Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Mimi kuna kisa kilinitokea nilikua kama darasa la 5. Wazee wameenda kulala na mimi nilikua na chumba changu tofauti na madogo zangu nikaenda zangu kulala,nakumbuka mlango nilifunga vizur kabisa dogo nikajipigia zangu mbonji usingizi mwororo! Asubuh kuamka LAHULA LAKWATA pembeni ya kitanda kwa chini kuna kimba moja la kinyesi,kuangalia mlango umefungwa vilevile,na udogo wangu nikaanza kutetemeka nikaenda kuwaamsha wazee,mshua kuja pale akacheka akasema hamna lolote huyu kashindwa akayamwagia majivu picha likaisha hivyo.
lakin ile nyumba ikifika mida ya saa mbili usiku kuna vitu vinatembea juu ya bati afu kama vinateleza af unasikia kishindo kama vimedondoka mkienda mliposikia kishindo hamna kitu.
Nakumbuka nilishawah kumwamsha dogo saa 9 usiku nikidhan kumepambazuka twende shule tukawah namba,fresh tumejiandaa tukaenda kuwaaga wazee tukaanza safari,hapa ndo hua naamin mungu yupo maana baada ya kufika mtaani maana inabdi tukatze mtaani afu tuvuke eneo la makaburi ndo tufike shule,ila ule utulivu wa mtaani nikamwambia dogo turudi home hii sio kawaida kama tukichelewa leo namba basi,tukarudi zetu home na kuingia vyumbani kwetu bila kuwataarifu wazee,kumbe huku room kwa wazee bi mkubwa akashtuka akasema hawa wametuaga wanaenda shule kwan saa ngapi?kuangalia muda ni saa 9 na dakika kadhaa ebana ee dingi alikurupuka na pensi flan ya kulalia kifua wazi akaelekea shule kutufata,kufika pale anaita mlinzi haonekani ikabdi arudi huku anasema kesho nasafiri naenda nyumbani naona watu hatuheshimiani,bi mkubwa akasema hebu tuwaangalie vyumbani mwao,kuja kuangalia bi mkubwa akasema SI HAWA HAPA!!
Wale mabibi jirani ***** zao lakin walikuja kuuelewa mziki
Mzee wako sio mtu mzuri [emoji23]Hataki masihara
 
Haya mambo kama huna macho ya kuyaona, usiombee maana yanatisha sana. Inahitaji moyo....

Sent using Jamii Forums mobile app
kwakweli[emoji23]
Hilo tukio lako la kukuta watu saa tisa wapo darasani wanasoma liliwahi kunikuta hata mimi, ila mimi haikuwa darasani....ilikuwa mida hiyo hiyo mibovu, nikiwa kikosi fulani huko Nachingwea mwaka 2013. Siku hiyo nipo zamu, kiongozi wa eneo nililopaswa kulifanyia ungalizi siku hiyo. Na niliwajibika kwa sehemu mbili zote zikiwa karibu: sehemu A, na ambapo zamu ilinisoma sehebu B, lakini nikiangalia sehemu zote mbili.

Jioni katika kushusha bendera nikawapanga watu wa kituo A ndo washushe, halafu sisi wa kituo B tutapandisha asubuhi. Na mimi nilikuwa wa mwisho kulinda siku ile, ina maana baada ya kuzurura zurura mpaka saa 6 nkaamua nilale ili saa kumi nishike zamu yangu. Sasa ilipofika saa kumi kasoro nikaamka, pako salama nikawapumzisha waliopo nasi wa zamu ya saa kumi tukaamka... Nikamwambia mwenzangu hebu baki hapo mi nifike kituo A nikacheki nako kuko poa, sasa nikiwa naenda kituo A nkapita sehemu ambapo kuna milingoti ya bendera... wacha kabisa, nikakuta watu wawili wafupi mno kwa kipimo cha kawaida wananifika kiunoni, wapo kwenye milingoti ya bendera wanashusha bendera, wamevaa kombati, wana silaha kama kawaida, na nyuma yao kuna watu nane wapo kwenye paredi ya kushusha bendera! Nikatulia nikawacheki, baadaye wakamaliza, wakageuka nyuma, wakaungana na paredi hao wakasepa kuelekea kwenye misufi... na wakapotea.

Nilishangaa sana maana sisi bendera tukishusha huipeleka kituo A, wao wakapeleka kwenye misufi na wakapotelea huko. Siku za baadae nilipowauliza wakongwe wakasema hiyo ni kawaida, yaani sisi tunaposhusha hao hupandisha, na sisi tunapopandisha wao huwa washashushandio , ila shukuru hawajakuona... wakasema hivyo vituo unaweza ukashangaa hata usiku magari yanawashwa hafu humuoni anayeyawasha, mabovu hutengenezwa na usimuone anayeyatengeneza pia... nikastaajabu sana!!!
wangekuona ingekuaje
 
Umenikumbusha mauza uza ya 835kj mwaka 2008
 
Nakumbuka nilipokuwa na miaka kati ya 5 au 6,tulienda kijijini na wazazi wangu kuwatembelea Bibi na babu,kwavile Mimi ndo nilikuwa mjukuu wa kwanza kwa babu alikuwa anapenda kutoka na Mimi kila akiwa na mizunguko yake pale kijijini,siku moja tumeenda kwa rafiki yake mmoja alitukaribisha kwenye nyumba yake ilikuwa ni zile nyumba za nyasi za mviringo,Basi akatuacha ndan mm na babu Kuna kitu Kama alifuata nje,zile akili za utoto kuangalia juu ya ile nyumba nikaona watu wamekaa wanatuangalia huku wakiwa wamejipaka kama unga usoni,nilivyomstua babu ili na yeye aangalie juu sikuwaona tena wale watu pale juu mpka tunaondka na babu kwa yule rafiki yake.
Ukiona misukile inapakwa unga usoni ujie ni movie za bongo movies,, kihalisia misukule haipakwi unga usoni, inakuwa na baadhi ya rangi za madawa inayopakwa na ni kiasi tu, ni michorochoro kadhaa mara nyingi ni myeusi au kijivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2012 nilienda wilaya ya rungwe kukusanya data, sasa katika harakati za kuzunguka nikafika kijiji fulani kinaitwa malalika sijui kama nimeandika sahihi, kipo 15km kutoka kiwila na 7km kutoka hospitali ya igogwe, nyumba niliyofikia ilijengwa mlimani hivi katikati ya shamba la chai, ilikua na vyumba viwili vya kulala nikapewa chumba kimoja kingine alilala mhudumu wa lile shamba, nyumba ilijengwa kwa tofali za tope ila ndani wamebandika magazeti chumba kizima ndio plasta na juu wameweka shuka ndio ceiling board, usiku nilipokua nimelala nilianza kusikia kishindo kikubwa juu ya bati kama mtu anatembea kutoka upande mmoja wa nyumba kwenda mwingine, mwanzoni nilihisi kama ndoto ila niliposhtuka usingizini niloendelea kusikia kama mtu anatembea juu ya bati, ile hali iliendelea kwa muda mrefu, niliinua kichwa kuchungulia dilishani nje sikuona kitu palikua na ukungu mkali ikabidi nirudi kujifubika branket langu huku moyo ukienda mbio sana nikajua leo kazi ninayo, baada ya muda ile sauti iliacha ghafla kikaja kitu kama kimbunga mle chumbani upepo mkali ukabandua yale magazeti yote ukutani mavumbi ya tofali yakawa yananiangukia kitandi mimi nimejifunika hadi kichwa nimekaza miguu shuka lisitoke, ule upepo ulipoisha nikaita alexxxx kwa sauti kubwa ambaye ni yule mwenyej wangu aliyelala chumba kingine alipoitika sikujua nimefikaje chumbani kwake, maana niliruka kitandani nikapiga teke kile kimlango cha chumbani nikavamia na mlango wake hadi chumbani kwake, nikamuuliza kama amesikia ivo vitu licha ya kuwa na baridi ila jasho lilikua linanitoka, jamaa alichonijibu ni tulia acha papara. Nikawa nimekaa kwenye kistuli pembeni ya kitanda chake huku tumewasha kibatali, jamaa akaniambia pametulia rudi ukalale nikakataa nikamwambia silali nakaa hapa hapa wewe lala, nilikaa pale hadi alfajiri nilipoona nje pameanza kupambazuka nikaenda mle chumbani palikua hovyo sana vumbi kila mahali nikachukua kibegi changu nikamwambia yule jamaa mimi nasepa badae njoo kiwira tuongee, nikatoka nikadandia magari yanayobeba ndizi na maparachichi kwenda mnandani, saa nne yule jamaa akikuja kiwira nikampa elfu ishirini nikamwambia ikitokea siku mabosi wangu wakija kijijini kuuliza kama nilifika awambie kuwa nilikuja na nikafanya kazi ila kiukweli nilikimbia huwa sisahau lilie tukio, kuna lingine nililiona wilaya ya mbogwe mkoa wa simiyu, ni vijijini huko ndani kabisa hata barabara hakuna mnapaki gari mnatembea 4km huko tulizinguana na mwenyekiti wa kijiji akatutumia kundi la fisi tukakimbilia kwenye nyumba ya mwanakijiji tukapiga simu kwa mtendaji akaja kutuokoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
simiyu kutumiwa fisi ni jambo dogo sana. Niliwahi kusoma shule flani kule enzi hizo ilikua shinyanga bado aisee kuna dogo aliliwa na fisi yan katika kufatilia ndo tukaambiwa ni fisi wa mazingaombwe aisee simiyu sio poa..
 
Mbozi vijijini. Zamani ilikuwa mkoa wa mbeya siku hizi Songwe. Wako mpakani na mkoa wa Rukwa a.k.a Sumbawanga
Mlikua na ujasiri
kuona viwili wili na bado mnaendelea kutembea bila woga
 
Mimi kuna kisa kilinitokea nilikua kama darasa la 5. Wazee wameenda kulala na mimi nilikua na chumba changu tofauti na madogo zangu nikaenda zangu kulala,nakumbuka mlango nilifunga vizur kabisa dogo nikajipigia zangu mbonji usingizi mwororo! Asubuh kuamka LAHULA LAKWATA pembeni ya kitanda kwa chini kuna kimba moja la kinyesi,kuangalia mlango umefungwa vilevile,na udogo wangu nikaanza kutetemeka nikaenda kuwaamsha wazee,mshua kuja pale akacheka akasema hamna lolote huyu kashindwa akayamwagia majivu picha likaisha hivyo.
lakin ile nyumba ikifika mida ya saa mbili usiku kuna vitu vinatembea juu ya bati afu kama vinateleza af unasikia kishindo kama vimedondoka mkienda mliposikia kishindo hamna kitu.
Nakumbuka nilishawah kumwamsha dogo saa 9 usiku nikidhan kumepambazuka twende shule tukawah namba,fresh tumejiandaa tukaenda kuwaaga wazee tukaanza safari,hapa ndo hua naamin mungu yupo maana baada ya kufika mtaani maana inabdi tukatze mtaani afu tuvuke eneo la makaburi ndo tufike shule,ila ule utulivu wa mtaani nikamwambia dogo turudi home hii sio kawaida kama tukichelewa leo namba basi,tukarudi zetu home na kuingia vyumbani kwetu bila kuwataarifu wazee,kumbe huku room kwa wazee bi mkubwa akashtuka akasema hawa wametuaga wanaenda shule kwan saa ngapi?kuangalia muda ni saa 9 na dakika kadhaa ebana ee dingi alikurupuka na pensi flan ya kulalia kifua wazi akaelekea shule kutufata,kufika pale anaita mlinzi haonekani ikabdi arudi huku anasema kesho nasafiri naenda nyumbani naona watu hatuheshimiani,bi mkubwa akasema hebu tuwaangalie vyumbani mwao,kuja kuangalia bi mkubwa akasema SI HAWA HAPA!!
Wale mabibi jirani ***** zao lakin walikuja kuuelewa mziki
Mziki gan kaka hebu endelea kutupa vitu
 
Nilmfata tajiri mmoja ana magari kibao(crane) ya kubebea mizigo kwenye gereji yake aniuzie mbuzi, maana mbuzi wake ni mbegu kubwa na wanazaa mapacha.
Akaniambia huna hela ya kununua hawa mbuzi nkamwambia nitajie bei ngapi maana najua hawa nkiwapeleka shamba watazaliana sana akagoma.

Siku nyingine nkamwambia niuzie hivi vipacha 50 kila kimoja, sasa kwa sababu nina nia ya kununua, mlinzi wake akaniambia hawa mbuzi hawezi kukuuzia kila anunuapo gari huwachinja na damu yake huzungishiwa kwenye hyo gari, nkajua kumbe mbuzi wa dawa.

Tajiri mwingine alikuwa anafuga bata bukini,akikuona unafanya same business kwenye eneo lake anakupa zawadi ya nyama ya bata ila akiwa anakupa lazima akupe hug(kumbato) miezi 6 mingi unakuwa mufilisi.

Sasa kuna jamaa mmoja alikuwa mshirikina sana ( dalali wa vyumba na nyumba) akapita karibu na wale bata, mara bata wakalia mlio wa sauti kuwa wameona mgeni au kitu kipya, kumbe wamelamba hirizi zake zote alizopewa kwa mganga, akajiona mwepesi, akamfata mmiliki wa bata akasema bata wako wamekula vitu vyangu sasa wengine hatujui lugha za kichawi, mmiliki anamuuliza dalali,

Bata wamefungiwa ndani ya fensi nimepga na uzio na ndani hawajatoka wamekulaje vitu vyako, toka siku hyo dalali hapti kwa mfuga bata, anasema wale c bata wa kawaida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilishapandishwa mamba na fisi sana kule kwenye utajiri wa ndago Iringa,Sasa hv aaaaah nina mapene mob,baadae ili nisitoe kafara za kumaliza watu wangu wa karibu,nikapata uchawi mwingine balaa ila kila siku moja j2 nakufa kabisa na siku moja sifi ila naoza tu kudadadeki,wale funza ndio mifedha yenyewe,kesho kwenye mishe zangu utashangaa tu unatokea mchongo wa kupita milioni 500,balaa sana inabidi uwe bandidu,balaa zit

Ila mwanangu huyo alikuja kufa kifo cha hatari mnoooo

rip to ze fallen soja tindwago
 
Back
Top Bottom