Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Nilipomaliza elimu ya msingi nikaenda pre form one shule fulani ya English medium ipo Njombe. Nilikuwa bweni na nilisoma hapo kwa miezi mitatu. Bweni nililokuwa nalala lilikuwa limepakana na makaburi kwa kutenganishwa kwa uzio wa mabanzi.

Mbele ya bweni kulikuwa na uwanja ambao paliwekwa bembea nyingi kwa ajili ya watoto kucheza nyakati mbalimbali. Siku moja nikiwa na mwenzangu tulitoka usiku wenzetu wakiwa wamelala tukaenda chooni. Wakati tunarudi zile bembea zote zilikuwa zimetulia, ghafla bembea mbili zikaanza kucheza Kama vile Kuna mtu anabembea.

Zilifanya hivyo kwa muda mrefu huku bembea nyingine Kama kumi na tano hivi zikiwa zimetulia. Ilikuwa ajabu Sana! Tulikimbia tukaenda kulala asubuhi tukawasimulia wenzetu, kumbe Kuna wengine Kama watatu hivi nao wamewahi kushuhudia tukio Hilo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaan anasema wale jamaa wanne wanakuja kwa Kasi kuelekea lango la kambi Lakini hawafiki.....nyinyi mnakua mnawaona.......anasema Askari wa zamu wanashituana na kutoa Amri kwa sauti jamaa wanakuja tu....
Wanazikoki bunduki Kupiga Risasi hazitoki
Inabidi Askari Wakimbie wanahisi labda bunduki ndio tatizo wanaenda chukua bunduki zingine Hali inajirudia ile ile.....Wana kimbia kwenda kuita wanajesh wengine akirudi hawakuti kitu...

😄😄😄wachawi sometimes wana comedy sana.
 
Rafiki yake baba angu ambaye kwa Sasa Ni mwanajeshi mstaafu....
Walikua gadi mlangon kambini Usiku Askari mwenzao akaja kuwa taarifu Kuna jamaa wanne wanakuja kwa Kasi kuelekea lango la kambi....
Wakatoka kwenda kuwasimamisha kutoa Amri watu wanakuja....
Wakazikoki bunduki Kupiga risasi hazitoki.......
View attachment 1457550
Jamaa walipo karibia geti wakapotea tukio hujirudia rudia kambini hapo
Hii ni kawaida sana hususani unavyokuwa nondo(guard). Ni matukio ya kawaida kutokea, kama huna moyo waweza "vunja umbo."

"Ungejua alacho Kuku, usingempa mgeni."
 
Miaka ya 90 somewhere hapa Tz katika harakati za kimaisha nilikuwa nalazimika kukatiza msitu mnene mida ya sanne hadi satano usiku nikiwa peke yangu karibu kila siku.
Basi ilikuwa kwamba kila ninapofika katikatii ya msitu huo nilikuwa nakuta joka kubwa (unene wake kipenyo sentimita 20) limelala kukatizaa barabara. Mimi si mwoga, sikuwai kumkimbia yule nyoka badala yake huokota mawe na kumshambulia hadi anatokomea.

Hii ilikuwa karibu kila s

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah kweli mkuu wewe si muoga, hukuwahi kujenga picha kichwani kwamba labda kageuza kichwa anakusubiria ukatize?
 
Hilo tukio lako la kukuta watu saa tisa wapo darasani wanasoma liliwahi kunikuta hata mimi, ila mimi haikuwa darasani....ilikuwa mida hiyo hiyo mibovu, nikiwa kikosi fulani huko Nachingwea mwaka 2013. Siku hiyo nipo zamu, kiongozi wa eneo nililopaswa kulifanyia ungalizi siku hiyo. Na niliwajibika kwa sehemu mbili zote zikiwa karibu: sehemu A, na ambapo zamu ilinisoma sehebu B, lakini nikiangalia sehemu zote mbili.

Jioni katika kushusha bendera nikawapanga watu wa kituo A ndo washushe, halafu sisi wa kituo B tutapandisha asubuhi. Na mimi nilikuwa wa mwisho kulinda siku ile, ina maana baada ya kuzurura zurura mpaka saa 6 nkaamua nilale ili saa kumi nishike zamu yangu. Sasa ilipofika saa kumi kasoro nikaamka, pako salama nikawapumzisha waliopo nasi wa zamu ya saa kumi tukaamka... Nikamwambia mwenzangu hebu baki hapo mi nifike kituo A nikacheki nako kuko poa, sasa nikiwa naenda kituo A nkapita sehemu ambapo kuna milingoti ya bendera... wacha kabisa, nikakuta watu wawili wafupi mno kwa kipimo cha kawaida wananifika kiunoni, wapo kwenye milingoti ya bendera wanashusha bendera, wamevaa kombati, wana silaha kama kawaida, na nyuma yao kuna watu nane wapo kwenye paredi ya kushusha bendera! Nikatulia nikawacheki, baadaye wakamaliza, wakageuka nyuma, wakaungana na paredi hao wakasepa kuelekea kwenye misufi... na wakapotea.

Nilishangaa sana maana sisi bendera tukishusha huipeleka kituo A, wao wakapeleka kwenye misufi na wakapotelea huko. Siku za baadae nilipowauliza wakongwe wakasema hiyo ni kawaida, yaani sisi tunaposhusha hao hupandisha, na sisi tunapopandisha wao huwa washashushandio , ila shukuru hawajakuona... wakasema hivyo vituo unaweza ukashangaa hata usiku magari yanawashwa hafu humuoni anayeyawasha, mabovu hutengenezwa na usimuone anayeyatengeneza pia... nikastaajabu sana!!!
Mike omba uhamisho huko hapafai. KJ kina extra company haha.
 
Kwamatendo yangu MKUU sidhanii asee kuna mada moja nili ilose pale juu ya UMUHIMU sana yule bibie kuna day moja katika zile nne alizonijilia Night alinitia stiki balaa asee

Yaani fimbo kabisa [emoji16][emoji16] nacheka kama mazuri

Ila zile stiki zilikua miongoni yasababu yakumtafuta japo nlikuja onana nae bila kutarajia

Ila pia kinachonishangaza nikwamba aliwahi nambia anakaa maeneo flan kwenda muulizia maeneo yale hawamjui kabisaa nahayo maeneo mimi najulikana kwel kwel maana kulikua na washkaji tulikua tunapiga nao soka kitambo nahicho

Pia katika wale watu wapale aliwahi nitajia jamaa mmoja ambae alidai kuwa mwanaume wake kabla yakuwa namimi ila yule jamaa ananambia hakuwahi kuwa namwanamke wanamna hio nahamna mwanamke wabamna hio kwapale

Kuna mambo yananifiirisha sana juu yayule manzi kiukweli yaani mpaka najishangaa yule mwanadada hakua mtu wasocial media yeyote ile ila alikua namuonekano wamambo hayo baada yakuachana na mimi maana katika maisha yakawaida bina adamu tunaweza tusionane ila mpaka kule kweli kwa mitandao ?! Nahuku kwamitandao pia hakuniumizi kichwa sana kama nikifika pale mitaa alowahi nambia anakaa halafu naambiwa hakuna mwanamke wanamna yake hasa wajina lake alowahi kukaa pale nlioneshwa wanawake wanamna namajina yake wapale karibu robo nawajua maana maeneo yale najulikana na napajua vyema.....

Ila immortal how hem nieke wazi hapa.....
Sent using My COVID-19
Huyo mwanamke ni jini mkuu wala usisumbuke kutaka kujua anaishi wapi maanisha majini yote makazi yao ni kwenye mapango, kwenye maziwa na bahari.

Chamsingi tafuta dawa ya kumfukuza kabisa asitokee wala kukuharibia maisha yako. Kama ni mkristo kamwone mchungaji akufanyie maombi na kama ni muislamu nenda kwa shekhe akakufanyie kisomo.
 
Yah vituo hivyo ni vituo vigumu, ila ongeza GO na vituo vya vyanzo vya maji, kama utakuwa camp ya ndichi huko. Ni balaa

"Ungejua alacho Kuku, usingempa mgeni."
GO ndio sehemu ya combania isiyoonekana inashinda na kufanya yao kama ile parade ya kushusha bendera uliyoiona. Haha sipati picha hivyo vibwengo vilibeba vipi SAR maana ni ndefu kuliko vyenyewe😂😂
Pia siwapatii picha mpiga buriji na paredi kamanda alivyokuwa akiamrisha, yaani kama nawaona vile😂😂😂
 
Miaka ya nyuma baada ya kumtibu ndugu yetu mmoja ikashindikana kupona ndipo mganga aliposema inabidi tuwaite wachawi waliomroga ili watuonyeshe dawa mana kwangu imeshindikana tukaa kama wanafamilia tukakubaliana na maneno ya mganga siku ya siku imefika tukabeba mgonjwa mpk makabulini na mganga.

nakumbuka ilikuwa saa 8 usiku tumefika pale mganga akaanza mambo yake mara akachukua filimbi akapiga mara 3 tukaanza kuona mauza mauza mganga akatwambia mnapaswa msiogope hiyo dawa niliyowapaka ni ya kuona wachawi ambao wamefanya hili jambo ila iwe siri yenu na watakachotaka muwatimizie ili tusijenge vita mimi na wao kweli bana akaanza kutokea paka anageuka kuwa mtu mara ndege anakuja pale anageuka na kuwa mtu yani siku hiyo niliona kila aina ya vitwimbwi ghafla wakawa watu kama 10 hivi na kila mmoja amekuja kwa style yake wakatuuliza tumewaitia nini mganga akawaeleza shida yetu watuonyeshe dawa ya kumtibu fulani tyliye naye pale dah ila wachawi wana maneno ya kejeli yani tulitumia kama lisaa mpk kuelewana na kiasi walichokitka tukawapa nusu siku hiyo wakamuonyesha mganga dawa ya hilo tatizo ndio kupona kwa ndugu yetu ila nilipomuuliza yule mganga kwanini imetubidi tuwaite wale wachawi alisema mchawi hata uwe mganga wa aina au mtu wa aina gani wakikuamulia wakumalize hawashindwi bila kujali una imani au huna.

Nyingine ni ktk utafutaji ridhiki hapo ndio nilikuja kuona duniani kuna viumbe tunaishi navyo bila sisi kujua
 
Miaka ya nyuma baada ya kumtibu ndugu yetu mmoja ikashindikana kupona ndipo mganga aliposema inabidi tuwaite wachawi waliomroga ili watuonyeshe dawa mana kwangu imeshindikana tukaa kama wanafamilia tukakubaliana na maneno ya mganga siku ya siku imefika tukabeba mgonjwa mpk makabulini na mganga nakumbuka ilikuwa saa 8 usiku tumefika pale mganga akaanza mambo yake mara akachukua filimbi akapiga mara 3 tukaanza kuona mauza mauza mganga akatwambia mnapaswa msiogope hiyo dawa niliyowapaka ni ya kuona wachawi ambao wamefanya hili jambo ila iwe siri yenu na watakachotaka muwatimizie ili tusijenge vita mimi na wao kweli bana akaanza kutokea paka anageuka kuwa mtu mara ndege anakuja pale anageuka na kuwa mtu yani siku hiyo niliona kila aina ya vitwimbwi ghafla wakawa watu kama 10 hivi na kila mmoja amekuja kwa style yake wakatuuliza tumewaitia nini mganga akawaeleza shida yetu watuonyeshe dawa ya kumtibu fulani tyliye naye pale dah ila wachawi wana maneno ya kejeli yani tulitumia kama lisaa mpk kuelewana na kiasi walichokitka tukawapa nusu siku hiyo wakamuonyesha mganga dawa ya hilo tatizo ndio kupona kwa ndugu yetu ila nilipomuuliza yule mganga kwanini imetubidi tuwaite wale wachawi alisema mchawi hata uwe mganga wa aina au mtu wa aina gani wakikuamulia wakumalize hawashindwi bila kujali una imani au huna.Nyingine ni ktk utafutaji ridhiki hapo ndio nilikuja kuona duniani kuna viumbe tunaishi navyo bila sisi kujua
hadi sasa bado sikubaliani na hizi mambo..
Najaribu kuamini akili inagoma kabisa.

kwanini wengine hatukutani na vitu vyenye taswila hii?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hadi sasa bado sikubaliani na hizi mambo..
Najaribu kuamini akili inagoma kabisa.

kwanini wengine hatukutani na vitu vyenye taswila hii?.

Sent using Jamii Forums mobile app
Siku utakapokutana navyo ndio utajua. Kingine Mungu ana sababu zake kwa kutoyafunua haya kwa baadhi ya watu maana wakiona wanaweza wakafa kwa mshtuko.
 
Miaka ya nyuma baada ya kumtibu ndugu yetu mmoja ikashindikana kupona ndipo mganga aliposema inabidi tuwaite wachawi waliomroga ili watuonyeshe dawa mana kwangu imeshindikana tukaa kama wanafamilia tukakubaliana na maneno ya mganga siku ya siku imefika tukabeba mgonjwa mpk makabulini na mganga nakumbuka ilikuwa saa 8 usiku tumefika pale mganga akaanza mambo yake mara akachukua filimbi akapiga mara 3 tukaanza kuona mauza mauza mganga akatwambia mnapaswa msiogope hiyo dawa niliyowapaka ni ya kuona wachawi ambao wamefanya hili jambo ila iwe siri yenu na watakachotaka muwatimizie ili tusijenge vita mimi na wao kweli bana akaanza kutokea paka anageuka kuwa mtu mara ndege anakuja pale anageuka na kuwa mtu yani siku hiyo niliona kila aina ya vitwimbwi ghafla wakawa watu kama 10 hivi na kila mmoja amekuja kwa style yake wakatuuliza tumewaitia nini mganga akawaeleza shida yetu watuonyeshe dawa ya kumtibu fulani tyliye naye pale dah ila wachawi wana maneno ya kejeli yani tulitumia kama lisaa mpk kuelewana na kiasi walichokitka tukawapa nusu siku hiyo wakamuonyesha mganga dawa ya hilo tatizo ndio kupona kwa ndugu yetu ila nilipomuuliza yule mganga kwanini imetubidi tuwaite wale wachawi alisema mchawi hata uwe mganga wa aina au mtu wa aina gani wakikuamulia wakumalize hawashindwi bila kujali una imani au huna.Nyingine ni ktk utafutaji ridhiki hapo ndio nilikuja kuona duniani kuna viumbe tunaishi navyo bila sisi kujua
Duh mkuu hukutoka nduki kweli?
 
Siku utakapokutana navyo ndio utajua. Kingine Mungu ana sababu zake kwa kutoyafunua haya kwa baadhi ya watu maana wakiona wanaweza wakafa kwa mshtuko.
Kuna tukio moja, niliwai kudondokewa matone ya damu nikiwa ndani ya nyumba tena mchana kweupe.
Matone kama 4 yanadondoka kutoka juu ya dali, lakini nikiangalii juu sioni kitu.

ni moja ya tukio tata kwangu, hadi leo sijui nini chanzo cha ile damu.
lakini siamini kwamba ni uchawi coz uchawi kwangu ni myth tu.

That's ain't enough for you to believe in which craft. It could be an injured rat running in the roof or something else I guess. Ila mkuu uchawi upo mi nishaona
 
Back
Top Bottom