Private investigator
JF-Expert Member
- Dec 28, 2012
- 303
- 287
Ni miezi sasa watumishi wanaotaka kuuza deni kutoka NMB kwenda mabenk mengine wamekuwa wakicheleweshewa balance zao ili tu kusudi wasikope huko kwingine isipokuwa NMB.
Watumishi hawa wana mipango mingi na hiyo mikopo wanayotaka kuichukua, na hivyo wataongeza mzunguko wa pesa mtaani.
Mathalani watu wanataka kujenga, watanunua vifaa, wanataka kununua magati, watalipa kodi na kununua mafuta, wanaotaka kuboresha biashara zao wataajiri na kulipa kodi, wanaotaka kuoa nk. Wapo wanaotaka kuwekeza sehemu mbalimbali.
Shughuli zote hizi zinaleta manufaa kwa uchumi wa nchi. Kwa mbinu hii ambayo yawezekana maafisa mikopo wote NMB wameambiwa ni kuwa wawe wanasingizia mfumo. Ila ukiwa unakopa kwao hakuna tatizo la mfumo, ukiwa unauza deni lao, kuna tatizo la mfumo. Hasa Mwanza branch zote zimeelekezwa hivi.