Hapa naweka stori ambayo nimehadithiwa na shuhuda na moja nili experience mwenyewe lakini sikutaka kuamini kuwa ni mauzauza.
****Niliwahi kufanya kazi kwenye hotel flan, hio hotel hapo ilipo, ikifika magharibi tu, hutamani kutoka, mana ipo isolated. Na ipo kwenye kijiji kimoja ambacho kuchawiana ni kama kunywa maji, watu hawaoni tabu kabisa kuambizana kuwa nitakuonesha. Haya mambo ya ushirikina ukiyashiriki, basi makazi yako yataathirika pia. Katika hii hotel naambiwa na wafanyakazi wa zamani kuwa mauza uza hayaishi, walinzi waliniambia kuwa walishawahi kumuona bibi kizee usiku wa manane anaenda kwenye pool anavua nguo zote anaogelea kisha anasepa zake. Kuna mfanyakazi mmoja alianguka chooni, akaanza kupapatika, kwa bahati kuna mfanyakazi (mwenyeji wa vijiji vya karibu na ilipo hotel) akasikia kishindo, akawashtua wenzake na kuwaambia wachote maji ya kwenye shimo la choo, wakampa jamaa akamnywesha yule dada, alizinduka.
*****Huyu mtu aliemnywesha hayo maji mwenzake, nimeambiwa yeye aliwahi kumfanyia dada mmoja aliekuwa mbishi kitisho. Wakati wanatia stori alimwambia kuwa hapa tulipo kuna mji mkubwa sana watu wanatembea hapa, yule dada akambishia kwa dharau, jamaa akamuuliza, je unataka kuyaona, akajibu ndio, akamwambia basi utayaona leo. basi kufika mida kila mmoja anaingia room kwake staff house, yule bi dada alikuja kumuona mshkaji yupo chumbani alipiga kelele kutoka kwa wenzake anamkuta jamaa yupo nje, jamaa alimuuliza tu nini. Bi dada naskia aliishia kusema kuwa hataki tena kuyaona.
*****Huyu huyu jamaa aliwahi kunihadithia story ambayo yeye alishuhudia mara hii. Na hii nimeconfirm kutoka kwa dada mhusika ambae kaka yake ndio yalimkuta haya. Katika management office ilikuwa kuna jamaa ameitamani nafasi ya mwenzake, maana ilikuwa ni ya kushika hela. SIku hio wakati mshika fedha kenda likizo, jamaa ananambia yeye alikuwa Restaurant anataarisha cocktail za wageni, ndipo alipomuona huyo anaetamani nafasi ya mwenzie akiingia na vibabu vizee vitatu ofisini. Ukikaa resta ilikuwa unaona ofisini ndani kama hawajafunga mlangu. Sasa mshika fedha alikuwa ameacha laptop ofisini. Vile vibabu vikafungua laptop ile na kujifanya kama vina type ivi, huku jamaa resta anawachora tu. Baada ya vile vibabu kumaliza, kila mmoja akapewa buku 50 wakasepa. Siku ya kurudi kazini mshika fedha hakufikia ofisini moja kwa moja. Alikuwa anachill TV lounge akitizama TV mwenyewe ndip hafla kichwa kikamuuma. Akainuka akamwambia yule jamaa alishuhudia mchezo sasa kuwa amtengezee chai konki mana kichwa kinamuuma, jamaa akamuuliza kimeanza kukuuma wapi, akamwambia wakati yupo anatizama TV, basi jamaa akamwambia tulia hapo hapo nakutengezea chai. Mshika fedha akasema anaenda ofisini kumalizia kazi za watu atume files kwa boss mana mda umepita wa kutuma report, jamaa akamwambia asiende ofisini na atulie tu hapo hapo kwenye TV chai inakuja. Mshika fedha alibisha na kwenda ofisini, kufika ile anafungua laptop yake tu, alianza kupiga makelele vibaya, wafanyakazi wengine walishtuka na kwenda wanamuona mtu kapata wazimu hafla, huku jamaa yupo resta anaendelea kutengeza chai aijuae mwenyewe anawachora tu. Wale wafanyakazi wakambeba kumpeleka chumbani kwake, jamaa akawaambia msimpeleke chumbani, mrudisheni TV lounge, hapo ndipo yalipoanzia, chai yake ishakuwa tayari, wafanya ubishi, wakampeleka chumbani, huko ndipo yalipozidi, akaanza kujipiga na makuta na kuvuja damu. Hapo wa dini zote wakasoma aya zao, jamaa alikuja akawaambia tu huyu kashakwisha tayari, niliwaambia mumuweke TV lounge mkajifanya wabishi. Akarudishwa kwao bara, akafariki maskini.
*****Katika kijiji icho icho, kuna jamaa alikuwa na jahazi yake katoka kupakia mizigo anasafirisha kuelekea Pemba na mombasa. Wakati anasafiri, maji yalikuwa ni low tide, kwa bahati lile jahazi likagonga mwamba na kutoboka, maji yalianza kuingia ndani lakini hayakuzamisha jahazi kwa sababu hakikuwa kina kirefu, sema jahazi lililala upande. Mwenyewe akashuka na kuliangalia, akaanza kusikitika, alitokea mzee from nowhere, akamuuliza shida nini kwani, jamaa akamuelezea akamwambia usijali utaondoka hapa, jahazi lilipigwa makofi na likainuka na kuendelea na safari. Hii siwezi kusema kama kweli au uwongo, alienipa hii habari ni mtu wa hapo kijijini na alikuwa serious, mana alikuwa ananipa mikasa ya kijijini kwao.
Sasa nilioshuhudia mwenyewe kwa macho, sio ya kutisha kiivo, naamini uchawi upo, lakini kwanza napenda kufikiria kuwa ni mambo yanayoeleweka kwanza kabla ya kuconclude ni uchawi.
******Nilitoka kazini mida ya saa sita usiku na kwenda staff house, nikatulia natizama documentaries youtube mpaka kama saa tisa inakaribia, nikasema niende nkaoge then nirud kulala tu. Niko kwenye shower maji yalikuwa baridi kidogo lakini si kiivo, nilanza kuona naishiwa nguvu, halafu kama kuna mikono mabegani yananisukuma chini, najiforce kusimama lakini nilishindwa nikajikuta nimekaa kwenye shower chini mzee sina nguvu, moyoni najisemea yale nnayoyasikia kweli yanataka kunitokea? basi sikufanya ubishi nikatulia kitako chini nikakubali nisiforce mwili kupambana, apo apo nikasema, au labda maji haya yalikuwa yabaridi. hapo bado maji yalikuwa yanatiririka. Nikajitahid kufikia mfereji kwa mkono nikapata ya maji ya moto, nikayafungua full nikarudi kupata nguvu nkasimama fresh. nikajisemea kuwa kama sababu maji ya baridi au ya moto, wacha nitoke chooni nkajilalie. Lakini akili ikanambia nimalizie tu kuoga, niliendelea kuoga na maji mchanganyiko yabaridi na yamoto yanatiririka lakini ya moto yalikuwa yamoto kweli mana hakukua na baridi, ebana hali ikajirudia tena, nikakalishwa chini, nikatulia hapo na nilipopata nguvu y kusimama nilivuta taulo nkaenda chumbani tu kulala.
****** Hii hapa ilikuwa nipo TV lounge hapo hoteli, baada ya kumaliza mechi ya Champions League tukabaki watu wawili tu tunatizama Tv mpaka saa nane usiku hapo mwangu ulokuwepo ulikuwa na wa TV na choo cha TV lounge tu hio Lounge tulizima taa, mara hafla nikasikia harufu nzuri sana, nikauchuna. ikapotea. Mara baada ya mda mfupi kidogo, nikasikia tena ile harufu hapa nikashindwa kuvumilia, nikamuuliza mwenzangu "Nasikia mie au na wewe umesikia?" Akaniuliza hio harufu? nkamwambia ndio, akajibu baba namie niliisikia mwanzo ikapotea ila ikarudi saivi, nkamwambia zima TV mzee baba tuwaachie wenye ukumbi wao. Tulisepa zetu tu.