Naomba nimuite ndugu
Mshana Jr aweke neno. Haya mambo yapo kwa kuusema usemi, "lisemwalo lipo,kama halipo, litatokea."
Binafsi sijawahi shuhudia chochote kwa macho yangu ya nyama zaidi ya haya...
Wakati flani nilikaa maeneo ya bonde la mpunga, hapo wakazi wake wengi ni waswahili na mie maisha yangu ilikuwa kwenda kazini kurudi najifungia ndani.
Usiku mmoja nimelala chumbani kwangu nikastuka naona taswira kama ya kibibi kinaingia dirishani kwangu kwa njia za kimiujiza huku anapiga kelele. Nikaanza kusema kwa jina la Yesu tokaa (nililelewa kwenye familia za kilokole) kikapotea nikarudi kulala.
Siku ingine nimelala nastuka kabisa nasikia mtu amevuta nywele zangu za utosini kwa kuzikata na kucha ya kidole chake na baada ya hapo akatoweka sikuona mtu ila hali ya nywele kutoka kwenye utosi wangu niliisikia kabisa japo sikusikia maumivu na hapakubaki kipara nilikuwa na nywele ndefu.
Mara nyingine inanitokea usingizini napambana na nguvu za giza usingizini maana ya kwamba kama mashetani au kitu kinanikaba. Kisha sauti inaniambia kemea, sali nikianza kusali napata nguvu na kile kitu kinakimbia, baadae kinarudi tena nakemea naongeza nguvu nazidi kukemea halafu najiona nguvu za maombi zinaniongezeka ghafla nastuka kutoka usingizini najikuta naendelea kusali na inaweza kuchukua hata nusu saa nzima kama si lisaa ndo maombi yanakata, nikijaribu kuacha kusali nashindwa nakuwa sina utashi wa kunyamaza hadi hali ya kusali iishe..
Huwa najiuliza kama ni ndoto nilipostuka ilitakiwa ikate, sasa nastuka bado najikuta naendeleza kusali kwa kukemea, safari moja hadi nikainuka kitandani out of my will nikiwa nasali.
Sijajua kama hayo nayo ni matukio ya kutisha au vimbwanga ama laah...
Nachojua, ulimwengu wa roho upo na unapande mbili, nuru na giza. Si mtu wa dini sana ila...lisemwalo lipo kama halipo litatokea.
Si muamini wa mambo ya kishirikina na yafananayo ila kwa dini yangu ya kikristo niliyokulia natambua ulimwengu wa giza unamazagazaga kama hayo waliyoelezea memba wengine halo juu.