Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Si faida hiyo Mkuu? kwanza anaolewa Mahari inatolewa, anapewa hela na mumewe kodi ya Meza, hali kwa jasho tena, angewashukuru waganga!
 
we mwanangu kwa ubishi huu,nadhani tukio pekee unalotakiwa kufanyiwa na wachawi

wakuchukue usiku wakuweke juu ya bati,ukiamka asubuhi ujikute kule juu ya dish la DSTV.

NADHANI baada ya tukio hilo utakua na adabu sana na ukiskia mchawi tu lazima usalimie.
 
Hapo nilivyosina akili nitasema dunia ililuzi gravity kwa muda hivyo nikachomoka ndani naelea mpk huko juu ya paa!!.

Nimekuwa nikisikia tu mambo hayo ila hakuna alieweza nithibitishia hapo ndipo tatizo linapoanzia.. ni sawa na mtoto umuambie huu ni moto unaunguza!! Atajiuliza kuunguza ni nini..?
Sasa hapo ndipo atakapotaka kutest moto unavyounguza!😅
 
B Baada ya kusoma hapa nimesisimka mwili mzma
 
Acha nami nishee story yangu japo si mzuri sana katka uandishi.
Ilikua 2010 Dar es salam enzi hizo nikiwa mwanafunzi wa chuo kimoja hapo. Ukweli sikukutana nakiumbe cha kutisha bali ni binaadam alienifanya nibaki na sintofaham na maono tofauti ktk maisha.

Sikubahatika kupata chumba ktk hostel za chuo ikanibidi nipange kitaa flan uswahilini karibu na mwenge hapo. Maisha yalikua fresh tu fadha house alikua na wake wawili na watoto kadhaa hapo kijana mkubwa wa mwenye nyumba alitokea kua mwanangu sana story za hapa na pale, jamaa alikua mstaalabu sana na anasura ya upole by that time alikua kama ana 30 yrs nakuendelea.

Tukio lilotokea lilinifanya nibaki mdomo wazi ni siku moja mida ya saa tisa kasoro huyo bro aliniamsha kwa kugonga mlango nlisita kuitika lkn mwisho nilifunua nakumkuta amemkamata kijana mmoja wa makamo. Jamaa akanambia kwamba huyu ni mwizi na huwa anaibia watu hapo mtaani. Nikamuuliza vp ushahidi unao akadai hana ila amemkuta na kisu mfukoni. Nilitaka kuacha kumpa ushirikiano ila nikaona nimsaidie huyo kijana asijedhurika kwani hakukua na ushahidi wowote.

Nilimshauri jamaa kua tuamshe majirani au ndg zake jamaa akawa mbogo. Ilibidi nimfate kwanyuma akiwa amemkamata yule kijana shingoni tukielekea nyumba iliokua opposite na hii tunayokaa. Nilipata bahati ya kumuuliza jamaa akakubali ni kweli hapo aliwahi iba shati na sendoz. Nilijua itakua kesi ndogo lkn tulipofika kwa huyu jirani aligonga mlango mara mbili tatu huyo mzee akafungua na kuelezwa dhumuni la sie kuwepo hapo. Alimtazama yule kijana kwa macho ya dharau na kuulizia mimi kwani hakuwahi niona maeneo hayo ndo jamaa akanitambulisha kama mpangaji wao. Yule mzee haraka bila uoga alitupa jukumu tumuue huyo dogo then tukimaliza tumchome moto hapo hapo.

Nilihisi kuogopa nikaona ni kama mzaha vile kwani tulikua wawili tunaopewa jukum hilo. Alipomaliza kufunga mlango wake mzee yule nilimwambia huyu mshkaj kwanini tusimteme tu dogo coz vitu alivyoiba nividogo sana. Msela alinifokea sana na kunipolomoshea matusi makali. Ilibidi niwe mtazamaji asikwambie mtu kifo ni kitu rahisi sana, dogo alishushiwa kipigo hevy ngumi na mateke mpaka akazimia ndipo jamaa alipoanza kutumia mawe yaliyokua pembeni . Ilifika muda dogo alipiga mayowe maskini it was too late, jamaa alihitaji kuua siku hiyo.

Baada yakama dakika saba dogo alivuta nikimshuhudia alimsihi yule jamaa akimtaja kwa jina kua unaniua bure bro mimi ni mdogo wako, haikusaidia kitu dogo alipigwa taili mbili na kumwagiwa mafuta ya taa. Aliwaka mpaka mwisho. Niliogopa sana na usiku huo sikulala tena taswira ya kile kipigo ilikua ikinijia kichwani. Niliogopa sababu dogo alouwawa na huyu jamaa ni wa pale mtaani vp mimi mgeni. Nakwanini jamaa hakutaka watu waamshwe na dogo mbona hakua amemuibia huyu jamaa kitu.

Ilibidi iwe siri yangu mpaka nilpokuja kufahamishwa na majirani wengine juu ya kuokotwa mara kwa mara maiti zisizo julikana mtaani. Ilibidi nihame kimya kmya na kujiapiza kua sintokuja kupanga uswahilini tena na hawa binadam wenye sura nzuri za upole niishinao kwa tahadhari kubwa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa mwaka 2009, Kuna siku nimelala nikawa naota kuwa nimepanda daladala kituo cha mwenge naelekea posta basi nikawa nimekaa siti ya nyuma ya Costa.

Basi kufika kituo cha Victoria akapanda mdada mmoja akaja kukaaa karibu yangu siti ya nyuma,tukaendelea na Safari kufika kituo cha mbuyuni yule dada wa ndotoni akaniachia kikaratasi kina namba za simu akashukia kituo cha mbuyuni,baada ya mda nikastuka kutoka ndotoni kucheki saa ya simu mda huo ni saa tisa za usiku.

Basi nimestuka kila kitu kwenye ndoto nilikuwa nakumbuka mpka namba za siku,kesho yake nawahadithia ndugu zangu nilichoota ndotoni na mpka namba za siku zilizokuwa kwenye karatasi nazikumbuka,wakaniambia tujaribu kuzipiga.

Baada ya kupiga anapokea msichana ana lafudhi ya kiarabu anaitwa Nasrat na anaishi sinza,nilichofanya ni kuvunja laini na kutafuta line nyingine mpka leo sielew ile ndoto na coincidence zake
 
Ndio naona hii post leo hakika nitakuja best

Jr[emoji769]
 
Kisa changu ambacho sitokisahau Cha kutisha kilitokea Mtwara 2010.
Nilipomaliza chuo niliomba kufundisha shule moja inayomilikiwa na masista wa kikatoliki Mtwara mjini. Tulipewa nyumba nzuri kabisa maeneo ya Shangani East karibu na bahari, mtaa huu huishi mabosi, ila Hawa masista Wana nyumba zao huko.

Kwakuwa tulikuwa mabachela tuliishi nyumba moja kila mtu chumba chake, tulikuwa wanne. Kila jioni tukitoka kazini tulikuwa na mazoea ya kwenda beach had Giza linatukutia hukohuko. Siku moja tukiwa tupo beach, peke etu(Mana wikiend ndo watu walikuwa wengi)
Tukamwona binti wa kiarabu anatembea pembezoni kabisa yanamoishia maji. Amevaa mavazi ya ufukweni. Sisi tukaona Ni kawaida, na yy yupo kupata upepo mwanana Kama sisi, hatukuwa na time nae tuliendelea na story.

Alipofika usawa ule tulipo akasimama, lakini alitupa mgongo, yaani akiitazama bahari na sisi tunamtazama kisogoni. Kufumba na kufumbua kumbe tulipatwa na usingizi wa ghafla na Giza limeanza kuingia Mimi nilikuwa wa Kwanza kuzinduka nikamwona Yule Dada anapotelea baharini Bila kuzama kwenye maji. Nikawastua jamaa, tulitoka mbio nakumbuka kulikuwa na manyunyu mda huo. Tuliteleza njian na kuanguka Kama walevi.

Tuliingia ndani na kujifungia milango kila mtu chumbani kwake, hatukupika kabisa siku hiyo kwa hofu. Hili tukio namkumbushaga rafiki angu ambaye sasa ni pastor mkubwa tu jijini Dodoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh pole mkuu vp walivyoawaachia hamkuwafata na mapanga asubuhi huku mkitema povu?
Mkuu.. thubutu ile ganzi ya kupooza viungo ilikuwa ni tiba yetu tosha, tulisamehe tukamuachia Mungu tu
 
tangu mwaka huo nahisi hujaenda tena mikindani[emoji23]
 
tangu mwaka huo nahisi hujaenda tena mikindani[emoji23]
Niliachana na private school, nilipata ajira ya serikali mikoa ya nyanda za juu kusini. Japo napenda sana zile moments za beach, upepo mwanana na kutizama vyombo vya wavuvi baharini na vitoweo Kama ngisi, pweza, kamba, kolekole, kibua, changu na kumbwa ndo basi tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee pole sana
 
Alikuwa Elisha, na msaidizi wake alikuwa ni Gehazi, ndie ambae alifunguliwa macho.

Elisha alirithi upako kutoka kwa Nabii Eliya, Eliya alipokufa, Elisha aliomba kwa Mungu apewe upako mara saba wa Eliya.

Huyo Eliya naye alikuwa ni wa moto saana Mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee huyo jamaa ni katili,mi ningeama kesho yake asubuh mapema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Matukio ya kutisha niliyowahi kushuhidia katika maisha yangu ni haya yafuatayo sitokuja kusahau kabisaaa[emoji41]

1. Nikiwa mwanafunz wa primary huko nyanda za juu kusini, maeneo ya nyumbani kwetu nikiwa naishi na shangazi yangu pamoja na wazazi japo wao walikua busy kidgo , shangazi alikua ndo kila kitu kuhusu kushiba usafi wa home nk. baada ya kutoka shule nachukua maji kwenye dish naenda kuoga nsmuacha shangazi Yule pale anapika, baada ya kuoga natoka zangu nashtushwa na sauti ya shangazi akisema maneno ya kiluga chetu akitaja jina langu, mfano, John kimbia mwanangu nyoka huyo anakufuata niliruka nilikimbia adi jikoni ile kugeuka nyuma naona joka la ajabu ambalo sijawahi ona kabisa lilikua ni joka linalovutia kwa kuliangalia kwani lilikua na rangi za aina tofauti tofauti kana kwamba lilichorwa na , lilikua na mistari ya kuvutia Sana baada ya shangazi kuendelea kupga kelele na kulia taratibu lilirudi zake bafuni toka siku hiyo nligoma kabisa kuoga mule.

2. Nikiwa form two usiku bwenini tukiwa tumelala ghafla Kama bluamshwa vile ile kufunua shuka namuona mwanamke akiwa amebeba mtoto mgongoni, Yule mwanamke alikua anatembea tembea mule bwenini kana kwamba Kuna mtu Ana mtafuta lakini hamuoni, nilimuona akiamia chumba kungne baada ya muda kidgo kupita nilimuona akija adi nilipokua Mimi alisimama kwa muda kidgo mm nikajifanya nimelala ili asinigundue baadae aliamua kuondoka zake, asubuhi nlisikia watu wakilalamika wameamka tofauti na waluvyo lala( waliamka kichwa kikiwa upande wa miguu, sio mmoja zaidi ya watatu wali lalamika sikusema nliyoshuhudia.


3. Baada ya kuamia kwenye shule flani huko Ruvuma nikiwa form 4 nikiisha ndgu yangu mwalimu tukiishi Kota za walimu, siku hiyo nikiwa darasani Mara ghafla nilipata uchovu wa ghafla kikiwa na mwalimu darasani niliomba ruhusa ili nikapumzike nliruhusiwa nlipofika ndani nikakaa kitandani MAAJABU ghafla km usingizi mzito Sana wa macho ulinijia na Kuna nguvu ilikua ikinisukuma kwa nguvu kitandani nikiwa miguu iko chini MAAJABU, nliona kiumbe sio kiumbe sijui ni Nini kile alikua km mwanamke akiwa kwenye umbile la maji yanayo cheza cheza ila yakiwa yameform umbile la binadamu kabisa kuanzia kichwa adi chini lakini hayamwagiki, alikukuja akanikalia hapa kiunoni na kuanza kunipa denda na mikono ikinipapasa nyeti zangu kwa nje, nlijitahidi kukwepesha mdomo lakini sikuweza alifanikiwa kudenda, nlipojitahidi kupapasa mikono sikushika maji nilishika vidole ambavyo vilikua sio vya binadamu vilikua Kama vidole vya miguu ya kuku hivi na kucha zake ,nlijilazimisha kumshinda lakini nilishindwa baada ya dakika kadhaa alitoweja Cha AAJABU akili ilirudi vema sio katika uchovu nliotoka nao darasani. .

4. Nikiwa advance level shule flani ya jeshi hapa Tz, siku flani bwenini usiku wanafunzi wamelala , Kama nimeashwa hivi naona Kama mtu hivi akiwa Hana miguu Wala kichwa yaani Kama mavazi meusi yameform umbile la binadamu akiwa ametokea mawingu ya chini aridhini anakuja juu( jitahidi kunielewa ) akaja adi nilipokua nimelala akiwa ameshika fimbo akiinyosha kwangu shingo ikageukia upande wa ukutani kwahiyo sikuelewa alichokua anafanya na nilijaribu kurudisha shingo ili nimuone lakini nilishindwa baadae alipotea , kesho yake nlifukuzwa shule moja kwa moja baada kukutwa asubuhi bwenini muda nliopaswa kua assemble, na ilikua sio kawaida yangu kukaa bwenini muda huo, na nlibaki kwa sababu nlikua nikitafakari kile nilichokiona usiku wake nlipopewa adhabu nlikataa katakata na kumtisha mwalimu, sikua na tabia za watukutu pale shuleni kwani nlikua mwanadini Sana nikihudhuria vipindi vya maombi pasi kukosa SITOSAHAU, nliharibikiwa Sana najitahidi kusahau lakini nishindwa

SITOSAHAU HAYO MAMBO KAMWE



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole je hayo maajabu siku hzi vp yameacha?
 
Dah!... huo ni ukatili aisee, huo mtaa sio wa kuishi kabisa bora ulihama.
 
ni Aqu........ sio mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…