Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jitahidi. Kabla kulala umtaje mwenyezimguu kwa imani yako. Na uachane usitumie vilevi punde unaenda kulalaMi sijielewagi kabisa
Sijui huwa sioti ndoto isipokua ndoto mbaya za KUTISHA?
Sikumbuki kiwahi kuamka na kukumbuka ndoto nzuri nilio iota
Siku ikitoka nimeota basi itakua nakabiliwa na hatari kubwa na ninakua kama ninusu nimelala na nusu nipo macho
Imefikia hatua sasa ndoto hizo zikinijia najiambiza binafsini nikiwa ndotoni kwamba hii ni ndoto tu na najua nifanueje kuimaliza fasta niamke
Ungekubali kutoka nje ingekuwaje?Ilikua mwaka 2004 nikiwa darasa la 5 mkoani Dodoma mitaa ya mailimbili almaarufu kwa Mwarabu.
Tulikua na nyumba kubwa tu ya vyumba kama 10 na frem tatu ambazo tulipangisha vyota tukabaki na vyumba 2 na seble tukivitumia kama familia. Kulia chumba cha wazee, katikati seble na kushoto chumba chetu ambacho kwa wakati huo tulikua tunalala watu 6, Mimi na broo kitanda cha kulia, madogo wawili kitanda cha pili na chini ya mlango wa kutokea sebleni kulikua na madada wawili wanalaza godoro chini na wanalala hapo.
Ilikua tumeshazoea shoo za ucku za kuckia watu wanatembea juu ya bati mpaka tukawa tunaona kawaida tu plus mandoto yasioeleweka pamoja na mauzauza mengi yaliyokua yakimtokea mama ndani kwake, lakini akawa hatusimulii coz alihofia kututisha na vle tulikua bado wadogo, so alimezea tu.
Kimbembe kilianza saa 8 za ucku broo aliamka akaniamsha nimsindikize chooni (choo kilikua nje) akakojoe. Nikaangalia saa yangu (nlikua nalala nayo) nikakuta ni saa nane na dkk kadhaa iv. Nikakataa kumsindikizs kwa uoga tu na vile nlikua nikiamini mida ya wachawi ni kuanzi saa 7 hadi 11. Nikamwambia mida hii siwezi kutoka akanambia poa na ww kuna cku utabanwa afu utaona.
Basi akafungua chandarua akatoka nje ya kitanda wakati huo me nmelala upande ukutani. Akawa kama anapiga push up iv baina ya vitanda viwili. Katika hali isiyo ya kawaida watu wote mle ndani tukajikuta tupo macho na stori zikaanza ucku ule huku broo bado akiwa nje ya kitanda.
Tulipiga story nyingi ucku ule mpaka mmoja wa wale wanawake akasema jamani tulaleni ucku tunapigia watu kelele. Tukakubali wazo la kulala ( broo bado yuko nje ya chandarua).
Yule binti alosema tulale wakati anajifunika vzur ili alale akageuka upande wa pili ndo tuamsikia akisema kumbwambia mwenzie "Fatuma muone huyu mtu kalala hapa". Kalikua na kamtu fulani kafupi kamelala pembeni yao lkn kwa nje ya chandarua. Ndipo Fatuma alipotazama akakiona na chenyew baada ya kuonekana kikainua pale kikawa kinakuja upande wetu mm na broo. Broo alipokiona alipanda kitandani katika spidi ambayo sikuielewa kwa kwel. Ndani ya sekunde chache tu alifungua chandarua akapenda kitandani akanitoa upande wa ukutani akaniweka mwanzo wa kitanda. Na hapo ndipo kelele za kumwita mama zilipoanza ( Baba alikua mpwapwa kikazi).
Tulipiga kelele za kuita mama huku mmoja katika wale mabinti akikitukana kile kimtu matuc heavy. Kikawa kinaendelea kuja upande wetu huku kimetunyooshea mikono kama style ile mazombi wanafanya. Wakati tunaendelea kupiga kelele nikackia kama mama anafungua mlango kuja ndani kwetu. Kile kimtu kilikuja mpaka pembeni yangu kabla ya kugusa kitanda kikapotea na hapo hapo mama akafika ndani kuangalia kuna nin.
Kwa kweli tulikua tunatetemeka na hakuna hata mmoja aliyeweza kumueleza mama kilichotokea. Basi mama akatubembeleza pale tulale kwa hakuna tena tatizo tukawa kama tumemwelewa iv.
Wakat anatoka kurud ndani kwake wote tukaanza kumfwata kwa nyuma hatukutaka kubaki.
Akatumia busara akatuletea redio akaweka kanda ya Quran then akatwambia hapo hakuna mchawianaweza ingia tena. Hapo kdg tukapata nguvu ya kulala.
Siwez kusahau abadan ile cku. Ilipita mwez mzima hatuwez lala bila kuweka casette za Quran
Litabaki tukio kubwa sana la kutisha nlilolishuhudia kwa macho yangu na siwez kilisahau na hasa pale broo alivokuja kujificha yeye kupitia mimi akaniweka mwanzo ili iweje? si nianze kunyongwa mimi au?
Kila nimimuuliza huwaga hanipi majibu ya kueleweka anacheka tu.
ata cjui ingekuaje akili zangu za kitoto nlikua naamini nikitoka mida ile ya ucku lazma ningekutana na mchawi au jini so nikawa naogopa kutokaUngekubali kutoka nje ingekuwaje?
walikuwa uchi?Kuna mwaka 2010 hivi ujana wetu tulikuwa tunataka kuona wachawi usiku kuna Mzee mmoja jirani yetu akatuambia mna moyo pia mna Siri tukamjibu tuna moyo na tuna Siri akatuambia mkitangaza mtakayoyaona mtakufa sie tukajibu atuwezi basi baada ya siku mbili akatuita njooni tupige story ili muone wachawi tukaenda kama mida ya saa kumi tukaoga dawa dawa nyingine tukanawa usoni tukakaanae barazani akatuambia subirin ilipofika kama saa Saba usiku hivi tukasikia jogoo wanawiki ss Mzee akasema ss hiyo ndio muito wao mara tukaona kundi kubwa la watu sio wengi kivile halafu kuna wengine tunawajuwa wangeni wafanyabiashara wanatuuzia vitafunwa wengine wafanyakazi tunawajua vizuri halafu kuna wazee watatu wakaja Hadi karibu yetu wakamwambia unataka tuwauwe hawa vijana akawaambia musiwauwe basi Yule Mzee akatuambia msitangaze Kwa mtu yyte kitendo cha kutangaza mnaweza mkafa bure Kwan wachawi hawependi wajupikane tangu siku hiyo kutaka kuona vitu visivyoonekana mwanza na mwisho
Walivaa sutiwalikuwa uchi?
Duh kwahiyo watu walikuwa wanakula hayo maembe?Nikiwahi kuhadithiwa na mzee wangu aliyekua anafanya kazi katika shule moja mkoani Tabora kwamba kuna mwanafunzi alipewa adhabu achimbe shimo lenye kimo kama chake na akimaliza aripoti kwa mwalimu aliyempa adhabu.
Shimo lilivyokamilika mwanafunzi hakuonekana tena shuleni tokea siku hiyo na lile shimo iliamriwa lifukiwe. Baada ya miezi kaza pakaota mti wa mwembe ukawa unazaa maembe mazuri sana lakini kila yakianguaka kwa kuiva au kutunguliwa ndani huwa linakuwa na damu.
Pole mkuuDogo hayupo tena duniani..ila naamini aliko saivi yupo huru kabisa..
Hii hali unayo mpaka sasa Vi?yes nikikasirika vitu vinavunjika au naanguka naumia
imepungua sasa hiviHii hali unayo mpaka sasa Vi?
Ulishafanyia kazi ushauri baadhi ya wadau waliokupa humu Kama vile wakuwaona viongozi wa dini yako na kupata ushauri toka kwao? Au kuipractice nguvu uliyokuwa nayo kwaajili ya manufaa yako?imepungua sasa hivi
Hapana na kusahau nishasahau labda nisome upyaUlishafanyia kazi ushauri baadhi ya wadau waliokupa humu Kama vile wakuwaona viongozi wa dini yako na kupata ushauri toka kwao? Au kuipractice nguvu uliyokuwa nayo kwaajili ya manufaa yako?
Haha ulichukulia simple. Tuyaache hapaHapana na kusahau nishasahau labda nisome upya