sawima
JF-Expert Member
- Jul 9, 2019
- 5,496
- 8,491
Miaka ya nyuma baada ya kumtibu ndugu yetu mmoja ikashindikana kupona ndipo mganga aliposema inabidi tuwaite wachawi waliomroga ili watuonyeshe dawa mana kwangu imeshindikana tukaa kama wanafamilia tukakubaliana na maneno ya mganga siku ya siku imefika tukabeba mgonjwa mpk makabulini na mganga nakumbuka ilikuwa saa 8 usiku tumefika pale mganga akaanza mambo yake mara akachukua filimbi akapiga mara 3 tukaanza kuona mauza mauza mganga akatwambia mnapaswa msiogope hiyo dawa niliyowapaka ni ya kuona wachawi ambao wamefanya hili jambo ila iwe siri yenu na watakachotaka muwatimizie ili tusijenge vita mimi na wao kweli bana akaanza kutokea paka anageuka kuwa mtu mara ndege anakuja pale anageuka na kuwa mtu yani siku hiyo niliona kila aina ya vitwimbwi ghafla wakawa watu kama 10 hivi na kila mmoja amekuja kwa style yake wakatuuliza tumewaitia nini mganga akawaeleza shida yetu watuonyeshe dawa ya kumtibu fulani tyliye naye pale dah ila wachawi wana maneno ya kejeli yani tulitumia kama lisaa mpk kuelewana na kiasi walichokitka tukawapa nusu siku hiyo wakamuonyesha mganga dawa ya hilo tatizo ndio kupona kwa ndugu yetu ila nilipomuuliza yule mganga kwanini imetubidi tuwaite wale wachawi alisema mchawi hata uwe mganga wa aina au mtu wa aina gani wakikuamulia wakumalize hawashindwi bila kujali una imani au huna.Nyingine ni ktk utafutaji ridhiki hapo ndio nilikuja kuona duniani kuna viumbe tunaishi navyo bila sisi kujua
Mliwapa nini hao wachawi mpaka wakakubali kuleta dawa ya kumtibu ndugu yenu?
Haya mambo kama movie vile dooh😄