Njooni tusemezane. Sheria gani inakataza watu kuchangishana? Waziri Mkuu yupo sahihi kumkamata Niffer?

1. Kukitokea maafa/janga la kitaifa, usichangishe fedha. Sheria ya usimamizi wa maafa ya mwaka 2022, kifungu cha 26(2) inasema jukumu la kuchangisha litafanywa na Kamati ya maafa iliyo chini ya ofisi ya Waziri mkuu, kupitia akaunti maalumu.

2. Ukichangisha fedha kwa matatizo mengine ambayo si maafa (eg matibabu, elimu, yatima) usitumie namba/akaunti binafsi. Ni kosa kisheria. Tumia taasisi (NGO) iliyosajiliwa.

Kwa mujibu wa Sheria ya NGO namba 24 ya mwaka 2002, kifungu cha 32, michango ya kibinadamu (charitable initiatives) inaratibiwa na mashirika yaliyosajiliwa na sio mtu binafsi. Lengo la sheria ni kuweka "Check & Balance" ili kudhibiti ubadhirifu kwa sababu NGO inafanyiwa auditing angalau mara 2 kwa mwaka (internal & external).

3. Kama unataka kumsaidia mtu na huna NGO, tumia namba za mhusika mwenyewe, lakini kwanza upate kibali kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya. Kifungu cha 122 cha sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 inataka michango inayokusanywa na mtu binafsi kwa ajili ya "charity" ipate kibali kwa DC.

#Swali: Je watu wanafahamu haya?

#Jibu: Hapana. Kuna watu wanachangisha pesa kwa nia njema kabisa (utmost good faith) lakini hawajui utaratibu wa kisheria ulivyo.

#Swali: Je nini kifanyike?

#Jibu: Wapewe elimu. Hawapaswi kutishwa, kubezwa au kukatishwa tamaa. Kama mtu amechangisha fedha kupitia akaunti yake binafsi ili aokoe maisha ya mgonjwa kwanini umshtaki? Ni kweli hajafuata utaratibu lakini kafanya jambo jema. Kwahiyo kunaweza kuwa na "actus reus" lakini kusiwe na "mens rea" na hivyo ikawa ngumu kuestablish jinai.

#Points3ZaKukariri;
1. Michango ya maafa/majanga inakusanywa na serikali tu.

2. ⁠Michango ya "charity" inakusanywa na taasisi/NGO iliyosajiliwa na inayowasilisha auditing report wizarani.

3. ⁠Ukitaka kuchangisha na huna NGO tumia namba/akauti za mhitaji mwenyewe kwa kibali cha DC.

#UshauriKwaSerikali: Watanzania wanapendana sana, lakini wengi hawana imani na serikali kuhusu michango. Wanakumbuka kuchangia wahanga Kagera pesa zikabadilishwa matumizi. Kwahiyo tumieni watu wenye ushawishi kuhamasisha (eg wasanii, viongozi wa dini, wanamichezo, wanahabari etc).!

copy and pasted kutoka kwa ukurasa wa instagram wa Malisa GJ
 
Maafa unayatafsirije
 
Nenda Central kamuwekee dhamana. Huu mjadala hautamsaidia
 
Acha basi mkuu, unataka kusemaje, kwamba hizo familia za waathirika zitatoshelezwa kimahitaji na serikali? Halafu unatofautishaje kuwa hili ni tatizo binafsi na hili sio, familia x iliyofiwa na mtu kwenye jengo kariakoo hilo kwao ni tatizo binafsi ama la kitaifa? Unataka kusemaje ?
 
Sitamsahau Diblo siku alipotupiga kamba kwamba yule mwamba yuko Ikulu anachapa kazi kumbe baba wa watu yuko kwenye friji nafsi yake isharejea kwa Muumba wake....

Dibloh nyoko sana wallah....
 
Sitamsahau Diblo siku alipotupiga kamba kwamba yule mwamba yuko Ikulu anachapa kazi kumbe baba wa watu yuko kwenye friji nafsi yake isharejea kwa Muumba wake....

Dibloh nyoko sana wallah....
Alienda Ruangwa kuzindua gereza badala ya hospitali.

Diblooo
 
Kuchangishana msibani ni mbaya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…