Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Nilipomaliza elimu ya msingi nikaenda pre form one shule fulani ya English medium ipo Njombe. Nilikuwa bweni na nilisoma hapo kwa miezi mitatu. Bweni nililokuwa nalala lilikuwa limepakana na makaburi kwa kutenganishwa kwa uzio wa mabanzi.

Mbele ya bweni kulikuwa na uwanja ambao paliwekwa bembea nyingi kwa ajili ya watoto kucheza nyakati mbalimbali. Siku moja nikiwa na mwenzangu tulitoka usiku wenzetu wakiwa wamelala tukaenda chooni. Wakati tunarudi zile bembea zote zilikuwa zimetulia, ghafla bembea mbili zikaanza kucheza Kama vile Kuna mtu anabembea.

Zilifanya hivyo kwa muda mrefu huku bembea nyingine Kama kumi na tano hivi zikiwa zimetulia. Ilikuwa ajabu Sana! Tulikimbia tukaenda kulala asubuhi tukawasimulia wenzetu, kumbe Kuna wengine Kama watatu hivi nao wamewahi kushuhudia tukio Hilo

Sent using Jamii Forums mobile app
 


😄😄😄wachawi sometimes wana comedy sana.
 
Hii ni kawaida sana hususani unavyokuwa nondo(guard). Ni matukio ya kawaida kutokea, kama huna moyo waweza "vunja umbo."

"Ungejua alacho Kuku, usingempa mgeni."
 
Dah kweli mkuu wewe si muoga, hukuwahi kujenga picha kichwani kwamba labda kageuza kichwa anakusubiria ukatize?
 
Mike omba uhamisho huko hapafai. KJ kina extra company haha.
 
Huyo mwanamke ni jini mkuu wala usisumbuke kutaka kujua anaishi wapi maanisha majini yote makazi yao ni kwenye mapango, kwenye maziwa na bahari.

Chamsingi tafuta dawa ya kumfukuza kabisa asitokee wala kukuharibia maisha yako. Kama ni mkristo kamwone mchungaji akufanyie maombi na kama ni muislamu nenda kwa shekhe akakufanyie kisomo.
 
Yah vituo hivyo ni vituo vigumu, ila ongeza GO na vituo vya vyanzo vya maji, kama utakuwa camp ya ndichi huko. Ni balaa

"Ungejua alacho Kuku, usingempa mgeni."
GO ndio sehemu ya combania isiyoonekana inashinda na kufanya yao kama ile parade ya kushusha bendera uliyoiona. Haha sipati picha hivyo vibwengo vilibeba vipi SAR maana ni ndefu kuliko vyenyewe😂😂
Pia siwapatii picha mpiga buriji na paredi kamanda alivyokuwa akiamrisha, yaani kama nawaona vile😂😂😂
 
Miaka ya nyuma baada ya kumtibu ndugu yetu mmoja ikashindikana kupona ndipo mganga aliposema inabidi tuwaite wachawi waliomroga ili watuonyeshe dawa mana kwangu imeshindikana tukaa kama wanafamilia tukakubaliana na maneno ya mganga siku ya siku imefika tukabeba mgonjwa mpk makabulini na mganga.

nakumbuka ilikuwa saa 8 usiku tumefika pale mganga akaanza mambo yake mara akachukua filimbi akapiga mara 3 tukaanza kuona mauza mauza mganga akatwambia mnapaswa msiogope hiyo dawa niliyowapaka ni ya kuona wachawi ambao wamefanya hili jambo ila iwe siri yenu na watakachotaka muwatimizie ili tusijenge vita mimi na wao kweli bana akaanza kutokea paka anageuka kuwa mtu mara ndege anakuja pale anageuka na kuwa mtu yani siku hiyo niliona kila aina ya vitwimbwi ghafla wakawa watu kama 10 hivi na kila mmoja amekuja kwa style yake wakatuuliza tumewaitia nini mganga akawaeleza shida yetu watuonyeshe dawa ya kumtibu fulani tyliye naye pale dah ila wachawi wana maneno ya kejeli yani tulitumia kama lisaa mpk kuelewana na kiasi walichokitka tukawapa nusu siku hiyo wakamuonyesha mganga dawa ya hilo tatizo ndio kupona kwa ndugu yetu ila nilipomuuliza yule mganga kwanini imetubidi tuwaite wale wachawi alisema mchawi hata uwe mganga wa aina au mtu wa aina gani wakikuamulia wakumalize hawashindwi bila kujali una imani au huna.

Nyingine ni ktk utafutaji ridhiki hapo ndio nilikuja kuona duniani kuna viumbe tunaishi navyo bila sisi kujua
 
hadi sasa bado sikubaliani na hizi mambo..
Najaribu kuamini akili inagoma kabisa.

kwanini wengine hatukutani na vitu vyenye taswila hii?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hadi sasa bado sikubaliani na hizi mambo..
Najaribu kuamini akili inagoma kabisa.

kwanini wengine hatukutani na vitu vyenye taswila hii?.

Sent using Jamii Forums mobile app
Siku utakapokutana navyo ndio utajua. Kingine Mungu ana sababu zake kwa kutoyafunua haya kwa baadhi ya watu maana wakiona wanaweza wakafa kwa mshtuko.
 
Duh mkuu hukutoka nduki kweli?
 
Siku utakapokutana navyo ndio utajua. Kingine Mungu ana sababu zake kwa kutoyafunua haya kwa baadhi ya watu maana wakiona wanaweza wakafa kwa mshtuko.
Kuna tukio moja, niliwai kudondokewa matone ya damu nikiwa ndani ya nyumba tena mchana kweupe.
Matone kama 4 yanadondoka kutoka juu ya dali, lakini nikiangalii juu sioni kitu.

ni moja ya tukio tata kwangu, hadi leo sijui nini chanzo cha ile damu.
lakini siamini kwamba ni uchawi coz uchawi kwangu ni myth tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
That's ain't enough for you to believe in which craft. It could be an injured rat running in the roof or something else I guess. Ila mkuu uchawi upo mi nishaona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…