Njoo utoe mbinu za kumsaidia mtoto awahi kuacha kujisaidia haja kubwa/kujikojolea

Njoo utoe mbinu za kumsaidia mtoto awahi kuacha kujisaidia haja kubwa/kujikojolea

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
9,514
Reaction score
23,523
Inasemekana mtoto kumvalisha pampasi muda mwingi ni kufanya zuzu alijitambue mapema hasa katika kitengo cha kujinyea na kujikojolea.

Ushauri ufanyeje:

1: Mnunulie vijaptula vingi (wa kiume) akiwa anajikojolea au anajinyea ilekero itamfanya kisaikolojia aanze kujipanga. Ukimsafisha mvalishe tena kengine.

2: Mshtukize Mara kwa Mara usiku au Mchana na kumforce akojoe au ajisaidie.

3: Mlazimishe mara kwa mara azoee poti. Kuna dogo alikuwa halipendi kabisa ila sasa hivi analitafuta mwenyewe unamkuta amekaa anashusha gogo.

4: Muache ajichanganye na wenzake aliona wanvyokojoa na yeye ataiga.

Note: Hapa inazungumzia chini ya miaka 2.5

Wale watoto wanaojitambua lkn bado wanakojoa.
1: Wasinywe majimaji usiku.
2: Kafimbo Mara moja moja Akili ichangamke.
3: Kuna njia za jadi kama kindumbwendumbwe.
4: Mnyweshe Maji ya Mchele (myth).

Hebu toa ujuzi zaidi kuwasaidia hawa madogo
 
Wale watoto wanaojitambua lkn bado wanakojoa.
hawa aina aja ya bakora sijui fimboo au kindumbwendumbwe. wanaachaga wenyewe tu kwa wakati
shule nilikua na mtu form 3 analiachia kojo kila siku, alafu alikua mmoja kati ya wanaofaulu vizuri darasani.
kama anajielewea basi anajua hali inavyomtesa aina haja ya kumsemasema au kumshushia mboko. unamsaidia kisaikolojia tu
 
Mie baada ya kuchoka na hekaheka hizo nilikuwa namtisha na kafimbo kadogo kwamba ukikojoa au kujinyea mii chapa, baada ya dk mbili anasahau anaachia vitu, Mama yangu akaniambia muda bado utashangaa atasema mwenyewe muda ukifika . Kuna siku nilimkuta anamfukuza kuku na fimbo kumuuliza akanibu ' chapa anyea'.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom