dawa yenu
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 2,825
- 3,675
Nilipomaliza elimu ya msingi nikaenda pre form one shule fulani ya English medium ipo Njombe. Nilikuwa bweni na nilisoma hapo kwa miezi mitatu. Bweni nililokuwa nalala lilikuwa limepakana na makaburi kwa kutenganishwa kwa uzio wa mabanzi.
Mbele ya bweni kulikuwa na uwanja ambao paliwekwa bembea nyingi kwa ajili ya watoto kucheza nyakati mbalimbali. Siku moja nikiwa na mwenzangu tulitoka usiku wenzetu wakiwa wamelala tukaenda chooni. Wakati tunarudi zile bembea zote zilikuwa zimetulia, ghafla bembea mbili zikaanza kucheza Kama vile Kuna mtu anabembea.
Zilifanya hivyo kwa muda mrefu huku bembea nyingine Kama kumi na tano hivi zikiwa zimetulia. Ilikuwa ajabu Sana! Tulikimbia tukaenda kulala asubuhi tukawasimulia wenzetu, kumbe Kuna wengine Kama watatu hivi nao wamewahi kushuhudia tukio Hilo
Sent using Jamii Forums mobile app