamekaa kama wako kwenye kikao halafu wote wakaniangalia ila sura sikuziona hapo ndio akili ikarudi kwamba nimezingua niligeuka mbio kurudi home halafu ule upande wa makaburi nilishuhudia watu wakiwa na mguu mmoja wanaruka ruka kwa mstari mbio zangu nilikuwa nahisi kuna kitu nyuma kinanifata kugeuka nyuma niliona mtu mrefu sana kichwa hakionekani ila kavaa vazi refu linag'aa kama mbaramwezi ilivyokuwa inag'aa mwanaume niliongeza speed nilienda nikaingia na mlango mpk ndani yule jini sijui nini nilipokaribia nyumbani nilisikia msonyoo mmoja hatari sana wazazi wakaamka kufungua mlango kuja kunikuta sijitambui wakanichukua nikaenda kulala kwao asubuhi ndio kuwaelezea ni moja ya tukio ambalo huwa sipendi kabisa kulikumbuka maana baada ya hapo mpk leo kuna vitu huwa naviona ambavyo sio vya kawaida na niliwasumbua sana wazazi baada ya hapo . nimejaribu kufupisha ila kuna mambo mengi sana kwa ule usiku na miaka ile niliyashuhudia baada ya ilo tukio.
Mwamba pole sana kwa uliyoyapitia. Si vibaya uka share nasi hayo unayoendelea kuyapitia hata kwa ufupi kama ulivyofupisha hichi ulichotupatia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una bahati ulikuwa bado mtoro huyo mrefu alokuwa anakufata nyuma huwa mshenzi sana sema haui ila huwa anasumbua balaaa. Hapendi kukimbiwa. Ukimkimbia imekula kwako, we akija jifanye humuoni ikiwezekana kaa chini ama lala chini ili apite. Ila komesha yake vua nguo zote utembee uchi ama vaa kwa mtindo huu. Anzia chupi igeuze nje ndani halafu ivae mbele nyuma fanya hivo kwa nguo zote soks na viatu kulia kushoto. Halafu tembea kawaida tu hatakiona. Ungekuwa mtu mzima ungekimbia ukastuoia akili zinarudi upo kijijiji cha 8. Ndo ungejiuliza umefikaje huko

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo Ishu Ilimpata Mzee wangu. Alikuta Yupo Umbali wa Kama 20KM hivi.
 
Back
Top Bottom