Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Fanya mpango wa namba hizo mzee

Mngoni%
 
Mkuu nyamatongo hiki kisa kinasisimua sana.

Labda niulize tu, baada ya hilo tukio uhusiano wako na huyo jamaa ulikuaje?

Pili, huyu jamaa yako alikua mwanausalama in any way? Kama sio..kama hutojali unaweza sema alikua akijishughulisha na nini?

Pia, huyo mzee mliyemuamsha usiku; baada ya hapo uliwahi kuonana nae tena? If so, mliongea nini?

Mwisho, unadhani wazazi wa huyu jamaa yako walijua hilo tukio in any way?

Nisamehe kwa maswali mengi....ila hili tukio linafikirisha sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
99
Boya Sana wewe uliogopa nini..?
Ungechukua toto hilo nyie kila kitu mnaonaga negative tu kwanini usiseme bwana kakuonyesha kimwana wa kuoa!
Mkuu Kama unaikumbuka namba yake nitumie halafu ntakupa mrejesho nimemfanya nini!
😂😂😂 Ni miaka zaidi ya 11 Sasa siwez kukumbuka namba
 
Mabaharia katika ubora wao 😂😂 Ila wanawake wnapatikana tu kwa njia ambazo hazina ukakasi
 
Hahahaaa Mimi ilikuwa siyo kukimbia,
nilikuwa nakatiza uwanjani mida ya saa sits hivi,
Ila nikitembea nasikia kabisa maisha yanaendelea kama mchana,napishana na watu na wanaongea,
nilikuja kushtuka alfajiri natembea palepale uwanjan
Kweli hii Dunia Ina Mambo. Viumbe Vyote eti vya Mungu, Kweli?
 
Duhh hapo kimbembe kinakuja ukijikwaa ukianguka.. Aisee unaweza kuzimia kwa Plesha😀
 
Ni pale wakuu wa nchi waliposema wananchi Wasiogope Gonjwa la Dunia, linalo Ua watu/wataalamu kwa Maelfu, eti mjitibu kwa kutumia Nyungu! ili hali wanakufa! lkn watu waka amini wasio wataalamu.

Hili linatisha, sintosahau aisee!!!!!
 
mkuu nakubaliana na ww, ninapokaa kuna mtoto wa mzee mwenye nyumba ni mwanamke wa makamo kuna nyepesi kua na yeye ni fundi, siku moja asubuh anamwambia mke wng eti usiku ameota pale kwangu kuna sherehe yuko yeye na mwanangu wanacheza mziki,wife alivyonambia vile nilimind sana maana kuna kitu nilihisi ila nikamwambia wife hamna tatzo kama kuna lolote baya litawarudia,

kesho yake asubuh mwanae wa mwisho kaenda kucheza kavunjika mkono mpaka hospital mpaka kufungwa POP, nikamwambia wife si alitaka sherehe bas hiyo hapo aruke nayo
 
Mshawishi aunt yako siku moja mkamtembelee hapo dukani...
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2012 nilienda wilaya ya rungwe kukusanya data, sasa katika harakati za kuzunguka nikafika kijiji fulani kinaitwa malalika sijui kama nimeandika sahihi, kipo 15km kutoka kiwila na 7km kutoka hospitali ya igogwe, nyumba niliyofikia ilijengwa mlimani hivi katikati ya shamba la chai, ilikua na vyumba viwili vya kulala nikapewa chumba kimoja kingine alilala mhudumu wa lile shamba, nyumba ilijengwa kwa tofali za tope ila ndani wamebandika magazeti chumba kizima ndio plasta na juu wameweka shuka ndio ceiling board, usiku nilipokua nimelala nilianza kusikia kishindo kikubwa juu ya bati kama mtu anatembea kutoka upande mmoja wa nyumba kwenda mwingine, mwanzoni nilihisi kama ndoto ila niliposhtuka usingizini niloendelea kusikia kama mtu anatembea juu ya bati, ile hali iliendelea kwa muda mrefu, niliinua kichwa kuchungulia dilishani nje sikuona kitu palikua na ukungu mkali ikabidi nirudi kujifubika branket langu huku moyo ukienda mbio sana nikajua leo kazi ninayo,

baada ya muda ile sauti iliacha ghafla kikaja kitu kama kimbunga mle chumbani upepo mkali ukabandua yale magazeti yote ukutani mavumbi ya tofali yakawa yananiangukia kitandi mimi nimejifunika hadi kichwa nimekaza miguu shuka lisitoke, ule upepo ulipoisha nikaita alexxxx kwa sauti kubwa ambaye ni yule mwenyej wangu aliyelala chumba kingine alipoitika sikujua nimefikaje chumbani kwake, maana niliruka kitandani nikapiga teke kile kimlango cha chumbani nikavamia na mlango wake hadi chumbani kwake, nikamuuliza kama amesikia ivo vitu licha ya kuwa na baridi ila jasho lilikua linanitoka,

jamaa alichonijibu ni tulia acha papara. Nikawa nimekaa kwenye kistuli pembeni ya kitanda chake huku tumewasha kibatali, jamaa akaniambia pametulia rudi ukalale nikakataa nikamwambia silali nakaa hapa hapa wewe lala, nilikaa pale hadi alfajiri nilipoona nje pameanza kupambazuka nikaenda mle chumbani palikua hovyo sana vumbi kila mahali nikachukua kibegi changu nikamwambia yule jamaa mimi nasepa badae njoo kiwira tuongee, nikatoka nikadandia magari yanayobeba ndizi na maparachichi kwenda mnandani, saa nne yule jamaa akikuja kiwira nikampa elfu ishirini nikamwambia ikitokea siku mabosi wangu wakija kijijini kuuliza kama nilifika awambie kuwa nilikuja na nikafanya kazi ila kiukweli nilikimbia huwa sisahau lilie tukio

kuna lingine nililiona wilaya ya mbogwe mkoa wa simiyu, ni vijijini huko ndani kabisa hata barabara hakuna mnapaki gari mnatembea 4km huko tulizinguana na mwenyekiti wa kijiji akatutumia kundi la fisi tukakimbilia kwenye nyumba ya mwanakijiji tukapiga simu kwa mtendaji akaja kutuokoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ilitokea miaka ya mwanzoni ya 80. Huko kamsamba kando ya mto Momba (ambalo ndo jina ya wilaya ya Momba). Hicho kijiji na vijiji jirani vilikuwa na matukio acha. Watu walikuwa wanga ile mbaya.

1. Tukio la kwanza baba alikuwa Mwalimu Mkuu wa shule ile. Sasa alikuwa na kawaida ya kuhesabisha namba saa Tisa. Siku moja wanafunzi wakaja kugonga kengele ya namba saa tisa kasoro hivi. Wakakuta kuna kundi la watu wapo shuleni wamejaa kwenye madarasa yote. Wengine wanafundisha, wengine wana pewa adhabu kama shule kabisa mchana. Wale wanafunzi wakaja wakagonga nyumbani ambapo baba akatoka na mdogo wake kwenda kuhakikisha. Baba akawaambia wagonge kengele, vilitoka vidudu mtu urefu havizidi kama mita moja na nusu. Waliwakimbiza mbaya. Bahati nzuri nyumba ilikuwa karibu na shule so wakawahi kuingia ndani. Sauti ikasikika ikisema ole wenu mtusumbue usiku tena. Ile ndo ilikuwa mwisho, kuanzia kesho yake wanafunzi wakaanza kuja kukiwa kumekucha kabisa.

2. Tukio la pili ilikuwa miaka hiyohiyo mida ya saa 12 jioni tukiwa tunaenda kuteka maji kwenye huo mto. Tukaona vyungu vingiii, vizuri vimepangwa pembeni ya mto. Mama akasema dah, vyungu vizuri sijui muuzaji yupo wapi ili aniuzie. Akaanza kuita kama kuna mtu karibu. Kwa mshangao mkuu vyungu vileserereka machoni petu na kukimbilia mtu... Ilikuwa kama nyoka anavyoteleza... Aisee, tulitoka mbio tukajikuta tupo ndani bila tumefikaje.

Kule Kamsamba kulikuwa na ushirikina na matukio ya kutisha acha kabisa. Sijui sasa hali ikoje. Kukutana na mtu anatembea upande upande badala ya kwenda mbele anakuwa anaenda kulia au kushoto ilikuwa kawaida. Tukiuliza wakubwa wanasema hao ni misukule. Mara nyingine tumeenda porini tukakuta kiwiliwili, damu bado mbichi, halafu masela hatuogopi tunaendelea na mishe yetu tu. Siku moja tukakutana na hao wajuba wana visu na ndoo, aisee tulikula nao ligi kwa masaa kama mawili hivi bila kutukuta.

Habari za kuchunana ngozi kule ndo ilikuwa chimbuko. Ilikuwa kama serikali haipo. Maana maiti inaokotwa na inazikwa tu. Vyombo vya habari ndo vikaja saidia.
 
nmecheka kama mazuri ila dunia jamani
 
Momba ndio wapi mkuu
 
Mimi kuna kisa kilinitokea nilikua kama darasa la 5. Wazee wameenda kulala na mimi nilikua na chumba changu tofauti na madogo zangu nikaenda zangu kulala,nakumbuka mlango nilifunga vizur kabisa dogo nikajipigia zangu mbonji usingizi mwororo! Asubuh kuamka LAHULA LAKWATA pembeni ya kitanda kwa chini kuna kimba moja la kinyesi,kuangalia mlango umefungwa vilevile,na udogo wangu nikaanza kutetemeka nikaenda kuwaamsha wazee,mshua kuja pale akacheka akasema hamna lolote huyu kashindwa akayamwagia majivu picha likaisha hivyo.

lakin ile nyumba ikifika mida ya saa mbili usiku kuna vitu vinatembea juu ya bati afu kama vinateleza af unasikia kishindo kama vimedondoka mkienda mliposikia kishindo hamna kitu.
Nakumbuka nilishawah kumwamsha dogo saa 9 usiku nikidhan kumepambazuka twende shule tukawah namba,fresh tumejiandaa tukaenda kuwaaga wazee tukaanza safari,hapa ndo hua naamin mungu yupo maana baada ya kufika mtaani maana inabdi tukatze mtaani afu tuvuke eneo la makaburi ndo tufike shule,ila ule utulivu wa mtaani nikamwambia dogo turudi home hii sio kawaida kama tukichelewa leo namba basi,tukarudi zetu home na kuingia vyumbani kwetu bila kuwataarifu wazee,kumbe huku room kwa wazee bi mkubwa akashtuka akasema hawa wametuaga wanaenda shule kwan saa ngapi?

kuangalia muda ni saa 9 na dakika kadhaa ebana ee dingi alikurupuka na pensi flan ya kulalia kifua wazi akaelekea shule kutufata,kufika pale anaita mlinzi haonekani ikabdi arudi huku anasema kesho nasafiri naenda nyumbani naona watu hatuheshimiani,bi mkubwa akasema hebu tuwaangalie vyumbani mwao,kuja kuangalia bi mkubwa akasema SI HAWA HAPA!

Wale mabibi jirani ***** zao lakin walikuja kuuelewa mziki
 
Tukio LINGINE LILINITOKEA MIAKA kumi iliyopita Nakumbuka yalikua maafali ya WASABATO...
NILIPEWA KADI ZAIDI YA MBILI KWA KUA MWENYEKITI ALIKUA NI RAFIKI ANGU....
STORY ILIKUA IVI....
ILIKUA SAA SITA KAMA NA DAKIKA 50 MCHANA..
NIKAPATA WAZO NIKAMPITIE RAFIK ANGU THABIT
RAFIKI ANGU THABIT ALIKUA ANAKAA JIRANI NA SHULE YA MSINGI....
ILI NIFIKE KWAO ILINIBIDI NIKATIZE KATIKATI YA UWANJA WA MPIRA....
ILE
ILE NAKATIZA KANDO KANDO YA UWANJA KUNA MTI MMOJA MKUBWA SANAA
MAJIRA HAYO YA MCHANA HAKUKUA NA MTU YEYOTE BARABARANI
NILIFIKA MITA CHACHE KARIBU NA MTI MKUBWA HAPO UWANJANI...
GAFLA
NIKAONA MDADA WA KIISLAMU ALIE VALIA HIJABU NYEUSI....
NILIPO
TUPA JICHO KWA MARA YA PILI TULIKUTANA USO KWA USO....
BINTI ALIKUA NA UZURI USIO WA KAWAIDA....
SURA ILIYO MELEMETA AKIWA AMESHIKILIA ULE MTI MKUBWA HUKU AKINITAZAMA
MPK NIKAOGOPA...
NIKA ANGALIA PEMBENI NIKARUDIA KUMUANGALIA TENA YULE DADA ALIENDELEA KUNITAZAMA MIMI NILIANGALIA MBELE SIKUGEUKA TENA NYUMA...
YULE DADA ALIKUA AMEVALIA HIJABU NYEUSI NDEFU MPKA CHINI MIGUU HAIONEKANI WALA MIKONO....
ALIKUA MWARABU SI MWARABU SHOMBE SIO SHOMBE
HAKUA MWEUPE WALA MWEUSI
UZURI WAKE ULIKUA KAMA WAHABESHI TOKA ETHIOPIA

KILICHO NIOKOA NI KIMOJA TUU HUWA SINAGA TABIA ZA KUSHOBOKEA WADADA....
TULI TAZAMANA ZAIDI YA MARA 3 NA YULE MDADA NA SIKUMSEMESHA KITU...
ALINITAZAMA SANA...ILA NILIJIKAZA KIUME NIKAKATIZA KAMA SIJAONA KITU....
NILIPO FIKA KWAO NA RAFIK ANGU MITA MIA 200 TOKA ENEO LA TUKIO FASTA NIKAMWAMBIA
TUKARUDI UWANJANI HATUKUKUTA MTU...
NILIOGOPA SANA TULIENDA KWENY SHEREHE YA WASABATO NILIPO MALIZA KULA TUMBO LILIANZA KUUMA NA NILI HARISHA SANAA
NILIOGOPA SANA TANGU SIKU IYO NILI ANZA KULALA NA BIBLIA KITANDANI.....
 
Wilaya ya mbogwe simiyu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo tukio lako la kukuta watu saa tisa wapo darasani wanasoma liliwahi kunikuta hata mimi, ila mimi haikuwa darasani....ilikuwa mida hiyo hiyo mibovu, nikiwa kikosi fulani huko Nachingwea mwaka 2013. Siku hiyo nipo zamu, kiongozi wa eneo nililopaswa kulifanyia ungalizi siku hiyo. Na niliwajibika kwa sehemu mbili zote zikiwa karibu: sehemu A, na ambapo zamu ilinisoma sehebu B, lakini nikiangalia sehemu zote mbili.

Jioni katika kushusha bendera nikawapanga watu wa kituo A ndo washushe, halafu sisi wa kituo B tutapandisha asubuhi. Na mimi nilikuwa wa mwisho kulinda siku ile, ina maana baada ya kuzurura zurura mpaka saa 6 nkaamua nilale ili saa kumi nishike zamu yangu. Sasa ilipofika saa kumi kasoro nikaamka, pako salama nikawapumzisha waliopo nasi wa zamu ya saa kumi tukaamka... Nikamwambia mwenzangu hebu baki hapo mi nifike kituo A nikacheki nako kuko poa, sasa nikiwa naenda kituo A nkapita sehemu ambapo kuna milingoti ya bendera... wacha kabisa, nikakuta watu wawili wafupi mno kwa kipimo cha kawaida wananifika kiunoni, wapo kwenye milingoti ya bendera wanashusha bendera, wamevaa kombati, wana silaha kama kawaida, na nyuma yao kuna watu nane wapo kwenye paredi ya kushusha bendera! Nikatulia nikawacheki, baadaye wakamaliza, wakageuka nyuma, wakaungana na paredi hao wakasepa kuelekea kwenye misufi... na wakapotea.

Nilishangaa sana maana sisi bendera tukishusha huipeleka kituo A, wao wakapeleka kwenye misufi na wakapotelea huko. Siku za baadae nilipowauliza wakongwe wakasema hiyo ni kawaida, yaani sisi tunaposhusha hao hupandisha, na sisi tunapopandisha wao huwa washashushandio , ila shukuru hawajakuona... wakasema hivyo vituo unaweza ukashangaa hata usiku magari yanawashwa hafu humuoni anayeyawasha, mabovu hutengenezwa na usimuone anayeyatengeneza pia... nikastaajabu sana!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…