Nkasi: Peter Lijualikali amdaka Mwalimu aliyemuoa Mwanafunzi na kuishi nae Nyumba za Shule

Nkasi: Peter Lijualikali amdaka Mwalimu aliyemuoa Mwanafunzi na kuishi nae Nyumba za Shule

Action and Reaction

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2021
Posts
1,438
Reaction score
1,496
Mwalimu wa Shule ya Msingi Itete kata ya Kirando Wilayani Nkasi, Clarence Mwanakurya (29) amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kumuoa Mwanafunzi wa kidato cha kwanza Jesca Mwanji (16) tangu mwaka jana na kuishi nae katika majengo ya Serikali yaliyopo katika Shule ya Msingi Itete anaposoma Mwanafunzi huyo.

We ticha unakuraa watoto wa Mama..... Zingatia maadili ya kazi

====

MWALIMU wa Shule ya Msingi Itete kata ya Kirando Wilayani Nkasi, Clarence Mwanakurya (29) amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kumuoa Mwanafunzi wa kidato cha kwanza Jesca Mwanji (20) tangu mwaka jana na kuishi nae katika majengo ya Serikali yaliyopo katika Shule ya Msingi Itete anaposoma Mwanafunzi huyo.

Haya yamebainika baada ya Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijuakali kuanza oparesheni ya kuzuia na kupambana na mimba za utotoni ambapo amewataka Walimu wa Msingi na Sekondari kuziheshimu sketi za shule kwani zitawaletea matatizo katika kazi zao na maisha kwa ujumla, oparesheni hiyo imeanza tarehe 01.11.2021 itaendelea mpaka wabainike waliowaachisha Shule Wanafunzi na kuwaoa.

Sambamba na tukio hilo, pia Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo naye amekamatwa pamoja na Clarence, sababu ya Mwalimu Mkuu kukamatwa ni kukaa kwake kimya na kuruhusu Clarence kuishi kuishi na Mwanafunzi huyo.
 
Mwalimu wa Shule ya Msingi Itete kata ya Kirando Wilayani Nkasi, Clarence Mwanakurya (29) amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kumuoa Mwanafunzi wa kidato cha kwanza Jesca Mwanji (16) tangu mwaka jana na kuishi nae katika majengo ya Serikali yaliyopo katika Shule ya Msingi Itete anaposoma Mwanafunzi huyo.
Mwambieni hizi kiki zitamuangusha mapema. Unatoka ofisini kwenda kusaka waliooa wanafunzi kama unavyosaka wapika gongo. Kajiunganisha kwenye kazi ya Polisi halafu kaigeuza kuwa operesheni ya Mkuu wa Wilaya?

Akueleze baada ya hapo walimkamata Nani tena?
 
Si chadema walisema Lijualikali amekwisha baada ya Magufuli kufa?

Kumbe ni mkuu wa wilaya
 
Wanawake wamejaa tele mitaani, sheria anazijua halafu anaamua kumueka mtoto kinyumba kabisa!?

Afungwe tuu hata miaka60 ikiwezekana ile iwe fundisho kwake na wenzake wenye tabia hiyo
 
Leta picha ya DC apongezwe

Huyo mwenye tabasamu zito aliyevaa tshirt mistari ya red, blue, white na black aliyevaa miwani
images (10).jpeg
 
Wanawake wamejaa tele mitaani, sheria anazijua halafu anaamua kumueka mtoto kinyumba kabisa!?

Afungwe tuu hata miaka60 ikiwezekana ile iwe fundisho kwake na wenzake wenye tabia hiyo
Tuangalie wapi tumejikwaa sio tulikodondokea!tuna adhabu ya 30yrs jela kuhusu ubakaji,je sheria hii imeondoa au kupunguza tatizo?tuna death sentence ndani ya sheria zetu ,je adhabu hii imeleta tija?,adhabu ya kifo ni barbaric LAZIMA tuifute pamoja na zingine,elimu kwa wote hasa mtoto wa kike na kiume kujitambua ndio muhimu hapa.
 
Acheni kurubuni watoto kwa kisingizio cha kuangalia mlikodondokea

Yaani wanawake wooote mtaani hutosheki hadi ukamrubuni mtoto asiye na uwezo wa kuchambua mambo?

Kama unadhani hiyo adhabu haina tija na wewe tafuta mwanafunzi umuweke kinyumba.

Kuna mambo yanaudhi ila hili la kirubuni watoto linauchi mnooooo.... Fungweni tuu kwa kweli
 
Mwalimu wa Shule ya Msingi Itete kata ya Kirando Wilayani Nkasi, Clarence Mwanakurya (29) amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kumuoa Mwanafunzi wa kidato cha kwanza Jesca Mwanji (16) tangu mwaka jana na kuishi nae katika majengo ya Serikali yaliyopo katika Shule ya Msingi Itete
Hizi nafasi za Ukuu wa Wilaya hazina maana kabisa,hiyo kazi ya kukamata ingeweza kufanywa na Mkuu wa kituo tena akishirikiana na Balozi wa nyumba kumi.
 
Hizi nafasi za Ukuu wa Wilaya hazina maana kabisa,hiyo kazi ya kukamata ingeweza kufanywa na Mkuu wa kituo tena akishirikiana na Balozi wa nyumba kumi.
Tutajuaje Lijualikali anafanya kazi? Lazima mavitu kama haya yamkuze!

Kukaa Namanyere ukasikike sio mchezo
 
Back
Top Bottom