Hilo tukio lako la kukuta watu saa tisa wapo darasani wanasoma liliwahi kunikuta hata mimi, ila mimi haikuwa darasani....ilikuwa mida hiyo hiyo mibovu, nikiwa kikosi fulani huko Nachingwea mwaka 2013. Siku hiyo nipo zamu, kiongozi wa eneo nililopaswa kulifanyia ungalizi siku hiyo. Na niliwajibika kwa sehemu mbili zote zikiwa karibu: sehemu A, na ambapo zamu ilinisoma sehebu B, lakini nikiangalia sehemu zote mbili.
Jioni katika kushusha bendera nikawapanga watu wa kituo A ndo washushe, halafu sisi wa kituo B tutapandisha asubuhi. Na mimi nilikuwa wa mwisho kulinda siku ile, ina maana baada ya kuzurura zurura mpaka saa 6 nkaamua nilale ili saa kumi nishike zamu yangu. Sasa ilipofika saa kumi kasoro nikaamka, pako salama nikawapumzisha waliopo nasi wa zamu ya saa kumi tukaamka... Nikamwambia mwenzangu hebu baki hapo mi nifike kituo A nikacheki nako kuko poa, sasa nikiwa naenda kituo A nkapita sehemu ambapo kuna milingoti ya bendera... wacha kabisa, nikakuta watu wawili wafupi mno kwa kipimo cha kawaida wananifika kiunoni, wapo kwenye milingoti ya bendera wanashusha bendera, wamevaa kombati, wana silaha kama kawaida, na nyuma yao kuna watu nane wapo kwenye paredi ya kushusha bendera! Nikatulia nikawacheki, baadaye wakamaliza, wakageuka nyuma, wakaungana na paredi hao wakasepa kuelekea kwenye misufi... na wakapotea.
Nilishangaa sana maana sisi bendera tukishusha huipeleka kituo A, wao wakapeleka kwenye misufi na wakapotelea huko. Siku za baadae nilipowauliza wakongwe wakasema hiyo ni kawaida, yaani sisi tunaposhusha hao hupandisha, na sisi tunapopandisha wao huwa washashushandio , ila shukuru hawajakuona... wakasema hivyo vituo unaweza ukashangaa hata usiku magari yanawashwa hafu humuoni anayeyawasha, mabovu hutengenezwa na usimuone anayeyatengeneza pia... nikastaajabu sana!!!