NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Hawa ndiyo NMB hakuna reply hata Moja Toka kwao.
Wameonesha rangi Yao ni ipi katika kutoa huduma
 
NMB sijawaelewa

hv ni mmepandisha makato kimya kimya kwenye ATM au

nimetoa 190 nimeakatwa 4000 hii imekaaje??
 
Jamani naombeni msaada,Card yangu ya NMB Imefutika Namba, Nifanyeje?

Lakini pia nahitaji kubadilisha Account kutoka kwenye Chapchap hadi kwenye account ambayo ni nzuri Zaid,msaada wenu pls
 
Nataka niwaulize swali hivi ukiingia kwenye ile app ya NMB click ukauliza salio pia kuna makato? Nimefanya kama mara tatu hivi naona 5000 imeondoka
Ndugu yangu huko kila kitu utakacho fanya lazima ukate tena sio kidogo hata huku kwenye menu ya kawaida nilazima ukatwe maana unatakiwa uwe na vocha kwenye simu sio kifurushi hapana ni vocha kama vocha
 

Ndugu wana JamiiForums,
Habari, samahani naomba usaidizi kidogo, nilitaka kufungua account ya NMB CHAP CHAP, kila mtoa huduma anapotaka kutaka kuisave account kwenye system, anaambiwa kuwa mimi tayari nina account ambayo nishaifungua,

Ili hali mimi maisha yangu yote sijawahi fungua account yoyote ya kibank,
Nimetumia kitambulisho cha NIDA imeshindikana, Nimetumia kitambulisho cha mpiga kula nako imeshindikana,

Naomba kufahamu nini tatizo
 
Of course NMB wamepandisha makato , sasa hivi kuna hadi makato ya kila mwezi 2000+
 
Tatizo la NMB kwa nini fedha ikiwekwa kwenye account mnamjulisha mteja lakini ikichukuliwa mnamficha mteja.kuna Siri gani hapo.hilo limewafanya wengi kukimbia wakidai kuna ufisadi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…