Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Aisee kama movie huyo jamaa hata polisi hawakumtafuta[emoji22] eeh
 
pole
 
Usiku mmoja nilikuwa nimelala ghafla nikahisi kama kuna mtu chumbani kwangu nikaamua kufungua macho na kukiona kiumbe wazungu wanaitwa black shadow amekaa kwenye stuli yangu ambayo niiacha laptop hapokipo katika shape ya mtoto wa kike huku ameshika mdoli cha kushangaza sikuweza kumove zaidi ya macho nikashangaa tunaanza ongea mental(bila kutumia midomo) nikamuuliza ww nani akawa ananiambia toka kwenye mwili wangu sio wa kwako naomba mwili wangu aisee niliogopa sana nikamwambia mbona huu ni mwili wangu akaanza kunisogelea nikafumba macho na kuanza kusoma dua ndipo nikastuka aisee sikulala usiku mzima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kisa chengine nakumbuka wakati nikiwa mdogo nacheza na watoto wenzangu ghafla nikamuona dada yangu mtoto wa ba mkubwa akipita maeneo ya uchochoroni nikamkimbilia kwenda kumpokea na kumhug ghafla giza nene likatanda machoni mwangu nakuja kuamshwa eti nilizimia pale uchochoroni kurudi home nikaulizia dada amekuja nikaambiwa mbona yupo chuoni kwao na huku hakuja. NIKIKUMBUKA HILI TUKIO HUWA MWILI UNASISIMKA
 
Aisee umenikumbusha nilivyotrmbea kutoka Arusha Mpaka Tinde kwa mguu
bila kujijua
 
Sijawahi kumbana na visa vya kutisha-ila maisha yangu yanavyokuwa na vikwazo na mbinde kibao...naamini uchawi upo kabisa.
Ila roho inagoma kwenda kwa mganga wa ndagu-...ila nasurubika mno

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekuona sehemu nyingi upo down
pole sana mkuu,maishs yana downs nyingi sana kuliko ups,
jipe moyo attracts positive energy na usonge mbele,
binafsi nimeamua tu kugeukia upande wa pili.
 
Hahahaaa Mimi ilikuwa siyo kukimbia,
nilikuwa nakatiza uwanjani mida ya saa sits hivi,
Ila nikitembea nasikia kabisa maisha yanaendelea kama mchana,napishana na watu na wanaongea,
nilikuja kushtuka alfajiri natembea palepale uwanjan
 
Mkuu hiyo ID name ina akisi mapito yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hhhha hivi sio movie kwel hiyo kiongozi!😀
 
Duuuuh aisee[emoji17][emoji17]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawapa story ilimtokea Aunt yangu kabisaa ni member wa jf pia, (i'm sorry Aunt nashare story yako, usinachambe, lol)

Siku moja yupo mitaa ya kariakoo anashangaa shangaa madukani ghafla akatokea mzee mmoja wa makamo akamsabahi kwa bashasha sana, akamuita jina lake na ubin wake, Aunt alijaribu kuvuta kumbu kumbu ni nani huyu kabla hajapata jibu yule mzee akajitambulisha majina yake yote matatu, mmh Aunt akakumbuka mbona huyu niliambiwa alishafariki ila akashindwa kumwambia hilo, kwa hiyo na yeye akamchangamkia na kukumbushana mawili matatu ya watu waliowafahamu,

Yule mzee akamwambia Aunt yeye anafanya kazi duka la muhindi akamuonesha duka lilipo halikua mbali na pale, akamwambia akiwa anahitaji chochote kariakoo afike pale dukani amuulizie kwa jina X (akamtajia a.k.a yake) atampata na kumpa msaada, basi Aunt akashukuru na kuondoka zake.

Lakini alikua bado ana wasiwasi, akampigia simu dada yake (mama yangu), hivi fulani bin fulani unafahamu habari zake? Dada yake akamwambia looh mbona alifariki miaka mingi sanaaaa, tushaanza na kumsahau,

Aunt alitetemeka, alishindwa kwenda kwake akaenda kwa dada yake, akamuhadithia alichokiona, dada yake akampigia simu ndugu wa karibu kabisa na yule mzee akauuliza habari zake jibu ni lile lile ushasahau kama fulani alifariki na tukazika miaka takribani 10 sasa, aliugua kichwa tu akafariki, na alizikwa mkoa wa mbali na pale Aunt alipomuona,

Waliogopa kumwambia yule ndugu aliyoyaona Aunt, lakini shoga angu mimi alishikwa na homa kali wiki nzima, alibaki mdogo akajuta ile safari yake ya kariakoo, hahaha

Uchawi upo kama ambavyo Corona ipo.

Boost your Immune System to fight a Covid-19.
 
Eliya mtishbi.
binadamu pekee aliepata nafasi ya kurudi duniani Mara ya pili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…