Ilikua mwaka 2004 nikiwa darasa la 5 mkoani Dodoma mitaa ya mailimbili almaarufu kwa Mwarabu.
Tulikua na nyumba kubwa tu ya vyumba kama 10 na frem tatu ambazo tulipangisha vyota tukabaki na vyumba 2 na seble tukivitumia kama familia. Kulia chumba cha wazee, katikati seble na kushoto chumba chetu ambacho kwa wakati huo tulikua tunalala watu 6, Mimi na broo kitanda cha kulia, madogo wawili kitanda cha pili na chini ya mlango wa kutokea sebleni kulikua na madada wawili wanalaza godoro chini na wanalala hapo.
Ilikua tumeshazoea shoo za ucku za kuckia watu wanatembea juu ya bati mpaka tukawa tunaona kawaida tu plus mandoto yasioeleweka pamoja na mauzauza mengi yaliyokua yakimtokea mama ndani kwake, lakini akawa hatusimulii coz alihofia kututisha na vle tulikua bado wadogo, so alimezea tu.
Kimbembe kilianza saa 8 za ucku broo aliamka akaniamsha nimsindikize chooni (choo kilikua nje) akakojoe. Nikaangalia saa yangu (nlikua nalala nayo) nikakuta ni saa nane na dkk kadhaa iv. Nikakataa kumsindikizs kwa uoga tu na vile nlikua nikiamini mida ya wachawi ni kuanzi saa 7 hadi 11. Nikamwambia mida hii siwezi kutoka akanambia poa na ww kuna cku utabanwa afu utaona.
Basi akafungua chandarua akatoka nje ya kitanda wakati huo me nmelala upande ukutani. Akawa kama anapiga push up iv baina ya vitanda viwili. Katika hali isiyo ya kawaida watu wote mle ndani tukajikuta tupo macho na stori zikaanza ucku ule huku broo bado akiwa nje ya kitanda.
Tulipiga story nyingi ucku ule mpaka mmoja wa wale wanawake akasema jamani tulaleni ucku tunapigia watu kelele. Tukakubali wazo la kulala ( broo bado yuko nje ya chandarua).
Yule binti alosema tulale wakati anajifunika vzur ili alale akageuka upande wa pili ndo tuamsikia akisema kumbwambia mwenzie "Fatuma muone huyu mtu kalala hapa". Kalikua na kamtu fulani kafupi kamelala pembeni yao lkn kwa nje ya chandarua. Ndipo Fatuma alipotazama akakiona na chenyew baada ya kuonekana kikainua pale kikawa kinakuja upande wetu mm na broo. Broo alipokiona alipanda kitandani katika spidi ambayo sikuielewa kwa kwel. Ndani ya sekunde chache tu alifungua chandarua akapenda kitandani akanitoa upande wa ukutani akaniweka mwanzo wa kitanda. Na hapo ndipo kelele za kumwita mama zilipoanza ( Baba alikua mpwapwa kikazi).
Tulipiga kelele za kuita mama huku mmoja katika wale mabinti akikitukana kile kimtu matuc heavy. Kikawa kinaendelea kuja upande wetu huku kimetunyooshea mikono kama style ile mazombi wanafanya. Wakati tunaendelea kupiga kelele nikackia kama mama anafungua mlango kuja ndani kwetu. Kile kimtu kilikuja mpaka pembeni yangu kabla ya kugusa kitanda kikapotea na hapo hapo mama akafika ndani kuangalia kuna nin.
Kwa kweli tulikua tunatetemeka na hakuna hata mmoja aliyeweza kumueleza mama kilichotokea. Basi mama akatubembeleza pale tulale kwa hakuna tena tatizo tukawa kama tumemwelewa iv.
Wakat anatoka kurud ndani kwake wote tukaanza kumfwata kwa nyuma hatukutaka kubaki.
Akatumia busara akatuletea redio akaweka kanda ya Quran then akatwambia hapo hakuna mchawianaweza ingia tena. Hapo kdg tukapata nguvu ya kulala.
Siwez kusahau abadan ile cku. Ilipita mwez mzima hatuwez lala bila kuweka casette za Quran
Litabaki tukio kubwa sana la kutisha nlilolishuhudia kwa macho yangu na siwez kilisahau na hasa pale broo alivokuja kujificha yeye kupitia mimi akaniweka mwanzo ili iweje? si nianze kunyongwa mimi au?
Kila nimimuuliza huwaga hanipi majibu ya kueleweka anacheka tu.