NMB Tanzania Hongereni sana kwa majukumu. Kwanza nawapa pole kwa CRDB kuwapiku kwa kushika namba 1 kuwa Benki yenye ukwasi Mkubwa kuliko nyie.
Mnapaswa kubadilika sana Vinginevyo NBC na TCB pia watawaaacha mbali sana. Muna maeneo mnakwama sana sana;
1. Wafanyakazi wengi wameanza kufanyakazi kwa mazoea. Kuna taasisi kubwa na Mashirika ya Serikali ambayo mpaka sasa NMB mmeshindwa kupeleka MOU za kukopesha watumishi wake na hivyo mnakosesha benki mapato. Kuna Taasisi MOU ina miezi 8 imesainiwa lkn waliopeleka hawajaenda kuichukua. Hatua hii siyo tu kwamba mnakosa wateja wa kukopesha bali pia watumishi wanakosa kupishia posho na mishahara kwa benki yenu kwani wakienda kukopa kwingine hulazimika kuwahama ili kukidhi vigezo vya huko wanapopewa mikopo.
2. Uhaba wa ATM mashine kwenye Wilayani na Majiji makubwa. Hapa sitaki kuongea lkn mnatia aibu sana maeneo mengi huko Mikoani ATM ziko chache na unazitafuta kwa tochi.
3. SIKU ZA WKEND ATM zenu hazina pesa au Network hakuna. Hiii imekuwa kero sana sana sana usiombe iwe wkend ya mwisho wa Mwezi utajuta pesa yako kuwepo NMB utakuta foleni ndeeeefu watu wakitukana na kulalamika kisa pesa hakuna. Hili tatizo limekuwa suguuu na watu wamehama benki yenu kwa ujinga huuu.
Msidharau hiii, kizazi kijacho kinapopita kwenye ATM kinaona huu ujinga kikifika umri wa kuwa na akaunti they will opt other BANKS not NMB kwa ajili ya kuepuka madudu ya sasa.
4. HUJUMA... Hii benki ya walalahoi tangu kuja kwa huduma ya NMB Wakala Kuna harufu ya Hujuma ili mawakala wafanyekazi. Hawa mawakala wenye hii michezo wamejiegesha karibu na ATM nyingi tuuuu. Kinachofanyika ATM muda wooote hazina pesa na ukifika Easy tu mlinzi anakuelekeza ingia pale kwenye Wakala. Ukitaka nikutajieni ATM zenye hii michezo anzeni na ile iliyopo MABIBO OILCOM karibu, Segerea OILCOM. Michezo hii huenda Sambamba na benki zingine hasa ABSA ATM full time zina pesa wateja wanaaambiwa na walinzi wazitumie kuuuuumbe makato yako juu zaidi.
WAkati ni muda, NMB ni benki ya Walipa kodi tunapooona uzembe na uhujumu hatuna budi kupaza sauti.
OMBI: Ifike pahala option ya kutoa LAKI 4 Iwe kwenye screeen as first option. Mnaongeza sana foleni na kuibia watu wasiojua kujaza figure pale ili watoe mikupuo mingi na nyie mpate pesa kisa tu mmeficha figures. Toa ile figure ya elfu 20 weka laki 4 wazi wazi au ifike pahala mlete ATM za kutoa 1 M kwa mkupuo hizi za sasa ni uzembe wa kufikiri sana.
Wkend njema najua nikienda ATM yoyote kupata pesa zangu ni mbinde soon ntachukua maamuzi magumu.
Hongera kwa mwangalizi wa ATM za MLIMANI CITY full time 24 ndio kimbilio hata tulioko Mbagala.