T11
JF-Expert Member
- Oct 11, 2017
- 5,101
- 4,560
[/QUOTE]Hii habari ya ikifika usiku ndio unajua kazi imeanza imenikumbusha mbali sanaNimeandika hapo na usingizi mwenyewe umekata maana hata chumba nilichopo nakiogopa ila mambo haya ni nguvu ya kishirikina na ninadhani ule ulikuwa ndio mwisho wangu ila Mungu mwenyewe alinipigania ila uchawi upo na unafanya kazi vizuri sana ile kitu ilikuwa planned na walioplan mmoja akiwa ni jirani yetu japo kwa umri sasa hivi ni mzee sana na wenzake walishatangulia mbele ya haki ila kiukweli mambo ni mengi mie ilikuwa ikifika usiku ujue raha sina maana najua kumekucha hakuna kulala moja ya tukio kuna siku pale home baada ya tukio hilo ilikuwa jmos asubuhi nikaambiwa nikateke maji mtoni nikazingua nikaendekeza kucheza kuja kustuka bi mkubwa ananiita huwezi nikakimbilia porini kwa kuogopa kuchapwa toka saa nne aasubuhi ajabu ni kuwa nilikuwa sijui polini nimeenda kutafuta nini na kumbuka tabora kunaoongoza kuwa na nyoka koboko basi mie ndio nikaenda huko zungunga sana jua la saa nane nipo huko nakula matunda pori tu nikawa nimesikia joto katika kuzunguka zunguka nilitokea sehemu kuna maji mengi kama ziwa na lile joto nililokuwa nalo nikasema ngoja nivue nguo nioge nikavua ila roho ikasita kuoga nikavaa nikaondoka nikajikuta sijui njia ya kunirudisha nyumbani na kigiza kinaingia Mungu saidia kuna mzee mmoja wa kijiji cha pili alikuwa anachunga ng'ombe akaniaona na anawajua pale home ndio kunirudisha nyumbani ajab mama hakunichapa na alikuwa ameshanitafuta kwa washikaji wangu wote hakunipata hivyo baada ya kuniona kwanza nimepauka nilipewa tu maji ya moto kuoga na kula nikashida nikaenda kulala sasa cha ajabu asubuhi ambayo ilikuwa j2 nikawasimulia sehemu nilipoona lile ziwa la maji ile sehemu hakuna historia ya kuwa ziwa la maji hata bwawa kuna miti ya Milumba na mitundu kwa wingi kama unaijua, wazee nao ikabidi waanze kuhangaika ndio mambo kutulia ila hii dunia ina mambo sana ukijiona mzima unalala vizuri unaamka salama hakuna wenge lolote mshukuru sana Mungu mie wazazi walikuwa watu wa dini sana walikuwa hawaamini uchawi ila waliamini
Sent using Jamii Forums mobile app