Ilikuwa mwaka 2004 Mzee wetu alihamishiwa kikazi mkoa fulani kanda ya ziwa, ikabidi familia yote tuhamie huko..
Kutokana na uchache wa nyumba za serikali akapangisha nyumba mtaani.
Mzee akapata safari ya kikazi kwa muda, Maza nae akawa chuo mkoa mwingine.. Nikabakia mimi na brother.
Mambo yakaanza, siku ya kwanza tukasikia madirisha ya nyumba yanafunguliwa na upepo mkali unaingia ndani ilikuwa saa nne usiku, tukatoka na mapanga kutafuta mwizi hakuonekana.
Siku ya pili mlango ukafunguliwa na kiumbe kilichoingia kikawa kinafanya shughuli zote tunazofanya mchana mf. Kuwasha radio na kubadili station, kufagia, kufungua fridge nk.
Tulihangaika ikawa kila siku mziki unanza saa mbili usiku, tukawa hatulali.. Akaja mshikaji wake broo akamwambia tukae nje usiku kwenye pembe ya nyumba tutawaona wanaotusumbua.
Tukajipanga tukaenda kukaa, baada kama ya dakika arobani alipita mtu wa kwana anakimbia kinyume nyume mwendo wake sijapata kuona, baada ya muda akarudi akiwa na mwenzake wakiwa na mwendo wa kawaida tukawatambua kumbe ni baba mwenye nyumba na jirani yetu.
Jambo la kutisha waliamua kutuadhibu baada ya kutugundua tumewaona.. Hivyo tulipigwa gazi karibia masaa matatu hamna kusogea wala kuongea hata kujikuna. Wao wakaendelea na mambo yao.