Kuunga mkono ccm ni sawa na kuunga mkono Shetani
Mkuu
Erythrocyte , kwanza uhalifu ni uhalifu, unaweza kufanywa na mtu yoyote, hivyo tuitenganishe CCM kama chama, na wana CCM watakaofanya uhalifu, wasikichafue chama.
Pili, kwa vile CCM ndio chama tawala nchini Tanzania, na ni Mungu ndie huweka serikali za mataifa, then CCM imewekwa na Mungu, CCM ndio chaguo la Mungu kwa Tanzania.
Kama kuunga mkono ccm ni sawa na kuunga mkono shetani, then ni Mungu ndie ametuchagulia shetani huyu, hivyo inapotokea unakabiliwa na mashetani wawili, au mazimwi wawili , then chagua zimwi linalokujua!.
Hili la ushetani na umalaika, nimeendesha darasa humu angalia tarehe ya bandiko hili
Kwa vile Tanu ndie baba wa CCM, na Tanu ndicho kilichotupatia ukombozi, then like father like son, CCM ni chama cha ukombozi wa Watanzania.
Wengine wetu kama sisi tunakifananisha na mkombozi, muokozi!.
NB. Huku kuendelea kueneza chuki dhidi ya CCM kwa njia ya kuivoke ridicules, its not gonna add up the votes come 2015!, CCM itarudishwa kwa sympathetic votes kuwa ilitukanwa sana!.
Pamoja na CCM kuwa ndie chama mwokozi wetu, bado hajaweza kutufikisha kwenye ile nchi ya ahadi!. Kufuatia hali hii, watu sasa wanaijengea chuki CCM na kuifanya ionekane kama ni li zimwi!. Kwa kuwa hakuna mwingine as of now aliyeonyesha uwezo wa kutufikisha, then 2015, kuna hatari ya kuendelea kulichagua hili hili li zimwi CCM maana ndilo likujualo!
Pasco.
Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019, tuliwapa, na uchaguzi wa leo wa serikali za mitaa, tunakwenda kuwapa tena!.
Twendeni tukapige kura!.
Kizungu wanasema, “in between the two devils, chose the lesser”
Nenda kapige kura, twendeni kupiga kura.
P.