NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Mnahujumu uchumi wa nchi kwa kuwacheleweshea watu balance statements hasa wanaotaka kuhamisha deni. Hamtaki watu wawahame huku mkilazimisha indirect wasiuze madeni yenu. Ni failed technique
 
NMB kuna shida gani, kutoa pesa through mobile, atm even dirishani.

Mkasema tuhakikiwe, okay, kuanzia Friday last week nimehakiki dsm mpaka leo I can't get service,

Shida iko wapi
 
NMB mmekuwa wazembe na huduma zenu, msilewe kuwa na wateja wengi,ipo siku mtakuja kujutia.
 
Riba ya mkopo asilimia ngapi? Makato mengineyo ada na bima kiasi gani?
 
Hampokei simu za dharura imekaaje hiyo halafu ukipiga inaita unaambiwa bonyeza moja pindi wahudumu wetu wakiwa free masa'a mawili baadae tutakupigia nako hampigi, acheni ubabaifu nyie. Mnatuzushia madeni tusiyodaiwa, tukihitaji maelezo sim hampokei angalieni nyie mambo hayakwendi hivyo mnavyoyaendesha.
 
Naona mmetuma sms kuwa mmeshusha riba nakuongeza muda wa kukopa, naomba kuuliza riba imeshuka hadi asilimia ngapi?
 
Mlichowai kunifanyia bank ya NMB ni wizi na uhuni sitaki hata kuwasikia mpaka nimehama bank yenu wezi katika account za watu.
 
Mie napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa NMB KAHAMA Business centre kwa huduma bora nilizozipata pale walinipa msaada mkubwa sana @ Pendo and her team [emoji109][emoji1666][emoji1417]
 
NMB hivi ni lini mtakuwa serious angalau kidogo? Miezi zaidi ya miwili nafwatilia swala ambalo kila nikienda bank ni kama ndo nafanya kulifufua na bado ni kiza kinene. Ngoja nipate wakili mzuri wa maswala ya mikataba halafu tutajua kifuatacho.
 
nyie NMB nyie sina hamu na nyie kabisa nlifungua account chap chap baada ya kuambiwa account ya mwanzo imefungiwa sasa namba yangu simu hamjaifuta toka mwezi wa saba mpaka sasa hivi haijafanyiwa chochote na yale mabarua mlionisumbua kuandika
Wazembe sana sana
 
Mmefanya vizuri kampuni za simu pia mnatakiwa mje humu kuna shutuma nyingi sana zinatukera mje na nyie kama hawa NMB walivofanya
Mbona sasa wala hawatujibu tunajiandikia wenyewe hapa weeee wala hawastuki. Yani ukiwa na madai hapa NMB ni useless kabisa.
Mmeniudhi sana sana
 
Kuna wateja wanaibiwa huku mkuje kujibu tuhuma msijikaushe


 
Kesho nakuja kuchomoa mkwanja wangu wooooote kwenye account, yani nipate shida kuitafuta pesa, niiweke kwenu mufanyie mambo yenu bado hamuridhiki tu munanikata, eti niniiiiii tozo?
 
Juzi akaunti yangu ya NMB nilikuwa na tshs 72,000/=kwenda kutoa nakuta tshs54,000/=tu naambiwa ni makato ya kodi,bado sijaelewa hiyo kodi ni %? Kiasi kwamba 70,000/= kodi iwe tsh16,000/=?
Naomba majibu tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…