Mimi kuna kisa kilinitokea nilikua kama darasa la 5. Wazee wameenda kulala na mimi nilikua na chumba changu tofauti na madogo zangu nikaenda zangu kulala,nakumbuka mlango nilifunga vizur kabisa dogo nikajipigia zangu mbonji usingizi mwororo! Asubuh kuamka LAHULA LAKWATA pembeni ya kitanda kwa chini kuna kimba moja la kinyesi,kuangalia mlango umefungwa vilevile,na udogo wangu nikaanza kutetemeka nikaenda kuwaamsha wazee,mshua kuja pale akacheka akasema hamna lolote huyu kashindwa akayamwagia majivu picha likaisha hivyo.
lakin ile nyumba ikifika mida ya saa mbili usiku kuna vitu vinatembea juu ya bati afu kama vinateleza af unasikia kishindo kama vimedondoka mkienda mliposikia kishindo hamna kitu.
Nakumbuka nilishawah kumwamsha dogo saa 9 usiku nikidhan kumepambazuka twende shule tukawah namba,fresh tumejiandaa tukaenda kuwaaga wazee tukaanza safari,hapa ndo hua naamin mungu yupo maana baada ya kufika mtaani maana inabdi tukatze mtaani afu tuvuke eneo la makaburi ndo tufike shule,ila ule utulivu wa mtaani nikamwambia dogo turudi home hii sio kawaida kama tukichelewa leo namba basi,tukarudi zetu home na kuingia vyumbani kwetu bila kuwataarifu wazee,kumbe huku room kwa wazee bi mkubwa akashtuka akasema hawa wametuaga wanaenda shule kwan saa ngapi?kuangalia muda ni saa 9 na dakika kadhaa ebana ee dingi alikurupuka na pensi flan ya kulalia kifua wazi akaelekea shule kutufata,kufika pale anaita mlinzi haonekani ikabdi arudi huku anasema kesho nasafiri naenda nyumbani naona watu hatuheshimiani,bi mkubwa akasema hebu tuwaangalie vyumbani mwao,kuja kuangalia bi mkubwa akasema SI HAWA HAPA!!
Wale mabibi jirani ***** zao lakin walikuja kuuelewa mziki