Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Kuna nyumba moja tulikuwa wapangaji 6,kuna kipindi ikifika usiku nasikia sauti za watu na mapaka juu ya Dari na kwenye korido, kelele zao zilikua zinadumu kwa dkk kama 15 hivi.Kiukweli nilikua nahisi moyo unatoka maana mapigo ya.moyo yalikua yanapiga kwa nguvu mno sababu ya woga. Asubuhi namuuliza mama na ndugu wengine kama walisikia chochote wanasema hapana. Siku moja nilikua naumwa sana tumbo usiku.

Mida ile ile ya kelele za paka na wale watu zikaanza walipomaliza Sasa kwa upande niliolalia likaanguka lipaka lina rangi nyeusi na nyeupe maana kulikua na dari lkn sijui ilikuaje likabomoka. Kikuweli sikulala tena usiku ule na hata lilipotoka pale chumbani hakuna anaejua.

Basi usike mwingine tukalala lkn hakukua na zile kelele sikuzisikia lkn sasa kulipokucha yule paka tukakuta kafa nje. Lkn hadi leo najiuliza iweje zile heka heka za usiku za watu wale na paka nisikie mimi tu[emoji848][emoji848][emoji848]!!!
 
Kuna nyumba moja tulikuwa wapangaji 6,kuna kipindi ikifika usiku nasikia sauti za watu na mapaka juu ya Dari na kwenye korido, kelele zao zilikua zinadumu kwa dkk kama 15 hivi.Kiukweli nilikua nahisi moyo unatoka maana mapigo ya.moyo yalikua yanapiga kwa nguvu mno sababu ya woga. Asubuhi namuuliza mama na ndugu wengine kama walisikia chochote wanasema hapana. Siku moja nilikua naumwa sana tumbo usiku. Mida ile ile ya kelele za paka na wale watu zikaanza walipomaliza Sasa kwa upande niliolalia likaanguka lipaka lina rangi nyeusi na nyeupe maana kulikua na dari lkn sijui ilikuaje likabomoka. Kikuweli sikulala tena usiku ule na hata lilipotoka pale chumbani hakuna anaejua. Basi usike mwingine tukalala lkn hakukua na zile kelele sikuzisikia lkn sasa kulipokucha yule paka tukakuta kafa nje. Lkn hadi leo najiuliza iweje zile heka heka za usiku za watu wale na paka nisikie mimi tu[emoji848][emoji848][emoji848]!!!
ilikua ni uoga tu huo
 
Siku moja nilikua nimeenda kijij flan hiv kwenda kuangalia fursa nilikua ni mgen kabisa huko sikuwahi kufka ila niliskia tu story kuwa kwenye vijiji vya maeneo Yale mazao yalikua yanakubal Sana,,,

Nilizunguka sana baada ya muda mref katka Hali isiyo ya kawiada niligundua kuwa nimeingia ndan ndan Sana ya vijiji vile na sikua nakumbuka tena njia ya kurudi na mida ilikua ni jion sikuon nyumba hata 1 wala hata mtu mmoja zaid ya mitimiti mingi tu.. , nilipata hofu sana bahat nzur nikakutana na mzee mmoja nilimsalimia lakin hakujibu wala kusimama , ilibid nigeuze nimuombe sana mzee wangu samahan sana mm nimepotea na sijui ni njia ipi ya kutokea ndan ya mapori haya.

Mzee alisimama akageuka akaniangalia kwa macho ya umakini kidogo, Kisha akanionyeshea ishara kuwa nimfate bila kuongea chochote,,, nikaanza kumfata nilitembea sana kama nusu saa hiv kwa mbal nikaanza kuona nyumba flan ya udongo mbele yetu, nilipofika tu kwake alinipa maji bila kuniongelesha akanipa ishara kuwa kunywa,,, niliogopa kimoyomoyo nikasema ni nini tena hik mbona mambo ya kushangaza na wala sijamuomba maji mm? Alivyoona sitak kutii sharti lake la kunywa maji akaninyang'anya kikombe alafa kanonyesha ishara ya kunifukuza kwa kidole...

Nilitaka kuondoka lakn nikagundua sina ujanja wa kutoka tena maeneo yale nilikia nimeshaingida ndan zaid,, nilipata ujasir nikamgeukia yule mzee nikamuomba maji kwa ishara akanipa nikanywa,, baada ya kunywa tu mzee akaniita kijana, nilishtuka nikamwambia mi nilijua ww Ni bubu kumbe unaongea mzee wangu? Alitabasam Kisha akaniambia mm siyo bubu ila huk maeneo haya tumekua tukikutana sana na viumbe vsivyo vya kawaida wakijidai wanaomba msaada wakikusemesha tu ukaitika unaweza ukapotea jumla,,, niliogopa sana,, lakin akanishika bega akaniambia usiogope kijana nimekutambua ww ni binadam wa kawaida baada ya kukubal kunywa maji Yale niliyokupa angekua ni kiumbe kisicho cha kawaida asingeweza hata kumeza fundo moja.

ilikua ni majira jua linaishia ishia kuzama, nikamwambia mzee wangu chonde chonde naomba unipe msaada niwez kutoka maeneo haya,,, akaniambia kwa sasa umeshachelewa na mida hii siyo mizuri kutembea wewe lala hapa subir kesho nitakusindikiza ,, dah hofu iliizid kuongezeka ila sikua na namna ilibid nikubal..nililala pale lakkn sikupata usingz usik ule nikihofia pengne kile kinywaji nilichokunywa siyo maji ya kawaida yanaweza kunidhuru,,, usik yule mzee alitoka nje na kibuyu chake baada ya kurud ndan akawa kama anakunywa yale maji na anatema kwwnye kona za kitanda cha ngozi alichokua amenipa nikawa namuangalia huku nimelala pale.. niliogopa sana..
Nitaendelea


Duh mkuu kijiji cha wapi hicho na mwaka gani?
 
Ukitaka kufatilia mambo ya kutisha iandae akili yako na mwili vinginevyo unaweza data kabisa,

Nikiwa kijijini nyumbani nasoma shule ya msingi nilikuwa mkorofi sana na jeuri siku moja rafiki yangu wa kike alinunuliwa Baiskel zile za gia na baba yake akatoka nayo kwao mjini hadi nyumbani kijijini basi mm na ukorofi wangu nikachukua ile baiskel nikaiendesha njia zote za kijijini zile nzuri nawavimbia watu kwamba nina chombo yenye gia nne ilipofika saa 12 jioni nikarudi home,nikapaki na rafiki yangu alinambia analala ataondoka kesho yake.

Ratiba yangu lazima nisafishe uwanja jioni ili nikiamka asubuhi uwanja msafi naamkia shambani laah kabla ya usafi nikachukua baiskeli nikaiweka ndani nikafunga chumba na kufuli kubwa la store then nikasafisha uwanja kilichofata ni kulala hapo ndio tatizo lilianza usiku nilishtuka usingizini nikasikia kelele nje ila sasa kelele ni kama mtu anaendesha baiskeli mwanzo nilijua mwizi ila nikatulia kidogo ndipo nilipogundua mchana nilifanya kosa kuwalingia watu na kile ki baiskeli usiku ule kama masaa matano baiskeli ile iliendeshwa kuzunguka nyumba mpaka nikachoka kusikiliza sauti nilipomwamsha kaka asikilize zile sauti ajabu hasikii kitu, nikijaribu kuwasha kibatari unatokea upepo unazima mpaka nikachoka nikaaamua kulala tu asubuhi nilikuta mistari ya baiskeli mji mzima kufungua store baiskeli ipo vilevile niliogopa hata kuigusa
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] walikokomesha mwana
 
Binafsi hizi habari nazisikia tu, machache sana nimejionea lakini hayana tafsiri ya moja kwa moja na ushirikina

Tabora, miaka flani niliishi, stori nyingi sana za majini lakini sikuwahi kushuhudia.
Then tulihamia mkoa mwingine kanda ya ziwa. Nyumba tuliyohamia asubuhi mama anasimulia vibweka alivyosikia usiku. Mara asikie mchanga umemwagwa batini lakini hasikii unatiririka kumwagika chini (unakua kama umeganda), mara mapaka, mara watu wanakimbizana darini etc

Then nikiwa chuo,mwaka wa mwisho tunakaa hostel (mabibo) mshkaji wangu tumebebana akawa analalamika kama wiki nzima akilala znamuona mtu anamkaba kooni, anajaribu kufurukuta au kupiga kelele lakini anakosa nguvu, hadi mwishoni jamaa akiondoka ndo anashtuka, ananiambia mimi lakini nampuuza...

Baadayenikapata kazi, ,miaka ya 2010s nikapelekwa mkoa flan unasifika kidogo kwa ushirikina. Bosi wangu akanipangia kituo cha nje ya mji kidogo, naripoti namkuta jamaa mwenzangu na mlinzi. Hiyo ni siku ya kwanza. Huyu usiku akatupigisha sana stori za wachawi na miujiza anayoshuhudia usiku hapo. Ilikua usiku, nilipochoka zile stori nikaaga nikalale. Napanda kitandani tu, hata dakika kumi hazijapita namuona yule mlinzi HUYOO, kanikalia tumboni akanikaba kooni, nikajaribu kufurukuta au kupiga kelele WAPII! Tukio likadumu kama dakika tano mlinzi akatoweka, ndo nikakurupuka. Niliwaza sana kuhusu yule mlinzi. Siku za mbele nikaambiwa yule mlinzi ni mganga na mshirikina. Nikamkumbuka rafiki yangu niliyekuwa nanpuuza na tukio lililonitokewa, nikasikitika kwanini nilikuwa nampuuza

Kwasasa sijaona tukio la ajabu, na ninatembea sana usiku tena maeneo yanayosemekana ni hatari lakini siogopi wala sioni kitu kibaya, tena ninajenga hisia labda USHIRIKINA ULIKUWA ZAMANI, miaka hii umekuwepo kidogo sana, MAY BE!

Kuna rafiki yangu ALIOKOKA, siku moja alinipa somo akaniambia, mambo ya ushirikina na uchawi huwakuta zaidi watu wanaoyaamini, WAKICHANJWA CHALE au KWENDA KWA WAGANGA. wanakuwa kama wametiwa SIGNAL ambazo wachawi wanaziona hivyo kuanza kuwafuata. Kama SIMU INAVYOPATA SIGNAL ZA NETWEK ya mtandao flan.Hata kazini nawaona wenzangu mara wamepakwa marangi, machale n.k nawashangaa tu maana sioni cha zaidi wanachopata wala mimi kuumizwa nao. EVERYTHING JUST NORMAL.
uyo mlinzi hakuzngunza tena boss
 
Nimejaribu kila njia ya kukutana na haya mambo lakini wapi
Nikisikia huyu bibi mchawi au huyu mzee ni mshirikina mimi kazi yangu ni kuwauliza tu hivi mnapata faida gani kuroga?
Yote hiyo natafuta huo wanga
Sina woga labda ndio sababu nao wananipuuza
Nikaona isiwe shida nikawa naenda kukaa makaburini manane ya usiku maana nikuambiwa ndio mda wa wawangaji kuwanga
Napo sikuambulia kitu zaidi ya mara mbili jamaa kunikimbia huku wanapiga yowe [emoji23][emoji23]
Yaani mpaka haunted house nimeingia sana zaidi ya baadhi ya vyumba kuwa baridi la kufa mtu lakini hakuna kitu cha kunifanya nikimbie
Kuna kizee Fulani waliniambia huwa kanapaa usiku
Nikakauliza naomba lift
Kakasema ya wapi tena nikakaambia kwenye ungo kalisonyaa mpaka kanapotea [emoji23][emoji23]


Sent from my iPhone using Tapatalk
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mungu aliumba vitu vinavyoonekana na visivyoonekana. Na kwa Bahati nzuri akaweka kizuizi kwa kupitia uwezo wake wa kiungu hili tusiweze kushuhudia viumbe hivyo ambavyo havionekani kwa macho yetu ya kibinadamu isipokua kwa utaalamu flani wa mambo ya kiroho.

Viumbe hivyo vikiwemo , Malaika, Majini , Wachawi pamoja na viumbe vingine vya kutisha sana, ikiwemo wanyama wa ajabu wenye ukubwa wenye kutetemesha na kuogofya kwa wanadamu wa kawaida.

Danieli 7:4 “Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu.”

Danieli 8:3 “Ndipo nikainua macho yangu nikaona, na tazama, mbele ya mto alisimama kondoo mume, mwenye pembe mbili; na pembe zile mbili zilikuwa ndefu; lakini moja ilikuwa ndefu kuliko ya pili, na ile iliyokuwa ndefu zaidi ilizuka mwisho.”

Danieli 8:5 “Nami nilipokuwa nikifikiri, tazama, beberu akatoka upande wa magharibi, juu ya uso wa dunia nzima, bila kuigusa nchi; na beberu yule alikuwa na pembe mashuhuri kati ya macho yake.”

Danieli 7:6 “Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.”

Wengi tukisoma Habari kama hizi za kuona simba mwenye vichwa vinne na miguu kama ya binadamu, beberu mwenye pembe kumi, nyoka mwenye vichwa saba na wanyama wengine wa kutisha, tunajipa moyo na kusema hiyo ni lugha tu ya biblia/ lugha ya picha hakuna viumbe kama hivyo. Ila ukweli ni kuwa viumbe hivyo vipo na vinaishi kwenye ulimwengu mwingine tofauti na huu wetu unaonekana. Na kuna binadamu wenzetu wameshashuhudia kabisa kwa macho yao.

Tuachane na hayo na turudi kwenye maada yetu ya leo . Tuzungumzie kuhusu mikasa ya kutisha ambayo tumewahi kukutana nayo kwenye ulimwengu huu ambayo kwa namna moja au nyingine vimekuacha midomo wazi na kukufanya uwe traumatized.

Ngoja nianze na mikasa / mambo ya kutisha niliyowahi kukutana nayo hapa duniani ambayo mpaka sasa hivi bado najiuliza kama ni viini macho au ni kweli , lakini ukweli unabaki kuwa ni kweli .

1. Jini kuchomoza baharini na kuelea hewani.

Nakumbuka ilikua ni usiku wa manane, nikiwa kwenye harakati za ushikirikina Uko sehem( sipendi kutaja jina). Nikiwa na mganga akiendelea kufanya mambo ya kishirikina baharini, Ambapo alisema anaita kiumbe( jini) hili anitimizie haja zangu . Kwa akili yangu nilijua tu ni danganya toto, hakuna lolote. Baada ya kama dakika 45 za yule mganga kufanya ushirikina wake. Ghafla akatokea mwanamke mrefu tofauti na urefu wetu wa kawaida wa binadamu alikua baharini anaelea tu, miguu haionekani kwa kweli nilikimbia, Bahati nzuri wale wasaidizi wa mganga wakanikamata kunizuia nisikimbie. Uzuri hakua anatisha wala nini, alikua tu ni mwanamke wa kawaida ingawa alikua na urefu usio na kawaida, na alikua kakasirika sana, alikua analalamika tunamuita sana tuna shida gani.....

2. Niliwahi kushuhudia kwa macho yangu , binadamu akiwa nusu mtu , nusu simba, Ana sura ya kutisha sana , mbaya mfano hakuna, ilibaki kidogo tu nizimie.

3. Binadamu mfupi kama stuli, Ana ndevu nyingi mpaka chini na alikua na mguu mmoja tu , na macho yake yanawaka moto.

4. Mzimu wa mtu maarufu ambaye alikufa miaka mingi iliyopita.

Hii ndo mikasa ya kutisha niliyowahi kukutana nayo hapa duniani, ambayo kiukweli mpaka leo inanipa shida sana, na ilichukua miaka kadhaa mpaka kuweza kukubali hii hali mpaka kufikia kuzoea kidogo. Ila hapa duniani kuna viumbe vya ajabu mno, na kama ukitaka kuviona unaweza.

View attachment 1430585



Sent from my iPhone using JamiiForums
ukiwa unajihusisha sana na ushirikina lazima ivo vitu ukutane navyo
 
Siku moja nilikua nimeenda kijij flan hiv kwenda kuangalia fursa nilikua ni mgen kabisa huko sikuwahi kufka ila niliskia tu story kuwa kwenye vijiji vya maeneo Yale mazao yalikua yanakubal Sana,,,

Nilizunguka sana baada ya muda mref katka Hali isiyo ya kawiada niligundua kuwa nimeingia ndan ndan Sana ya vijiji vile na sikua nakumbuka tena njia ya kurudi na mida ilikua ni jion sikuon nyumba hata 1 wala hata mtu mmoja zaid ya mitimiti mingi tu.. , nilipata hofu sana bahat nzur nikakutana na mzee mmoja nilimsalimia lakin hakujibu wala kusimama , ilibid nigeuze nimuombe sana mzee wangu samahan sana mm nimepotea na sijui ni njia ipi ya kutokea ndan ya mapori haya.

Mzee alisimama akageuka akaniangalia kwa macho ya umakini kidogo, Kisha akanionyeshea ishara kuwa nimfate bila kuongea chochote,,, nikaanza kumfata nilitembea sana kama nusu saa hiv kwa mbal nikaanza kuona nyumba flan ya udongo mbele yetu, nilipofika tu kwake alinipa maji bila kuniongelesha akanipa ishara kuwa kunywa,,, niliogopa kimoyomoyo nikasema ni nini tena hik mbona mambo ya kushangaza na wala sijamuomba maji mm? Alivyoona sitak kutii sharti lake la kunywa maji akaninyang'anya kikombe alafa kanonyesha ishara ya kunifukuza kwa kidole...

Nilitaka kuondoka lakn nikagundua sina ujanja wa kutoka tena maeneo yale nilikia nimeshaingida ndan zaid,, nilipata ujasir nikamgeukia yule mzee nikamuomba maji kwa ishara akanipa nikanywa,, baada ya kunywa tu mzee akaniita kijana, nilishtuka nikamwambia mi nilijua ww Ni bubu kumbe unaongea mzee wangu? Alitabasam Kisha akaniambia mm siyo bubu ila huk maeneo haya tumekua tukikutana sana na viumbe vsivyo vya kawaida wakijidai wanaomba msaada wakikusemesha tu ukaitika unaweza ukapotea jumla,,, niliogopa sana,, lakin akanishika bega akaniambia usiogope kijana nimekutambua ww ni binadam wa kawaida baada ya kukubal kunywa maji Yale niliyokupa angekua ni kiumbe kisicho cha kawaida asingeweza hata kumeza fundo moja.

ilikua ni majira jua linaishia ishia kuzama, nikamwambia mzee wangu chonde chonde naomba unipe msaada niwez kutoka maeneo haya,,, akaniambia kwa sasa umeshachelewa na mida hii siyo mizuri kutembea wewe lala hapa subir kesho nitakusindikiza ,, dah hofu iliizid kuongezeka ila sikua na namna ilibid nikubal..nililala pale lakkn sikupata usingz usik ule nikihofia pengne kile kinywaji nilichokunywa siyo maji ya kawaida yanaweza kunidhuru,,, usik yule mzee alitoka nje na kibuyu chake baada ya kurud ndan akawa kama anakunywa yale maji na anatema kwwnye kona za kitanda cha ngozi alichokua amenipa nikawa namuangalia huku nimelala pale.. niliogopa sana..
Nitaendelea
Malizia basi kamanda maana tumesimama hapa hadi miguu inaingia tumboni
 
ulishawahi kumastamurbate halafu ukajikuta mtu kakutia kidole bila kumuona,fikiria tu wewe unamasturbate kumbe kuna mtu unampa utam bila kujijua halafu ile unamaliza unajiona kama una majimaji vile ! acha huo mchezo sio mzuri
Duuuu
 
MAAJABU YA PAKA
Paka ni mnyama mwenye hisia kali sana na pia paka anauwezo mkubwa wa utambuzi, na paka anapo ona roho yoyote katika nyumba kitu cha kwanza cha kufanya hujalibu kuangalia kama roho hiyo ni nzuli au mbaya.

Na akikuta roho hiyo ni mbaya basi hulia kwa mlio wa mshangao na kuonyesha ya kwamba katika nyumba kuna kiumbe ambacho si cha kawaida. Kwa hiyo kuamakini sana na paka wako na uangalie akiwa anaendelea kuzunguka na kubadili rangi yake ya macho basi jua kua kuna jini mbaya kaingia katika nyumba yako unatakiwa ufanye utaratibu wa kumfukuza.

Wakati paka anapoona roho ndani ya nyumba, jambo la kwanza analofanya ni kumfuata kote ili kufahamu nia ya roho zilizo ingia ndani ya nyumba zina maana gani. Ili kuhakikisha kwamba chombo hiki hakitatishi eneo lao, paka hufanya kila jaribio liwezekanalo kulifukuza jini hilo katika makazi yake ya nishati yaani mahali anapo ishi.

Ikiwa njia ya kupiga makelele haitafanya kazi paka hubeba kipengele katika uwanja wake wa nishati yake yaani katika viumbe wake na huiongoza nje ya nyumba na ndipo utaanza kuona paka anagoma kukaa nyumbani.

katika mila zingine, kulikuwa na njia wakati roho mbaya hupanda au kuruka kwenye paka basi walikua wakimuita paka na kumfinya au kumlingishia kitu ili apige kelele jini huyo aondoke.

watu wenye kuwasiliana na roho hua hawaruhusu paka kuingia katika chumba cha ibaada cha kuitia roho,au mahali walipo fugia huyo jini maana akija na akakuta kuna paka jini huyo hatakaa ataondoka.

Kwa hiyo, tunapaswa kuelewa kwamba wakati paka atakua anajipitisha pitisha na kupiga piga au kukugusa gusa miguu yako, si tu kwamba sio kwamba zamila yake anataka tu chakula kutoka kwako bali anaweza kua anakufikishia ujumbe furani, lakini pia inamaanisha kwamba paka inashirikisha uchawi wake na wewe, nguvu ya astral, na wakati mwingine paka anaweza kukuchukia basi ujue ya kwamba kuna uwezekano wa wewe kua na jini mchafu.

Ili kuamini kua paka ana utambuzi wa hali ya juu hebu jalibu kumpa sumu, ndipo utaamini maana hawezi kula hiyo sumu na kijaliwa kuila basi kufa kwake ni kugumu.


Paka sio tu kulinda nyumba kutokana na roho wabaya kuingia ndani ya nyumba, lakini pia analinda nyumba kutokana na nguvu hasi ambayo ilikaa hapo kabla ya paka hata kuja nyumbani. Pia kuna baadhi ya watu walikua wakitaka kuhama nyumba walikua wakimtanguliza paka kwanza kabla hawaja hamia ili iwasaidie kufukiza nguvu hasi za kichawi ambazo huenda zikawa katika nyumba hiyo.

Pia paka akiona mgeni kaja na mgeni huyo ni mchawi basi paka hua hachezi mbali na eneo hilo na huenda akaanza kumparua au kumgusa gusa kwa kutumia mkia wake, hapo anakua anategua uchawi
Kwa kuwa paka ni njia za nishati ya cosmic, zinaweza kuleta nishati nzuri ndani ya nyumba, ambayo itasaidia ustawi na ustawi wa familia nzima.

Warusi walikuwa na ibada ya kuvutia sana: wakati wa kuhamia mahali papya wao kwanza walitanguliza paka ndani ya nyumba. Ikiwa nyumba ilikuwa mzee yaani nyumba ya zamani ambayo ilisha tumika, paka ilikuwa ikivuta nishati zisizo hitajika. Ikiwa nyumba ilikuwa mpya basi pia walikua wakimtanguliza paka ili aingize nishati za kinga na nuru katika nyumba hiyo.


Matumizi makubwa ya nguvu za kichawi za paka hupatikana katika uponyaji na hasa kwa paka mwenye langi nyeupe au alie changanyika madoa meupe na meusi.

Paka mwenye rangi nyeusi tupu hua na nishati za kichawi na mazingaombwe na dawa za giza.

Paka mweusi wachawi humtumia katika dawa za kumpoteza mtu na kumfanya msukule asionekane katika macho ya kawaida.

Paka za uzazi na rangi yoyote zina uwezo wa kutibu na zinaweza kuwatendea mabwana wao bila uwazi, ziko kwenye maeneo yao maumivu. Mojawapo ya mbinu rahisi za matibabu kwa msaada wa paka - rahisi kumpiga, kutolewa watu kutokana na matatizo ya akili na kihisia. Katika paka za uponyaji hutumiwa kuboresha maono pia. Ili kufikia mwisho huu, waganga wengine wanashauriana mchanga paka mweupe.

RANGI ZA PAKA NA KAZI ZAKE.
1. Nyeusi: wivu, nguvu za uchawi, ulinzi, uchawi mwingi! Licha ya tamaa zote, wanyama wa rangi huchukua nishati mbaya huondolewa katika matatizo ya kaya (miji) hutoa hekima na ufahamu.


2. Paka nyekundu (mwekundu): wachawi wa kawaida wa mwezi, wenye nguvu za kiume, nguvu za jua na nguvu ya miujiza hawatakiwi kumuona paka akifanya mapenzi maana wakimuona huwatia mikosi, na malaika au kiumbe anae mmiliki paka huyu wa rangi nyekundu ni kiumbe wa utajili.


3. (paka wa rangi ya kijivu): Paka za rangi hii huleta upendo, furaha, bahati nzuri, pamoja na utulivu wa kihisia na amani ya kimwili na huongeza furaha katika ndoa kama utakua umemfuga paka wa rangi hii.



4. Paka mweupe: paka mweupe wachawi humtumia kuunda uchawi wa mwezi, pia paka mweupe wana nguvu za uponyaji ndo maana katika baadhi ya nchi ukifika kwa mganga au kwa mchungaji utakuta kuna paka mweupe. Paka mweupe huwapa watu hisia za uzuri na kupendeza machoni pa watu, hupunguza matatizo katika familia.

Amerika, inachukuliwa kuwa ni mleta amani katika mji.


5. paka mwenye rangi tatu= nyekundu,kijivu na nyeupe:

Paka mwenye langi hizi kwa Amelika huhesabika kama paka wa kifalme, na paka akizaa paka wa ainahii hupendwa sana.

Pia paka amepewa uwezo mkubwa wa kuona kitu katika giza na mawindo yake mengi huyafanya kwa urahisi kukiwa na giza.
Hahahaha majabula
 
Siku moja night nilikua nina mihadi na demu wangu na tulikua tukihishi jirani, tulikua na mazoea kila usiku demu anachomoka kwao anakuja kulala gheto kwangu Kisha anarudi kwao alfajiri Sana kabla hakuja pambazuka na kulikua na tetesi mtaani kwamba kwao ni wachawi, Ila sikutilia maanani Sana kwakuwa sikuamini hizo issue na tulikua katika misingi ya ukristo.siku ya tukio nilikua na mihadi na bibie na hakutokea kwa wakati inabidi nikaskikizie kulikoni, kipindi hichi simu za mkononi hajifikirika kutolewa, kwahiyo nikaenda kumgongea dirishani kwao,

lakini sikupata response yeyote, nikaenda mlangoni bado ilikua kimya, nikarudi dirishani kwake nikawa nahita kwa kwa sauti ya chini Sana , baada nisikia mlango unafunguliwa taratibu, nikajua ndie anatoka, fasta nikawahi mlangoni kumtoa bibie, kitu nilichokutana nacho sitoweza kusahau mpaka leo, lilitoka jitu Lina manyoya, minywele na kucha ndefu Sana...nilikutana nae hana kwa hana nilikimbia, nikajikuta home nikihema na mapigo ya Moyo yakienda Kasi snaa.

Toka siku hiyo uhusiano ukafa, nikaamini uchawi na mazingira yapo.
 
Siku moja night nilikua nina mihadi na demu wangu na tulikua tukihishi jirani, tulikua na mazoea kila usiku demu anachomoka kwao anakuja kulala gheto kwangu Kisha anarudi kwao alfajiri Sana kabla hakuja pambazuka na kulikua na tetesi mtaani kwamba kwao ni wachawi, Ila sikutilia maanani Sana kwakuwa sikuamini hizo issue na tulikua katika misingi ya ukristo.siku ya tukio nilikua na mihadi na bibie na hakutokea kwa wakati inabidi nikaskikizie kulikoni, kipindi hichi simu za mkononi hajifikirika kutolewa, kwahiyo nikaenda kumgongea dirishani kwao, lakini sikupata response yeyote, nikaenda mlangoni bado ilikua kimya, nikarudi dirishani kwake nikawa nahita kwa kwa sauti ya chini Sana , baada nisikia mlango unafunguliwa taratibu, nikajua ndie anatoka, fasta nikawahi mlangoni kumtoa bibie, kitu nilichokutana nacho sitoweza kusahau mpaka leo, lilitoka jitu Lina manyoya, minywele na kucha ndefu Sana...nilikutana nae hana kwa hana nilikimbia, nikajikuta home nikihema na mapigo ya Moyo yakienda Kasi snaa..Toka siku hiyo uhusiano ukafa, nikaamini uchawi na mazingira yapo.
msukule uo
 
Siku moja night nilikua nina mihadi na demu wangu na tulikua tukihishi jirani, tulikua na mazoea kila usiku demu anachomoka kwao anakuja kulala gheto kwangu Kisha anarudi kwao alfajiri Sana kabla hakuja pambazuka na kulikua na tetesi mtaani kwamba kwao ni wachawi, Ila sikutilia maanani Sana kwakuwa sikuamini hizo issue na tulikua katika misingi ya ukristo.siku ya tukio nilikua na mihadi na bibie na hakutokea kwa wakati inabidi nikaskikizie kulikoni, kipindi hichi simu za mkononi hajifikirika kutolewa, kwahiyo nikaenda kumgongea dirishani kwao, lakini sikupata response yeyote, nikaenda mlangoni bado ilikua kimya, nikarudi dirishani kwake nikawa nahita kwa kwa sauti ya chini Sana , baada nisikia mlango unafunguliwa taratibu, nikajua ndie anatoka, fasta nikawahi mlangoni kumtoa bibie, kitu nilichokutana nacho sitoweza kusahau mpaka leo, lilitoka jitu Lina manyoya, minywele na kucha ndefu Sana...nilikutana nae hana kwa hana nilikimbia, nikajikuta home nikihema na mapigo ya Moyo yakienda Kasi snaa..Toka siku hiyo uhusiano ukafa, nikaamini uchawi na mazingira yapo.
Hahaha nyege zilikucost mbio ambazo hukutarajia.
 
Nimesoma na utu uzima mitihani ulikuwa imekaribia Sana. Vitabu ilikuwa nimeviweka sebuleni kwenye meza , nikawa nasomea chumbani nikisoma sirudishi sebuleni navipanga pale chumbani upande WA pili WA kitanda pako wazi kabisa hakuna chochote.

Vikawa vingi. Siku moja nilipiga msuli Hadi saa 8 nikazima taa Niko kwenye Neti nikasikia binge la kishindo vile vitabu vinaanguka nikasema Kwa sauti 'Da vimeanguka siamki nitaviokota asubuhi'. Asubuhi naamka nakuta viko vile vile na ilikuwa ni mivolome ya hatari. Nilikuwa peke yangu. Nilichoka ,Kesho yake Nililala mapema kihede chote kiliisha.
 
Dah imenikumbusha miaka ya 90s nikiwa Tabora wilaya moja hivi kijijini nikichukua elimu ya msingi shule yetu ilikuwa upande wa magharibi kuna makaburi halafu shule ina miti kibao ya mikaratusi,mikorosho mijohoro mizambarawe na miti fulani hivi inatoa ubani upepo ukipiga inavuma kama gari,

Dah nakumbuka hiyo siku niliamka kwenye kigheto changu pale home kama saa nane hivi mabalamwezi imekubali nje maana ilikuwa wiki ya mwalimu mmoja hivi kusimamia usafi na wechelewaji na ukichelewa unapata bakora za miguuni na lile baridi la kijijini balaa mwanaume mbalamwezi ile nikajua kumekucha nikanawa faster faster hata sikuwastua wazazi ambapo sio kawaida huwa lazima niwaamshe kwenye gheto lao mzee nikanyanyua ufagio mkononi na kidumu cha maji mbio kwenda kabla ya kufika shule kuna kipori fulani lazima ukipite ndio ufike shule mwanaume sikujari japo njiani sikuona mtu yeyote hiyo haikunistua mie nilijona mshindi leo nawahi namba shule,

aisee nimepita chini ya mikorosho na hiyo miti mingine bila kujari nahisi akili haikuwa yangu nakumbuka nafika shule nikakimbilia darasani nafika mlangoni nilichokishuhudia acha niliona moto mkubwa unawaka mule na kuna watu wamekaa kama wako kwenye kikao halafu wote wakaniangalia ila sura sikuziona hapo ndio akili ikarudi kwamba nimezingua niligeuka mbio kurudi home halafu ule upande wa makaburi nilishuhudia watu wakiwa na mguu mmoja wanaruka ruka kwa mstari mbio zangu nilikuwa nahisi kuna kitu nyuma kinanifata kugeuka nyuma niliona mtu mrefu sana kichwa hakionekani ila kavaa vazi refu linag'aa kama mbaramwezi ilivyokuwa inag'aa mwanaume niliongeza speed nilienda nikaingia na mlango mpk ndani yule jini sijui nini nilipokaribia nyumbani nilisikia msonyoo mmoja hatari sana wazazi wakaamka kufungua mlango kuja kunikuta sijitambui wakanichukua nikaenda kulala kwao asubuhi ndio kuwaelezea ni moja ya tukio ambalo huwa sipendi kabisa kulikumbuka maana baada ya hapo mpk leo kuna vitu huwa naviona ambavyo sio vya kawaida na niliwasumbua sana wazazi baada ya hapo . nimejaribu kufupisha ila kuna mambo mengi sana kwa ule usiku na miaka ile niliyashuhudia baada ya ilo tukio.
Ungwasalimia uwaombe na hela saa hizi ungekua billionaire, hawanaga roho mbaya wale jamaa
 
Nimesoma na utu uzima mitihani ulikuwa imekaribia Sana. Vitabu ilikuwa nimeviweka sebuleni kwenye meza , nikawa nasomea chumbani nikisoma sirudishi sebuleni navipanga pale chumbani upande WA pili WA kitanda pako wazi kabisa hakuna chochote. Vikawa vingi. Siku moja nilipiga msuli Hadi saa 8 nikazima taa Niko kwenye Neti nikasikia binge la kishindo vile vitabu vinaanguka nikasema Kwa sauti 'Da vimeanguka siamki nitaviokota asubuhi'. Asubuhi naamka nakuta viko vile vile na ilikuwa ni mivolome ya hatari. Nilikuwa peke yangu. Nilichoka ,Kesho yake Nililala mapema kihede chote kiliisha.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom