Wilderness Voice
JF-Expert Member
- May 19, 2016
- 921
- 1,649
Sijawahi ona kiumbe Cha ajabu wala kuhisi sijui minyato ya kichawi au uchawi hapana kabisa!.. hii inanifanya hata niwe mgumu kuuamini huo ulimwengu! Japo nimekuwa muda mwengine mzururaji sometimes maeneo hatarishi ambayo wengine huogopa lkn binafsi hakuna la ajabu nililoliona!.. yanayonitokea ni matukio ya kawaida kabisa ila Kuna baadhi yanaleta utata ila sio utata wenye kunifanya niamini kuwa kuna walakini!!
Mfano kuna mahali palikuwa panasemekana kuwa huwa kuna sijui majini ama mizimu ila kuna miti ya miembe na mapera,siku moja nipo mi najamaa fulani ktk pitapita tukakuta mti wa mpera tukaanza kuchuma lkn sio kwa kupanda punde tukiwa tunachuma aliongezeka kijana mwengine Sasa utata baada ya kuondoka Yule kijana ndo tukaanza kujiuliza alitokea wapi!!
Maana kipindi anakuja hatukumuona! Si tulishangaa tu tupo watatu nae anachuma mapera lkn chengine alichotutatanisha ni ni maswali yake juu ya ule mpera na hata sikumbuki Kama alichuma hata!!
Swala la kutokumuona alivyokuja nililivunjilia mbali maana kibarabara tulikuwa bize kutafuta mapera wahuni😂
Na apotelea pote huko tukio lake halina mantiki..
Sijui nini kitakuja nifanya niamini haya mambo ila mi nachohisi kitu usipokiweka bayana nawe kukuzingua au kujionyesha mbele yako kina nafasi ndogo Sana ya kujionyesha..
Na mnaona hayo mambo na muone siku nikishuhudia huo ulozi kwa sababu ya kimantiki iliyoshiba nitakuja kusimulia humu.
Kuna binadamu wamepewa uwezo wa kung'amua vitu na kuna wengine katika ulimwengu wa kiroho ni vipofu wasioona kitu chochote. Macho yao yamefungwa. Sikumbuki vizuri ila katika biblia kuna mtume mmoja walizingirwa na maadui lakini hakuonesha wasi wasi wowote. msaidizi wake akamwambia sasa tunauwawa. Yeye akajibu ondoa wasiwasi tunaulinzi yule akashangaa ulinzi u wapi.
Ndipo yule mtume akamfungua macho yule mtumishi akaona jeshi kubwa la malaika limewazunguka. Ndipo wasiwasi ukaondoka. wanaojua Biblia watasema ni nani. Nilitaka tu kukwambia haya mambo ni ktk roho. uwezi yaona mpaka uwe katika ulimwengu wa rohoni. Majini, Malaika uwezi waona kwa macho ya nyama. Kuna watu wanazaliwa wananguvu maalum za kiroho. Haya mambo yapo!