Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani


Mliwapa nini hao wachawi mpaka wakakubali kuleta dawa ya kumtibu ndugu yenu?

Haya mambo kama movie vile dooh😄
 
hadi sasa bado sikubaliani na hizi mambo..
Najaribu kuamini akili inagoma kabisa.

kwanini wengine hatukutani na vitu vyenye taswila hii?.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nimekutana navyo baada ya kuhangaika sana na hasa kuuguza huyo ndugu yangu na mambo ya biashala zangu na kwenye biashala ndio nilikutana na mambo mengi sana
 
Mliwapa nini hao wachawi mpaka wakakubali kuleta dawa ya kumtibu ndugu yenu?

Haya mambo kama movie vile dooh😄
Kutokana na tukio lile nilichojifunza ni kuwa kuna mda wachawi wanaweza kukuloga ili wapate hela na nikajifunza kuwa kumbe wachawi huwa wanapata hela sana kupitia kuloga watu na kuwadai hela kingine ni kuwa unaweza kutafuta mchawi kumbe ni mtu wa karibu yako tu kwa yale niliyoyaona pale makabuli
 
That's ain't enough for you to believe in which craft. It could be an injured rat running in the roof or something else I guess. Ila mkuu uchawi upo mi nishaona
. It could be an injured rat running in the roof or something else I guess.


Hiki ndicho nilichokihisi na hadi leo ninaamini kuwa kuna kiumbe(kama unavyosema) panya, mjusi etc alilaluliwa na mwezie.

Lakini kilichokuwa kikinitatanisha ni pale nilipokuwa ninaangalia juu sioni kitu, ila matone yanaendelea kudondoka.

Nb: kuhusu uchawi kuwepo ni ngumu kumeza sana kwangu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
 
Mimi kijijini kwetu katika mkoa wa Songwe kuna jamaa ni mtu wa kujituma kufanya kazi na ana biashara zake za kununua na kuchinja ng'ombe hivyo mshiko anao ambao umemwezesha kuwa na wake wanne.

Alinunua ng'ombe wa kisasa wa maziwa na kuwafuga ili familia yake isipate shida ya maziwa na kuongeza wigo wa mapato. Ngombe wake walipozaa alianza kuwa na mashaka na mwenendo wa utoaji maziwa wa ng'ombe wake maana kila wakienda kukamua mida ya saa kumi alfajiri wanakuta ng'ombe kesha kamuliwa hakuna maziwa, kwa mchana walipata maziwa kiasi shida hiyo alfajiri.

Jamaa akaona huu mchezo hatouweza akaenda kwa wataalamu wakampatia zindiko na kuzindika zizi la ng'ombe. Waliokuwa wanamfanyia mchezo mchafu walirudi tena wakidhani ni Kama walivyozoea ila wakaishia kunaswa mle zizini wakiwa watupu Kama walivyozaliwa. Tuliitwa kwenda kushuhudia na kuwakuta majirani wawili mwanaume na mwanamke wakiwa uchi wa mnyama hawawezi kuongea wala kutembea.

Mbele ya viongozi wa mtaa mwenye ng'ombe aliwatangazia msamaha kwamba wasirudie tena na kuamuru waondoke. Cha ajabu yule mwanamke hakuridhika alirudia tena mara hii alipigwa scud ya nguvu na kufia humo zizini akiwa uchi. Mpaka Sasa huyo jamaa hakuna anayejaribu kuharibu Mali zake hata mabinti zake wanaogopwa.
 
Duniaa ina mengi..



"Nilipokuwa mdogo ,Mama alinambia kuwa uone , binadamu wabaya na wenyee 🎶🎶🎶🎶🎶 ..

Mwenye anakumbukaa huu wimbo ,,unaitwaje ???
They are so fascinating mkuu😂
Sasa mkuu ulijuaje hayo uliyoyaona kwamba ni uchawi na sio kitu kingine tu usichokijua?.

Sent using Jamii Forums mobile app
That's ain't enough for you to believe in which craft. It could be an injured rat running in the roof or something else I guess. Ila mkuu uchawi upo mi nishaona
 
Kulikuwa na mauza uza gani na upande gani? bwawani, Kota, uwanja wa damu au mahangani? Wanakijiji wa komsanga, kodiwawala, gendagenda na chekereni hawana jipya wazigua wale..
Hahaahaha umenikumbuksha kitambo kile ..mahangani kulikua kunaibuka vitu vya ajabu .kule bwawani nako full mauza uza wanaokwenda gadi usiku
 
Kitu kimoja ambacho watu wengi hawajui ni kuwa mganga nae ni mchawi na pale walikua tayar washapangana huko nyuma na hao wenzake ili ionekane imeshindikana lkn la...ni michezo ambayo waganga wengi wanacheza na usipokuwa na akili kubwa huwez ng'amua....lkn duniani hapa tunachezeana sn michezo lkn nguvu yao ni moja hata km watakuja trilion nae ni Mungu pekeee
 
Mimi nimekutana navyo baada ya kuhangaika sana na hasa kuuguza huyo ndugu yangu na mambo ya biashala zangu na kwenye biashala ndio nilikutana na mambo mengi sana
Lete hayo mambo ya kwenye biashara hapa jitahid hata kusimulia kwa code nadhan utaokoa wengi mana wengi bado wamefungwa
 


Aisee pole sana mkuu najua hilo tukio lilikuvuruga sana kisaikolojia.
 
Yaaani nikipata hii dawa, nitafrahi sana maana kuna vidokozi wa mifugo ningewamaliza wote, tatizo upo ni mbali dah.
 
Sio st.beNedict apo man
 
Hiyo nayo kuna mshikaj aliniambia dah kumbe kweli mi sikumamini,aliniambia mkewe huwa anaona usiku wanga kwaiyo walienda kwa mganga ili wawakate wawazalilishe,mganga akawaambia hao wana jeshi lao wakikuamulia hakuna mganga anayeweza kushindana nao mradi hawawadhuru basi waache tu tusiwachokoze,mi siwezi vita nwa wachawi na hakuna mganga anayeweza nimeamua kuwaambia ukweli tu sitaki hela zenu.
 
Ndivyo inavyokuwa mara nyingi ipo hivyo mana yule mzee aliniasimulia mambo mengi mwisho alichoniambia ni kuwa madhari mgonjwa amepona ibaki kuwa siri yenu tu japo tulimuona na ndugu kabisa wa pale home
 
Ndivyo inavyokuwa mara nyingi ipo hivyo mana yule mzee aliniasimulia mambo mengi mwisho alichoniambia ni kuwa madhari mgonjwa amepona ibaki kuwa siri yenu tu japo tulimuona na ndugu kabisa wa pale home
Yani hawa kuwashinda kwao sio kwenda kwa mganga ukimjua ni kushika panga nakwenda kukatakata,vp huyo ndugu yenu baada ya kumuona alikuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…